S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 82
Kambuntas ni Kabuntas tu hata kama wapewe elimu ya juu.
Timu ya JK Starz ni bure kama jina lake na sintapenda kuwaita taifa Starz kwani mlitaka sifa zimfuate JK na sasa lawama zinamfuata yeye.
Hawa jamaa wamekwenda Brazil, wametembelea nchi kadhaa za Ulaya na Arabuni wakicheza mechi huku shopping yao kubwa kila wanapotua. Hawakukaa muda mrefu kambini kama timu na kupewa majaribio makubwa ndani ya nchi na timu zetu.
Leo mkategemee ushindi wa bure kwa kufiria tu kwamba Wamakonde hawauwezi mchezo huu...
Taifa Starz ile ya kina Sunday Manara, King Kibaden waliwekwa kambini haswa, walikunjwa toka ktk timu zao na makocha wa hali ya juu toka ktk club zao. Simba ilikuwa Simba na Yanga ilikuwa Yanga ukiacha hizo timu za Mwadui, Pamba, Mseto, Coast Uniun CDM, Kagera yaani mpira ulikuwa mpira hasa. Kila wilaya na mikoani mkoa kulikuwa na ushindani ndani kabla hujafikia ligi kuu.
Matokeo ya ujenzi wa msingi ule uliendelea kwa zaidi ya miaka 10 hadi tukawapokea akina Peter Tino, Mohammed Salim, Adolf, Chama, Omar Hussein, Mogella, n.k.
Mpira umekwisha pamoja na kuwa na wanja kubwa la kileo haina maana wamo!..
Defunk aliyasema haya awali na hata mimi baada ya kuiona mechi katiyetu na Senegal nilisema JK boyz hawana safari!
Hivi huyu karume ana hata bahati na soka kweli? labda angekuwepo Muungwana tungeshinda
Labda tuwalaumu watu wa makanisa na misikiti kwa kutoiombea Stars
Shindwa na
Legea kabisa
Mshikaji naona unafurahia unacheza bila hata kupunzika? unafurahia nini wakati sisi tumefungwa, ujue tunatafuta mtu wa kumbebesha lawama na hatujampata?Labda tuwalaumu watu wa makanisa na misikiti kwa kutoiombea Stars
Hivi huyu karume ana hata bahati na soka kweli? labda angekuwepo Muungwana tungeshinda
Wachezaji wengi katika timu hii hawana hadhi ya kimataifa. Na kiwango cha uchezaji wao ni kidogo mno ukilinganisha na enzi za akina Kitwana Manara, Sunday Manara, Gibson Sembuli, Kibadeni, Willy Mwaijibe, Mohamed Salim, Mohamed Kajole, Adolph Rishard, Maulid Dilunga, Chitete, Jellah wa Mtagwa, Hassan Gobbos, Zamoyoni Mogella, TX # 1 Hamis Gagarino, TX 2 Lilla Shomari na wengine wengi. Miaka hiyo ya nyuma tulikuwa na wachezaji wenye viwango vikubwa mno, tatizo lilikuja kwenye maandalizi. Wangepata huduma kama wanazopewa hawa sasa hivi basi labda mafanikio yangekuwa makubwa mno.
Kusema kweli hata ukiangalia mchezo wa timu yetu kiwango chao cha uchezaji ni kidogo mno. Leo mnaweza kuwaita JK Boys. Wale wa miaka ile walikuwa wanajulikana kama Taifa Stars.
hahahah, hii kaliJamani dua zetu kwa Mungu pia zilimchanganya, wakati wengine tunaomba abariki Taifa star tushinde, wengine waliombea ishindwe ili isisahaulishe mambo ya msingi kwa Taifa letu hasa ufisadi unao endelea!
kwahiyo Mungu kajibu maombi ya kundio moja wapo, tusonge mbele sasa na mpambano wa hao mafisadi kieleweke, ama la tutakosa vyote!
kutafuta mchawi sasa hivi hakusaidii!
Hapa namtetea EL, timu ya taifa iko chini ya TFF ambacho siyo chama cha serikali ni kivipi kiongozi wa serikali alaumiwe kwenye mambo yasiyo ya kiserikali? Kama nilivyosema huko nyuma serikali inafanya makosa makubwa ya kiutendaji kuigharamia timu ya taifa kwani ni chombo binafsi kama ilivyo miss Tanzania. Ushauri ambao niliutoa huko nyuma kama serikali inataka kujihusisha moja kwa moja na timu hiyo iieweke chini ya baraza la michezo la taifa kama nchi nyingi zinavyofanya. Lawama ambazo EL anaweza kuzibida kwa nini wanashindwa kupeleka timu olympic au kwenye michezo ya commonwealth ambayo timu zinatakiwa ziandaliwe na serikali. Kwa hili muacheni EL alalale salama kwa kupata support toka kwa sam.