Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Kambuntas ni Kabuntas tu hata kama wapewe elimu ya juu.
Timu ya JK Starz ni bure kama jina lake na sintapenda kuwaita taifa Starz kwani mlitaka sifa zimfuate JK na sasa lawama zinamfuata yeye.
Hawa jamaa wamekwenda Brazil, wametembelea nchi kadhaa za Ulaya na Arabuni wakicheza mechi huku shopping yao kubwa kila wanapotua. Hawakukaa muda mrefu kambini kama timu na kupewa majaribio makubwa ndani ya nchi na timu zetu.
Leo mkategemee ushindi wa bure kwa kufiria tu kwamba Wamakonde hawauwezi mchezo huu...
Taifa Starz ile ya kina Sunday Manara, King Kibaden waliwekwa kambini haswa, walikunjwa toka ktk timu zao na makocha wa hali ya juu toka ktk club zao. Simba ilikuwa Simba na Yanga ilikuwa Yanga ukiacha hizo timu za Mwadui, Pamba, Mseto, Coast Uniun CDM, Kagera yaani mpira ulikuwa mpira hasa. Kila wilaya na mikoani mkoa kulikuwa na ushindani ndani kabla hujafikia ligi kuu.
Matokeo ya ujenzi wa msingi ule uliendelea kwa zaidi ya miaka 10 hadi tukawapokea akina Peter Tino, Mohammed Salim, Adolf, Chama, Omar Hussein, Mogella, n.k.

Mpira umekwisha pamoja na kuwa na wanja kubwa la kileo haina maana wamo!..
Defunk aliyasema haya awali na hata mimi baada ya kuiona mechi katiyetu na Senegal nilisema JK boyz hawana safari!


Bob...mimi nasema Amen to that...
 
Labda tuwalaumu watu wa makanisa na misikiti kwa kutoiombea Stars

jakesdance.gif

Shindwa na
Legea kabisa


Aaaaiiimeeennn

Brazameni...hii clip imenivunja mbavu sana..lol
 
Hivi huyu karume ana hata bahati na soka kweli? labda angekuwepo Muungwana tungeshinda


Bahati ya Karume ipo kwenye Uwanja wa Amani...

Stars wamejitahidi sana, ukichukulia ni mara yao ya kwanza kucheza mbele ya Umati wa Watu zaidi ya Hamsini Elfu..
 
Mimi simlaumu mtu,ila Tanzania ndivyo tulivyo,hakuna kitu tunachojivunia duniani,kila kitu kilitupita kushoto,soka la bongo bado sanaaaaa,wenzetu Kenya wanajulikana kwa marathon duniani,kwenye mashindano ya juzi juzi yaliyofanyika Osaka Japan,walikua namba 2 duniani kwa kuchukua medali nyingi,huku Tanzania tukiondoka bila chochote.Halafu tulivyofika nyumbani,katika mahojiano wakadai wanariadha wetu wameshindwa kwa
sababu kulikua na joto kali sana.Hivi wakenya walivyokua wakishinda hilo joto hawakulisikia,au walikua na air condition tumboni.Hatui wazi tukishashindwa,maandalizi yetu huwa ni ya pupa.Hapa asilaumiwe mtu tujiulize tuna kimavi gani bongo?
 
Wachezaji wengi katika timu hii hawana hadhi ya kimataifa. Na kiwango cha uchezaji wao ni kidogo mno ukilinganisha na enzi za akina Kitwana Manara, Sunday Manara, Gibson Sembuli, Kibadeni, Willy Mwaijibe, Mohamed Salim, Mohamed Kajole, Adolph Rishard, Maulid Dilunga, Chitete, Jellah wa Mtagwa, Hassan Gobbos, Zamoyoni Mogella, TX # 1 Hamis Gagarino, TX 2 Lilla Shomari na wengine wengi. Miaka hiyo ya nyuma tulikuwa na wachezaji wenye viwango vikubwa mno, tatizo lilikuja kwenye maandalizi. Wangepata huduma kama wanazopewa hawa sasa hivi basi labda mafanikio yangekuwa makubwa mno.

Kusema kweli hata ukiangalia mchezo wa timu yetu kiwango chao cha uchezaji ni kidogo mno. Leo mnaweza kuwaita JK Boys. Wale wa miaka ile walikuwa wanajulikana kama Taifa Stars.

hayo mambo yakutukumbusha enzi za wakati timu ya taifa ilipokua timu halisi yanatutia huzuni. lakini pia wapambe wa JK walitaka kila timu inaposhinda tuiite JK Boys lakini ikifungwa kwenye magazeti yao wanaandika "Taifa stars yafungwa" lakini ikishinda wanaandika kwa mbwembwe nyingi "JK Boys yafanya kweli! tumewastukia kila kizuri wanataka kiwe cha JK
 
Jamani dua zetu kwa Mungu pia zilimchanganya, wakati wengine tunaomba abariki Taifa star tushinde, wengine waliombea ishindwe ili isisahaulishe mambo ya msingi kwa Taifa letu hasa ufisadi unao endelea!
kwahiyo Mungu kajibu maombi ya kundio moja wapo, tusonge mbele sasa na mpambano wa hao mafisadi kieleweke, ama la tutakosa vyote!

kutafuta mchawi sasa hivi hakusaidii!
 
Jamani dua zetu kwa Mungu pia zilimchanganya, wakati wengine tunaomba abariki Taifa star tushinde, wengine waliombea ishindwe ili isisahaulishe mambo ya msingi kwa Taifa letu hasa ufisadi unao endelea!
kwahiyo Mungu kajibu maombi ya kundio moja wapo, tusonge mbele sasa na mpambano wa hao mafisadi kieleweke, ama la tutakosa vyote!

kutafuta mchawi sasa hivi hakusaidii!
hahahah, hii kali
 
Kifupi Ushindi wa kutupeleka Ghana haukuwa karibu hata kidogo!..Ila tulipewa tumaini na wadau wa CCM kuweka matumaini pale pasipokuwa na uwezekano hata mdogo..

Kabla ya mchezo wa jana hali halisi ilikuwa:-
Tukiondoa timu 12 zilizokwisha Qualify Tanzania tulikuwa tukigombea ktk nafasi 3 (tatu) zilizobaki na sisi tulikuwa na point 8, chini ya Sudan 12 na Uganda 11 na Togo 9. Tazameni chat hii kisha mtakuja jua kwamba tunadanganywa sana.. Yawezekana yote haya yanatokana na sisi kutofuatilia Ukweli bali kuwasikiliza viongozi wetu kuwa wao ndio wakweli... wengine akina sisi tunatakiwa kuleta Ushahidi.

Tuliokuwa tukigombea nafasi tatu ni kama ifuatavyo:-
Sudan wana point 12; Uganda wana point 11; Togo point 9, Zambia wana point 8, Algeria point 8, Eritria point 8, Tanzania point 8; Eq. Guinea point 7, Botswana point 7.

Kwa hiyo tulichokuwa tukiomba ni nafasi ya tatu tu kwani hata kabla mpira wetu kuanza Uganda walikwisha shinda... Hivyo kuwafanya Sudan na Uganda tayari kunyakua nafasi mbili kati ya tatu..na mategemeo yetu ni Togo ifungwe,Zambia ifungwe, Algeria ifungwe Eritrea ifungwe na sisi kama tutashinda iwe zaidi ya magoli 4 mtungi!..Hapa hope yetu ilikuwa wapi hasa?
 
ndugu zangu hapa hamna wa kumlalamikia,,tukubali tukatae hicho ndio kiwango chetu wajameni,,naomba niwakumbushe hata ushindi tuliokuwa tukipata ulikuwa ni wa miujiza

1.game na BUKINAFASO kumbukeni ushindi ulitokana na walivyojifunga wenyewe,,
2.game na UGANDA tulishinda kweli lakini mpira ulikuwa mbovu kabsa jamani,,mungu atupe nini jamani marefa tumewalinda wametusaidia hatubebeki,,NGOMBE WA MASKINI AZAI AKIZAA BASI KILEMA""MAOMBI WALISHAOMBEWA SANA KAKA,,ILA UKIENDA KWENYE MAOMBI KUOMBA UFANIKIWE MTIHANI HUKU UJASOMA UKIFELI HAKUNA WA KULALAMIKA HATAKA
 
Kocha wa timu ya Taifa aliletwa mahsusi kwa ajili ya kuipeleka Tanzania Ghana kwenye fainali za mataifa ya Africa. Kwa sababu kazi hiyo imemshinda ni matumaini yangu kwamba atafungasha virago vyake haraka inavyowezekana na sisi tuanze kujiuliza kulikoni tumeshindwa kufikia lengo hili bila kupoteza wakati na kuanza kufikiri upya mfumo mzima wa michezo nchini.
 
Baada ya kipigo Taifa Stars, mashabiki wamgeukia Maximo
Na Waandishi Wetu
Kutoka Gazeti la Mwananchi

KWA mara nyingine, Tanzania imeendelea kuongeza miaka zaidi ya kuzikosa fainali za Afrika tangu 1980 baada ya mwishoni mwa wiki, timu yake ya taifa, Taifa Stars kuchapwa bao 1-0 na Msumbiji.

Mchezo huo ulioanyika kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, ulihuzunisha mashabiki 60,000 waliokuwa wameketi kwani uwanja wote uliokuwa umejaa. Stars ilichapwa bao hilo katika dakika ya kwanza na sekunde 28, lililowekwa kimiani na Tico Tico baada ya ngome ya Stars kujichanganya.

Mwananchi iliyokuwa ikivinjari maeneo mbalimbali ya majukwaa wakati wa mapumziko na baadaye ya mpira kumalizika, baadhi ya mashabiki walipokea kipigo hicho kwa mawazo tofauti.

Baadhi walidai kuwa uwezo wa Maximo umefikia kikomo na kwamba amekuwa akiamini wachezaji fulani bila kuwajaribu wengine ambao wanaleta mabadiliko baada ya kuusoma mchezo kwa muda mrefu.

Shabiki mmoja aliyekuwa amekusanya wenzake wakati wa mapumziko nyuma ya majukwaa, alisikika akisema Maximo alikuwa na kila sababu ya kumtoa Mecky Maxime na nafasi yake kuchukuliwa na Erasto Nyoni.

"Angalia Mecky, alishapoteza mwelekeo, ilikuwa amtoe na nafasi yake acheze Nadir Haroub 'Canavaro' asimame na ile namba 10 yao (Dario)...," alisikika shabiki huyo. Dario alikuwa mwiba kwa Stars.

Shabiki mwingine alisikika akisema kuwa Maximo ameachiwa mno kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine hukosea. "Inatakiwa apewe ushauri...hata mkuu wa brigedi pamoja na ukubwa wake, wakiwa vitani, askari wadogo humshauri pia..."

Huku akiwasha sigara yake wakati wa mapumziko, mmoja wa mashabiki wa Stars alisema ipo haja ya kutengeneza kwa nguvu timu za vijana na kuachana na wachezaji waliopo kwani hawafundishiki tena.

"Maximo bonge la kocha, tatizo wachezaji wetu..., sasa mtu anabaki yeye na kipa, hapo utasema kocha!?....angalia mchezaji sehemu ya kutoa pasi anaanza kupiga chenga, utasema kocha? Tatizo hatuna msingi wa vijana," alisema shabiki huyo huku akiendelea kuvuta sigara yake.

Baadhi ya mashabiki walidai kuwa kufungwa kwa Stars ni kutokana na kukosekana kwa Maximo katika benchi la ufundi kwani walikuwa wakishindwa kutoa maamuzi.

"Tatizo Maximo hakuwepo, anajua sana kusoma mchezo. Wale wamechelewa kutoa maamuzi ya kumuingiza Joseph Kaniki mapema baada ya kuona wachezaji wa Msumbiji wanatumia nguvu.

"Kaniki ana nguvu, wamechelewa kumuingiza, muda mfupi alioingia ameonyesha vitu, sasa angeingia mapema!?," alisema shabiki huyo. Kaniki aliingia dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Said Maulid.

Baada ya filimbi ya mwisho, mashabiki mbalimbali walikuwa wakidai Maximo amekuwa na misimamo ambayo wakati mwingine haina maana kwa kuwa lengo ni kujenga timu moja yanye nguvu.

Msumbiji imezima ndoto za Tanzania kwenda Ghana mwakani na hata hivyo, ni Senegal pekee iliyofuzu kutoka kundi la saba. Msumbiji imefikisha pointi tisa na kushika nafasi ya pili, Tanzania ya tatu ikiwa na pointi nane wakati Burkina Faso imeshika mkia baada ya juzi kutandikwa mabao 5-1 na Senegal.

Kwa upande mwingine, mashabiki wameigeukia TFF wakiitaka kujiuzulu mara moja kwa kushindwa kufanikisha safari ya Ghana. "Ni wakati wao kuonyesha kweli na wao limewakwaza na kujiwajibisha wenyewe," alisikika shabiki mwingine.

Kabla na baada ya mchezo huo, Maximo alisema kuwa kushindwa kwa Stars si mwisho wa program zake kwa kuwa kuna mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini, 2010.

Mechi za awali zitaanza mwezi ujao wakati Tanzania itaanza moja kwa moja hatua za makundi baadaye Novemba.
 
Hapa namtetea EL, timu ya taifa iko chini ya TFF ambacho siyo chama cha serikali ni kivipi kiongozi wa serikali alaumiwe kwenye mambo yasiyo ya kiserikali? Kama nilivyosema huko nyuma serikali inafanya makosa makubwa ya kiutendaji kuigharamia timu ya taifa kwani ni chombo binafsi kama ilivyo miss Tanzania. Ushauri ambao niliutoa huko nyuma kama serikali inataka kujihusisha moja kwa moja na timu hiyo iieweke chini ya baraza la michezo la taifa kama nchi nyingi zinavyofanya. Lawama ambazo EL anaweza kuzibida kwa nini wanashindwa kupeleka timu olympic au kwenye michezo ya commonwealth ambayo timu zinatakiwa ziandaliwe na serikali. Kwa hili muacheni EL alalale salama kwa kupata support toka kwa sam.
 
kwanza timu yenyewe haikuwa inacheza km inataka kwenda ghana kwani ni aibu kuona timu ya taifa haiwezi kupiga hata pasi tano?

bora tulivyofungwa tuendelee na mambo mengine

cha kufanya kwa sasa ni kuwekeza zaidi kwa timu za watoto wadogo kama walivyofanya timu ya taifa ya nigeria under 17 kwani wameweza kucheza kitimu zaidi mpaka dk 120 dhidi ya uhispania na kutwaa kombe kwa mikwaju ya peneti

kwa hiyo tuachane na hiyo mijitu isiyofundishika tuwekeze zaidi kwa vijana wadogo hapo ht sauzi 2010 tutaweza kwenda

ni hayo 2
 
Natamani kuwaona wachezaji kama akina Peter Tino, Zamoyoni Mogella,,, waliokuwa at any time (t), wanafahamu kwa nini wao ni washambuliaji na kwa nini wamepewa jezi na. 9 au 10... kwa kifupi moja ya woga wangu wa kushinda jana ni kukosekana kwa watu ambao nawaamini kama walivyokuwa hao waheshimiwa hapo juu!!!

Ni mchezaji gani wa taifa stars ya sasa unamwaminia kwamba kwenye mechi tatu, at least atakuwa na goli moja?
 
Hapa namtetea EL, timu ya taifa iko chini ya TFF ambacho siyo chama cha serikali ni kivipi kiongozi wa serikali alaumiwe kwenye mambo yasiyo ya kiserikali? Kama nilivyosema huko nyuma serikali inafanya makosa makubwa ya kiutendaji kuigharamia timu ya taifa kwani ni chombo binafsi kama ilivyo miss Tanzania. Ushauri ambao niliutoa huko nyuma kama serikali inataka kujihusisha moja kwa moja na timu hiyo iieweke chini ya baraza la michezo la taifa kama nchi nyingi zinavyofanya. Lawama ambazo EL anaweza kuzibida kwa nini wanashindwa kupeleka timu olympic au kwenye michezo ya commonwealth ambayo timu zinatakiwa ziandaliwe na serikali. Kwa hili muacheni EL alalale salama kwa kupata support toka kwa sam.

Si ndiye huyu kule Bungeni wakati wametoka Burkina Faso alitamba kwamba ni matunda ya sera za CCM ndio maana inafanya vizuri? Kumbe ikishinda ni matunda ya Uongozi wake ila ikishindwa yeye hahusiki!!!!
 
Viwango vya hawa watoto vilikuwa vidogo, lakini kutokana na wehu wa CCM na media zao, waliweza kuwabebesha majina makubwa zaidi ya uwezo wao. Na hayo ndio matokeo ya dhambi hiyo.

I hope watu wataendelea kupeperusha bendera za nchi kwenye baskeli na mabanda ya kuuza dagaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom