Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
825
Kwa mtazamo wangu nadhani ZITTO na bosi wake wanastahili lawama kuwa kuwaweka watu bize mpaka tukasahau kuwahudumia vijana wetu

Tusisahau kuwa kuna habari KARAMAGI inawezekana ali saboteji mechi

LOWASA naye lawamani kwani wakati watu wa KAMATI wanamtafuta alikuwa anzunguka mikoani bola sababu ya msingikp_95.jpg


lakini mnaruhusuiwa kumwaga lawamazenu humu

msiandike magazeti tafadhalini
 
Mimi namlaumu Makamu wa Rais Dr Shein yaani wenzie wote wanafuatilia timu kwenda kambini na kwenye mechi yeye hata kutoa salam hajawahi kutoa!

Hivi baina yake na Boss wake ni nani alie busy zaidi?
 
Mimi sijafuatilia mechi ilikuwaje, lakini inawezekana tulianika zaidi mipango yetu ya maandalizi wakati wenzetu walikaa kimya. pengine walishatusoma kabla ya mechi.

Inauma kufungwa tena ukifungwa nyumbani
 
Nafikiri matokeo haya si mabaya sana kwani, yanatufanya turudi kwenye hoja za msingi. Hii safari haikuwa yetu, cha kufanya ni kujipanga na kuwa na long term programmes sio zimamoto kama hii. tujenge timu ya 2010, ni muda mzuri sana. Football is costing tusitake cheap.
 
Mimi namlaumu Makamu wa Rais Dr Shein yaani wenzie wote wanafuatilia timu kwenda kambini na kwenye mechi yeye hata kutoa salam hajawahi kutoa!

Hivi baina yake na Boss wake ni nani alie busy zaidi?

masatu.....

nafikiri dr shein yupo Uk kwa matibabu,tusilaumu ndio safari.

mie naomba kusema yafuatayo......

one.....unajua lazima tukubali kuwa kuna kosa nafikiri limefanyika kuwa sisi mafunzo yetu wa-tz tulikuwa kila kitu mambo hadharani mara leo ohh tupo ulaya etc,lkn tulikuwa hatujui nini mambaz wanafanya ninietc ktk matyarisho juu ya game hii.

two....na zaidi nahisi inawezekana bado stars walikuwa wanaona mambaz watakuwa wale wale walotoka nao draw kule msumbiji etc,lkn inaonekana jamaa wamebadilika sana na kujitayarisha vilivyo.

three.... inawezekana wachezaji wetu walikuwa na tension kubwa sana,lkn upande wa pili wenzetu walikuwa tayari kuyapokea matokeo ya iana yoyote ile KUFA KUPONA.

four....inawezekana mambaz walikuwa wanafuatilia kwa umakini sana matayarisho ya kambi ya stars etc inawezekana hata walikuwa wametuma watu wao huko ulaya kuwaangalia taifa stars walipokuwa nje kwa mechi za kirafiki,lkn upande wa pili sisi tulikuwa bizi na siasa za bongo,leo mara karamagi,kesho ZITTO,kuufungua uwanja mpya etc.labda suala rahisi tuwaulize stars jee tokea wamemaliza game na msumbiji wamewahi harta kuwaangalia tena ktk video etc?

five....tupuunguze sifa na majigambo yasokuwa na maana,mf kusema PIGA UA ushindi lazima etc,hahyo yote hayafai.tukae chini tujipangeni tena naamini mambo yatakuwa mazuri tu.

six...suala la kocha nalo ni kitendawili,kila siku timu kubadilikabadilika etc,leo si mnaona tumeenda na wachezaji fulani fulani ulaya,basi after 3wks utasikia timu imepanguliwa na wengine wameachwa na wengine wameletwa etc,hii inasikitisha sana yaani hatuna au hatuangalii mbali,kwa maana hiyo m-brazili anatakiwa apewe vijana wachanga awafunze na sio wachezaji wameshakuwa watu wazima etc.

huo ni mtazamo wangu tu washikaji,is not end of the LIFE.tukaeni chini wapi tumekosea tukjireebsiheni naamini tutafika tu mola akipenda.TUPEANE POLE SOTE.sio muda mwafaka kumlaumu EL,NK,RA,KAMATI YA STARS ISHINDE etc.

wekend njema kwa nyote jamani.
 
....huo ni mtazamo wangu tu washikaji,is not end of the LIFE.tukaeni chini wapi tumekosea tukjireebsiheni naamini tutafika tu mola akipenda.TUPEANE POLE SOTE.sio muda mwafaka kumlaumu EL,NK,RA,KAMATI YA STARS ISHINDE etc.

Tusimsingizie Mungu ktk mambo kama haya.... ni lazima tujue kuwa jitihada yashinda kudra...
 
Kambuntas ni Kabuntas tu hata kama wapewe elimu ya juu.
Timu ya JK Starz ni bure kama jina lake na sintapenda kuwaita taifa Starz kwani mlitaka sifa zimfuate JK na sasa lawama zinamfuata yeye.
Hawa jamaa wamekwenda Brazil, wametembelea nchi kadhaa za Ulaya na Arabuni wakicheza mechi huku shopping yao kubwa kila wanapotua. Hawakukaa muda mrefu kambini kama timu na kupewa majaribio makubwa ndani ya nchi na timu zetu.
Leo mkategemee ushindi wa bure kwa kufiria tu kwamba Wamakonde hawauwezi mchezo huu...
Taifa Starz ile ya kina Sunday Manara, King Kibaden waliwekwa kambini haswa, walikunjwa toka ktk timu zao na makocha wa hali ya juu toka ktk club zao. Simba ilikuwa Simba na Yanga ilikuwa Yanga ukiacha hizo timu za Mwadui, Pamba, Mseto, Coast Uniun CDM, Kagera yaani mpira ulikuwa mpira hasa. Kila wilaya na mikoani mkoa kulikuwa na ushindani ndani kabla hujafikia ligi kuu.
Matokeo ya ujenzi wa msingi ule uliendelea kwa zaidi ya miaka 10 hadi tukawapokea akina Peter Tino, Mohammed Salim, Adolf, Chama, Omar Hussein, Mogella, n.k.

Mpira umekwisha pamoja na kuwa na wanja kubwa la kileo haina maana wamo!..
Defunk aliyasema haya awali na hata mimi baada ya kuiona mechi katiyetu na Senegal nilisema JK boyz hawana safari!
 
Wachezaji wengi katika timu hii hawana hadhi ya kimataifa. Na kiwango cha uchezaji wao ni kidogo mno ukilinganisha na enzi za akina Kitwana Manara, Sunday Manara, Gibson Sembuli, Kibadeni, Willy Mwaijibe, Mohamed Salim, Mohamed Kajole, Adolph Rishard, Maulid Dilunga, Chitete, Jellah wa Mtagwa, Hassan Gobbos, Zamoyoni Mogella, TX # 1 Hamis Gagarino, TX 2 Lilla Shomari na wengine wengi. Miaka hiyo ya nyuma tulikuwa na wachezaji wenye viwango vikubwa mno, tatizo lilikuja kwenye maandalizi. Wangepata huduma kama wanazopewa hawa sasa hivi basi labda mafanikio yangekuwa makubwa mno.

Kusema kweli hata ukiangalia mchezo wa timu yetu kiwango chao cha uchezaji ni kidogo mno. Leo mnaweza kuwaita JK Boys. Wale wa miaka ile walikuwa wanajulikana kama Taifa Stars.
 
Ebu tufanye tathmini ya kweli, first brow ilianza jana wakati wachezaji walipopiga picha na rais wamevaa Kandambili, mimi nilianza kupata mashaka kutokea hapo. Pili tukienda kwa mtido wa probability, trial mechi karibu zote Taifa star ilipoteza ukiacha waliocheza na wamanga uswis na Yoso wa uganda, sasa nyie mlitegemea maajabu gani tena kama kila siku walikuwa wanafundishwa na bado wanakosea? Mjue trial marches count when assesing possibility for a team to win. Lakini cha msingi this indicates aina gani ya leadership tulionayo, mafanikio ya kila kitu ni process sio event, hakuna kinachowezekana overnight, kwa hiyo na uchumi wa kikwete anao tengeneza leo kwa kujaza watu mabilioni ni sawa na kujaza puto upepo,we need to learn na matokeo ya taifa sends a very big message.
 
Hivi huyu karume ana hata bahati na soka kweli? labda angekuwepo Muungwana tungeshinda
 
Waungwana naungana na wadau wote kutoa masikitiko kwa kushindwa mechi muhimu usiku wa leo lakini kama wasemavyo asiekubali kushindwa si mshindani.
Jambo moja sote tunakubaliana pasi na kikomo cha shaka kuwa soka la nchi yetu limekuwa, limekuwa sana kiasi sasa tunachukuliwa kwa dhati na vyombo vya habari vya nje k.v. BBC na wengineo waliokuwa wakiripoti kwa ukaribu habari ya mechi ya leo.
Kiwango cha soka cha Stars kimekuwa sana kiasi wachezaji waliong'ara katika mechi hizo na ziara za Ulaya sasa wamepata mikataba ya majaribio kwenye soka la kulipwa la Ulaya kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika.
Tumefanya vizuri, kama alivyopata kusema Rais JK alipokuwa London,''Tulikuwa kichwa cha Mwendawazimu sasa ni Vinyozi'' lakini kama tujuavyo kinyozi hunyolewa....
Naam sasa kutokana na matunda makubwa tuliyopata,tumeshinda mara mbili, kutoa draw mara mbili na kufungwa mara mbili sio mafanikio haba, sasa tunatazamika katika soka.... Kama ni mgonjwa amesharuhusiwa hospitali muda na anapona taratibu.
Kushindwa huku kusituvunje moyo...Kushindwa kubaya na ni rahisi kutupa lawama kwa huyu ama yule lakini haitusaidii katika mikakati ya muda mrefu. Tujipange twende mbele.We are getting ready to strike again, We have shown the world that Tanzania is a force not to be ignored, NOW LETS PLAN AHEAD AND SHOW THE WORLD THAT FOR TAIFA STARS....THE BEST IS YET TO COME!!!
 
Hivi huyu karume ana hata bahati na soka kweli? labda angekuwepo Muungwana tungeshinda
Siyo swala la bahati, ni ufundi wa timu. Timu yetu ingekuwa na ufunzi wa kutosha wasingeteteleka na bao hilo walolofungwa dakika za kwanza kabisa.

nadhani ninakubalina kabisa na Bubu kuwa miaka ya hivi karibuni tumekuwa hatuna wachazji wa uhakika kutokana na hadhi ya mpira yenyewe. Kinachoitakiwa ni kuendeleza uzi huu huu ili kusudi baada ya miaka minne hivi tuweze kupata timu nzuri tena. Ninadhhani kuwa juhudi za serikali kuboresha mchezo wa mpira na juhudi za kocha Maximo ni nuri ila zimekuta gogo liko bondeni kabisa. Itahitaji muda wa kutosha kulivuta hadi juu.
 
Saidi Yakubu,
Nitakubali maneno yako kama una maana kwamba kiwango cha mpira wetu kimepanda baada ya kudondoka. Yaani tulikuwa + 7 tukarudi hadi - 2 na sasa tumeanza kupanda hadi kufikia +3. Lakini kupanda huku kumeanza wakati wa mwinyi kisha tukashuka tena hapo katikati.
Kumbuka tu nchi nyingine zote kiwango chao pia kimepanda kiasi kwamba Rwanda wanaweza kabisa kutupiga mabao. Kuweka sawa msemo huu tumeisha pigwa sana. Yaani hapa east Africa hatuwezi kujihesabu kama ndio wa kuogopewa kama ilivyokuwa miaka ile.
Haya maswala ya kusajiliwa nje nadhani utakumbuka kwamba Sunday Manara ni miongoni mwa waafrika wa kwanza kucheza mpira wa kulipwa nje akiwa pamoja na Mohammed Polo wa Ghana. Na kwa sababu utaratibu wa zamani FAT ulikuwa hauruhusu wachezaji wetu kutoka ndio maana ilichukua miaka mingi sana, nakumbuka mwaka 1985 kuweza kupeleka wachezaji nje, unajua tena Ujamaa ulikuja na mengi. Lakini hakuna kitu bob, kila nchi kiwango cha mpira kimepanda bado sisi ni tairi lanyuma tukijaribu kufukuza tairi la mbele.
Kupanda kwa kiwango cha mpira huanzia ktk shina la mchezo huu, na kama bado tunapuuza mashindano ya shule zetu za msingi, secondary, vyuo na hata madaraja madogo ambayo ndio chimbuko la wachezaji basi kuanda huku ninguvu ya soda.
Mimi nafikiri kama kuna ubinafsishaji wa kitu basi mpira ndio ungechukua nafasi ya kwanza ili wachezaji wawe waajiriwa kabisa wa timu zao. Iwe full time job hasa kwa timu za daraja la kwanza na ligi kuu badala ya kutegemea kupanga mstari kila asubuhi mlangoni kwa mhindi kusubiri kukatiwa kitu.
Mpira bado kabisa ni shamrashamra zilizokuzwa kuonyesha maendeleo kutokana na Uwanja ulojengwa zaidi ya hapo hatuna timu... Yaani Mozambique wamekiweka zaidi yetu, sisi pasi mbili ya tatu mpira hatuna.
Control yenyewe tunaomba Mungu maanake mtu akipata mpira kitu anachofikiria ni kukimbia tu kuelekea golini na pasi zote hutolewa mbele iwe umekabwa ama laa. Sikuona hata sehemu moja wakianza nyuma baada ya kushindwa kupata mwanya wa kupenya ngome. Akina tenende kibao (mpira wa Ugokoni) utafikiri hawakufundishwa. Duh! Noma mjomba nonaaaaaaa.
 
Saidi Yakubu,
Nitakubali maneno yako kama una maana kwamba kiwango cha mpira wetu kimepanda baada ya kudondoka. Yaani tulikuwa + 7 tukarudi hadi - 2 na sasa tumeanza kupanda hadi kufikia +3. Lakini kupanda huku kumeanza wakati wa mwinyi kisha tukashuka tena hapo katikati.
Kumbuka tu nchi nyingine zote kiwango chao pia kimepanda kiasi kwamba Rwanda wanaweza kabisa kutupiga mabao. Kuweka sawa msemo huu tumeisha pigwa sana. Yaani hapa east Africa hatuwezi kujihesabu kama ndio wa kuogopewa kama ilivyokuwa miaka ile.
Haya maswala ya kusajiliwa nje nadhani utakumbuka kwamba Sunday Manara ni miongoni mwa waafrika wa kwanza kucheza mpira wa kulipwa nje akiwa pamoja na Mohammed Polo wa Ghana. Na kwa sababu utaratibu wa zamani FAT ulikuwa hauruhusu wachezaji wetu kutoka ndio maana ilichukua miaka mingi sana, nakumbuka mwaka 1985 kuweza kupeleka wachezaji nje, unajua tena Ujamaa ulikuja na mengi. Lakini hakuna kitu bob, kila nchi kiwango cha mpira kimepanda bado sisi ni tairi lanyuma tukijaribu kufukuza tairi la mbele.
Kupanda kwa kiwango cha mpira huanzia ktk shina la mchezo huu, na kama bado tunapuuza mashindano ya shule zetu za msingi, secondary, vyuo na hata madaraja madogo ambayo ndio chimbuko la wachezaji basi kuanda huku ninguvu ya soda.
Mimi nafikiri kama kuna ubinafsishaji wa kitu basi mpira ndio ungechukua nafasi ya kwanza ili wachezaji wawe waajiriwa kabisa wa timu zao. Iwe full time job hasa kwa timu za daraja la kwanza na ligi kuu badala ya kutegemea kupanga mstari kila asubuhi mlangoni kwa mhindi kusubiri kukatiwa kitu.
Mpira bado kabisa ni shamrashamra zilizokuzwa kuonyesha maendeleo kutokana na Uwanja ulojengwa zaidi ya hapo hatuna timu... Yaani Mozambique wamekiweka zaidi yetu, sisi pasi mbili ya tatu mpira hatuna.
Control yenyewe tunaomba Mungu maanake mtu akipata mpira kitu anachofikiria ni kukimbia tu kuelekea golini na pasi zote hutolewa mbele iwe umekabwa ama laa. Sikuona hata sehemu moja wakianza nyuma baada ya kushindwa kupata mwanya wa kupenya ngome. Akina tenende kibao (mpira wa Ugokoni) utafikiri hawakufundishwa. Duh! Noma mjomba nonaaaaaaa.
1. Maandalizi yetu ya soka bado hayajazingatia ukweli halisi, SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI na hili ndio inatakiwa sasa tuonyeshe kushughulikia zaidi ikiwa kweli tunataka kufanikiwa. We can't emphasise this enough.


2. Viwango vya FIFA vya hivi karibuni vimeonyesha tumevuka kwa kiasi kikubwa orodha yao kutokana na performance yetu kwenye mashindano yaliyomalizika jana ingawa hatufuzu. Tumefanya vizuri generally kiasi kwamba sasa FIFA wametuingiza moja kwa moja katika mechi za makundi ya kuwania kwenda South Africa badala ya kuanza mwanzo kabisa kama ilivyokuwa, na hii ni kwa sababu tumeonyesha jitihada kubwa ya kufufua soka.

3. Kubinafsisha SOKA? Not a solution I believe kwani sijaona nchi iliyofanya hivi, pengine unazungumzia kuwa na soka la kulipwa? Kama ni hivyo nadhani itakuwa ni wazo zuri kutekelezwa, jambo moja inabidi litajwe hapa nalo ni UTAWALA BORA KATIKA CHAMA CHETU CHA SOKA TFF pamoja na matatizo ya hapa na pale, I am impressed na uongozi wa Tenga katika kipindi kifupi cha uongozi wameweza kuwa na mikakati inayoonekana ya kuinua Soka, wameweza kuondokana na nadharia kuwa TFF ni kijiwe cha ulaji na kufanya kazi, tuseme kuwa wamekuwa very professional katika kazi zao na hili tuwaonyeshe kuwa tunawaunga mkono....YES yapo mengi ya kufanikisha na kufanyia kazi kama vile Managing uwanja wa Taifa [sina hakika kama ni kazi ya TFF moja kwa moja!], kusuka upya kikosi chetu, kuimarisha ligi KUU yetu, kurejesha mapenzi ya wananchi katika SOKA [kwenye hili tumeliona kwa kiasi kikubwa] na mengineyo kadhalika...

3. SOKA LA KULIPWA sijaielewa pointi yako hasa, labda uifafanue kiasi lakini kwa kufanya vizuri kwenye mashindano haya tumeweza kugenerate interest ya ma-scout duniani...Tukumbuke ni kutokana na mafanikio yetu ya hivi karibuni ndio tuliweza kupata mialiko toka Uswizi na Denmark, vijana hapa London na kwingineko kwa uzalendo wao walipeleka mascout huko na though it's early days lakini najua tuna wachezaji kadhaa wamekuwa spotted na wanakwenda majaribuni....tunawaunga mkono na nina hakika kwa ziara ya Taifa Stars nje ingawa bado hatujapata eye catching matches za global audience lakini we are getting there...

4. SOKA KUWA FULL TIME JOB....I am up for this kwani umasikini wa wachezaji unawaangusha sana, careful planning is needed here and hopefully we will get there..tukumbuke kuwa ni sponsorship deals ndio huinua vipato vya timu na wachezaji, tuwatie moto wenye makampuni na matajiri watangaze biashara zao kupitia soka kwa vilabu mbali mbali...hapa tunaweza kuajiri vijana na kupromote soka yetu, SERENGETI kwa kufadhili TAIFA STARS na VODACOM kwa kufanya vivyo hivyo kwenye LIGI KUU ni mfano mzuri sana...


Nadhani the best way is to be optimistic na kutoa credit when one is due...
 
Wale vijana hawajaiva kisychologia always kuchangamka kwao ni mpaka game lichanganye bila kujua kuwa kila dk mpirani ni muhimu.
Alafu hawana munkari kabisa na game angalau kidogo Canavaro,Kaniki na Mecky ingawa uzee unamnyemelea.
Otherwise tuwajenge kisaikologia wajue kuwa mpira ni kazi na wacheze kwa kujituma kama walivyofanya dk 20 za mwisho ingekuwa vivyo ivyo toka mwanzo.
Ila aluta continua huu ni mwanzo na tusitarajie mafanikio ghafla after all at mwaka bado
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom