S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 82
Kambuntas ni Kabuntas tu hata kama wapewe elimu ya juu.
Timu ya JK Starz ni bure kama jina lake na sintapenda kuwaita taifa Starz kwani mlitaka sifa zimfuate JK na sasa lawama zinamfuata yeye.
Hawa jamaa wamekwenda Brazil, wametembelea nchi kadhaa za Ulaya na Arabuni wakicheza mechi huku shopping yao kubwa kila wanapotua. Hawakukaa muda mrefu kambini kama timu na kupewa majaribio makubwa ndani ya nchi na timu zetu.
Leo mkategemee ushindi wa bure kwa kufiria tu kwamba Wamakonde hawauwezi mchezo huu...
Taifa Starz ile ya kina Sunday Manara, King Kibaden waliwekwa kambini haswa, walikunjwa toka ktk timu zao na makocha wa hali ya juu toka ktk club zao. Simba ilikuwa Simba na Yanga ilikuwa Yanga ukiacha hizo timu za Mwadui, Pamba, Mseto, Coast Uniun CDM, Kagera yaani mpira ulikuwa mpira hasa. Kila wilaya na mikoani mkoa kulikuwa na ushindani ndani kabla hujafikia ligi kuu.
Matokeo ya ujenzi wa msingi ule uliendelea kwa zaidi ya miaka 10 hadi tukawapokea akina Peter Tino, Mohammed Salim, Adolf, Chama, Omar Hussein, Mogella, n.k.
Mpira umekwisha pamoja na kuwa na wanja kubwa la kileo haina maana wamo!..
Defunk aliyasema haya awali na hata mimi baada ya kuiona mechi katiyetu na Senegal nilisema JK boyz hawana safari!
Bob...mimi nasema Amen to that...