Shock absober | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shock absober

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NewDawnTz, Jan 3, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hellow wanafamilia wenzangu, Heri ya Mwaka Mpya kwenu wote.

  Huu ndio ujumbe nilionao kwa wale ambao wako kwenye ndoa na wale walioko kwenye mahusiano kwa mwaka huu wa 2011.

  Maisha ni pilikapilika na tunatumia muda wetu mwingi kwenye pilikapilika hizi nje ya familia zetu katika kuhakikisha zinaendelea kuwa imara kwa kuhakikisha mahitaji ya msingi yanakuwepo.


  Hata hivyo pilikapilika hizi huwa hazituachi salama hata kidogo, huwa ziko na mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine huwa zinatuumiza. Mikwaruzano na matatizo katika kazi zetu na katika kutembea kwetu huwa inatokea na matokeo yake hutuchafua mioyo na hata wakati mwingine kututibulia mood zetu tulizonazo.

  Kwa bahati mbaya mara nyingi tunajikuta tunashindwa kuhimili michafuko hii ya moyo kwa itokanayo na pilika za maisha na matokeo yake huenda na michafuko hii hadi majumbani kwetu. Matokeo yake waathirika wanakuwa ni familia.

  Mfano baba anarudi na mihasira na michafuko ya moyo na anamalizia kwa mke, mke nae anamalizia kwa mtoto, mtoto nae anamalizia kwa mbwa, mbwa nae anamalizia kwa paka, paka nae anamalizia hasira kwa kuku na katika purukushani za paka na kuku mwisho wake wanamwaga sufuria ya maji ya kuoga ya baba na kwa hasira mzunguko unaanza tena. Hii ni vicious cycle inayoleta makovu kwenye mahusiano yetu mengi.

  Kwa kuzingatia hili, ili kuepuka pilika hizi zisiathiri mahusiano yetu, ni lazima tuwe na naman ambayo michafuko ya moyo na kihisia ya pilika zetu za kazi ibaki njiani na wala isifike majumbani mwetu. Hapa ndipo tunapokutana na kitu ninachoweza kukiita RELATIONSHIP SHOCK ABSOBER.


  Wengi wenye magari tunakifahamu vema kifaa hiki na namna ambavyo kinatusaidia katika kuhakikisha magari yetu yanaeendelea kuwa salama hata yanapopita kwenye njia mbovu (rough roads). Maisha yetu nayo, kama yalivyo magari yetu, pia hupita kwenye rough roads na hovyo umuhimu wa kufunga shock absorber ni muhimu sana kama ilivyo kwenye gari yako. Kama huna gari waulize wenye nazo jirani yako ni kitu gani kinatokea unapoendesha gari huna shock absorber?

  Nini hii shock absober? Naomba niseme wazi kuwa shock absober sio pombe au aina nyingine ya kilevi cha kukupotezea mawazo kwa muda. Hivi vimethibitika kutokusaidia matatizo bali wakati mwingine kuyachochea zaidi. Kwa tafsiri ya article yangu hii, shock absorber ni binadamu, mtu mwaminifu ambae kwa uwazi na uaminifu atakusaidia kushusha hectic za pilika za maisha ili zisidhuru mahusiano yako.

  Kanuni za Shock absorber wako.

  1. Asiwe partner wako (mke au mume wako): Wengi wetu tunawafanya wake au waume kuwa ndio shock absorber zetu. Hili ni kosa kubwa. Hata wengi wanapoamua kuoa wanamawazo ya kuhitaji watu wa kuwamwagia matatizo wanayopitia, say kazini. Lakini uzoefu unaonesha kuwa wanawake au wanaume (hasa wanawake) wamekuwa wakiathirika sana kwa kutumiwa kama shock absober za partners wao. Hii hupelekea kuchafuka mioyo. Kwa mfano siku za awali nilikuwa namtumia wife kama shock absorber na baadae nikagundua nikizungumza nae juu ya mfanyakazi fulani alienitibua siku hiyo kazini basi na yeye anachafuka moyo na huenda hata akataka kujenga kachuki na huyo mtu.
  Sio biashara unafika tu nyumbani unaanza (tena wengine mbele ya watoto) lile lijamaa kazini lishenzi sana lile, mi nakuambia likiingia kwenye 18 zangu litanijua mie nani. Mwenzako ankuuliza, nini tena baba (mama) unamwambia we acha tu!! hadi hapo umemuwekea kitu akilini ambacho kitamjengea kitu kingine kisichokuwa na manufaa na mwisho yanapozidi moyo unaota kutu...madhara tunayajua.

  Mke wangu huwa namuambia tu nikiwa nimeshapata suluhu na moyo wangu umetulia uko safi na akiwa anaona tabasamu langu badala ya ndita. huwa namuambia, mama kuna jamaa kidogo ofisini leo mambo hayakuwa sawa lakini tumesameheana na tumeweka sawa na sasa tunachapa kazi kama kawaida tena urafiki wetu umezidi wa kwanza. Presenting in a positive way baada ya kusaidiwa ku-solve na Shock absober wako

  2. Mtu mwenye “Mbawa” kama zako (Shock absorber sio marital Counselor): Mara nyingi kwa wale walioko kwenye ndoa huwa tuna watu ambao ni washauri wetu wa masuala ya ndoa. Hawa ni watu wazima na waheshima kwenye jamii tulizonazo tuliowachagua wenyewe au kuchaguliwa na wengi wetu wakitumia viongozi wao wa dini. Hata hivyo kwa kanuni ya uzoefu wangu wa muda mfupi kwenye mahusiano na huyu binti mrembo nilienae, inaonesha wazi kabisa kuwa Shock absorber haifai kuwa huyu mshauri wako wa ndoa. Shock absorber ni mtu wa kumkimbilia mara kwa mara mambo yanapokutibukia wewe na kukufanya kuwa kwenye mood inayoweza kuathiri ndoa au mahusiano yako. Huyu mshauri wa Ndoa abaki kuwa mshauri wakati ambao umeshindwa kuhimili shocks na matokeo yake umezipeleka kwenye familia na sasa uhusiano uko mahali tata. Shock absorber ni kuzuia yasifike kwenye familia (Kinga) wakati mshauri wa ndoa ni kuwasaidia kuweka mambo sawa na kurekebisha yaliyokwisha kuingia kwenye ndoa (Tiba)
  Kwa mantiki hiyo hapo juu, shock absorber lazima awe ni mtu mnaelewana vema, rafiki wa karibu sana na wewe ambae pia unamuona kuwa na heshima na hawezi ku-take advantage kwa muweweseko wako akitegemea ‘kidondokacho mtini’ hakifai kwa mti ila cha muhimu kwa muota jua chini ya mti. Itapendeza akiwa mshikaji wako wa karibu sana maana inapasa iwe ni mtu ambae ukifika kwake unauhuru wa kutosha wa kusema yote. SI MNAJUA TENA KUONGEA NAKO TIBA!

  3. Mtu mwenye kifua:
  anahitajika mtu ambae gari yako ikiingia rough road unaweza kumkimbilia mkazungumza mambo then akawa na kifua cha kuweza kuyatunza bila kuyabwagwa kwa wengine. Lazima umchague kwa makini na uwe na uhakika ya kuwa ni mtu mwenye kujiheshimu na mwenye usiri (kuweza kutunza mambo kifuani


  4. Ongea na mwenza wako juu yake
  : Ni muhimu mwenza wako amfahamu mtu unaemkimbilia wakati unapotibuka moyo na hutaki yeye atibuke. Hii itasaidia mke wako kujua kuna mtu wa muhimu ambae anafanya uhusiano wenu unaenda vizuri na kama ukiw ana mambo yaliyopinda unamfata kwa kukusadia kurudisha mood. Ikiwezekana ongea na mwenza wako juu ya kusudi la kuwa nae kama shock absorber (yaani umuhimu wake) na kasha mjadiliane ili nae aone na kujithibitsha kuwa mtu unaemchagua ni mtu sahihi.
  Binafsi nilikaa na best tukazungumza, nikamweleza juu ya umuhimu wa kuwa na huyu mtu na madhara ya kutokuwa nae ikiw ani pamoja na kumchafua moyo wake kwa michafuko ambayo inaweza kumtdhuru na baadae nikamwambia ni nani ninaempendekeza kwa nafasi hiyo nay eye akaridhia kwa kule kugundua kuwa huyu mtu analiweza jukumu hili. Mara nyingi huwa nakuja nae nyumbani na wife anamwambia anamshukuru kwa kuwa mtu wa muhimu kusaidia uhusiano wetu kuwa sawa maana machafu yote anachuja na kwenda kutupa kabla ya kufika kwake
  Pia ni lazima ukishamteua Shock Absorber wako umwite na kumweleza (inapendeza zaidi kama itakuwa mbele ya partner wako) ni kwa nini umeamua kumteua na ni nini umuhimu wake kwako na kwenye uhusiano wako na partner wako na pia kwamba unatarajia atawasiadia kufanya vema jukumu hilo (kama una maonyo au maangalizo muhimu unaweza kumpa pia)
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  Nasikitika nimechoka na bibie anataka tutoke kidogo na hivyo siwezi endelea kutoa vi-point zaidi juu ya shock absorber lakini wadau wenye uzoefu zaidi watawaongezea.

  [FONT=&quot]
  Angalizo tu ni kuwa makini na uteuzi wako wa Shock absorber usijeweka ya Mchina ukalia kesho au ukaweka ya Grand Premio kwenye Volvo, itakula kwako na mie simo!


  [/FONT]
  [FONT=&quot]Happy Relations in this new year 2011[/FONT]
   
Loading...