Shivji, Ulimwengu kuwasha moto wa Katiba Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shivji, Ulimwengu kuwasha moto wa Katiba Dar

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 13, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  Shivji, Ulimwengu kuwasha moto wa Katiba Dar


  na Nasra Abdallah


  [​IMG] KONGAMANO kubwa kuhusu mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Januari 15, mwaka huu.
  Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), litawashirikisha wadau mbalimbali wakiwamo wananchi wa kawaida, makatibu kutoka vyama mbalimbali vya siasa, wasomi na viongozi wa asasi za kiraia.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti na Mratibu wa Makongamano wa Udasa, Dk. Kitila Mkumbo, alisema mada kuu katika kongamano hilo ni haja, maudhui na mchakato wa Katiba mpya.
  Alitaja sababu hasa ya kongamano hilo na kusema kuwa wanalifanya pia kutokana na wadau wengi wa demokrasia na maendeleo kutoa wito wa kuandikwa upya kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
  Hata hivyo alisema kumekuwa na kusigana juu ya mchakato unaofaa kufuatwa katika kufikia Katiba mpya na kuongeza kuwa wananchi wengi wamekuwa wakihoji nini hasa matatizo ya Katiba iliyopo na maadhui gani yawekwe katika Katiba hiyo mpya.
  “Hivyo basi lengo kuu la kongamano hili ni kutoa fursa kwa wananchi kuelewa misingi mikuu ya Katiba ya sasa na kutafakari kwa kina haja, maudhui na mchakato wa kupata Katiba mpya.
  “Katika kufikia lengo hili, tumewaomba na wamekubali wananchi wawili waliobobea na wenye uzoefu wa muda wa kupigania demokrasia ili wawe wazungumzaji wakuu.
  “Wananchi hao ni Profesa Issa Shivji, Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Jenerali Ulimwengu wa gazeti la Raia Mwema,” alisema mratibu huyo.
  Kwa mujibu wa Dk. Mkumbo, wote hao wanafanana kwa jambo moja kwamba wametumia zaidi ya nusu ya maisha yao katika kupigania haki za wanyonge Tanzania na katika Bara la Afrika kupitia maandishi, machapisho na mihadahara inayoibua hisia, matumaini na wakati mwingine hasira.
  Alisema pia kuwa watu hao ni miongoni mwa Watanzania wachache wanaoelewa historia ya mapambano ya kidemokrasia na ya kijamii ya Watanzania na Bara la Afrika kwa ujumla.
  Alisema kwamba ni matarajio yao kuwa kongamano hilo litatoa mwongozo kuhusu maudhui na mchakato mwafaka katika kufikia Katiba mpya yenye kubeba matakwa na utashi wa Watanzania.
  Pia alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Katiba na Sheria, ni miongoni mwa waalikwa katika kongamano hilo, ambapo aliwaomba wananachi bila kujali elimu zao kujitokeza kwa wingi.
  Naye Mwenyekiti wa Udasa, Dk. Mushumbuzi Kibogoya, alisema kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano mengine, na kwamba mwaka huu utakuwa ni wa makongamano ya Katiba.
  Dk. Kibogoya alisema kwa kuwa suala la uundwaji wa Katiba mpya linahitaji umakini ni vyema wananchi wakashirikishwa kwa karibu, kwani bila hivyo Katiba mpya inaweza kuja kuwa mbovu kuliko iliyopo sasa.
  Alitoa tahadhari kwamba kufanyika kwa kongamano hilo si kuandika Katiba bali ni msingi wa kuandika Katiba, ambapo wananchi wataweza kuelezwa ni mapungufu gani yaliyoko kwenye Katiba ya sasa na kuweza kuchangia yale wanayoona yaongezwe kwenye Katiba au kuondolewa.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  Hawa wasomi ni vyema wangejikita katika utaratibu upi unafaa katika kuandika katiba shirikishi kati ya Tume ya Raisi au Mkutano wa kikatiba kama wanajaribu kutoa mapendekezo yao juu ya katiba iwaje wanapoteza muda wao..................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  BAADA ya malumbano, mijadala mbalimbali kuhusu Katiba Mpya ya nchi na Rais Jakaya Kikwete kuridhia kuwa nayo, wasomi nchini wamejipanga kutoa mchango wao.

  Hatua hiyo imetokana na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), kuandaa makongamano endelevu ya kujadili mchakato wa Katiba hiyo.

  Kwa mujibu wa Udasa, makongamano hayo yatafanyika kwa mwaka mzima ambapo pamoja na mambo mengine, haja na maudhui ya Katiba iliyopo na mpya vitajadiliwa kwa kina.

  Katika Kongamano la kwanza litakalofanyika Januari 15 kuanzia saa nne asubuhi pamoja na mambo hayo, pia ubaya na uzuri wa kuundwa Tume ya kushughulikia uratibu wa Katiba vitajadiliwa.

  Suala la uundwaji wa Tume alilisema Rais Kikwete alipotoa hotuba yake ya salamu za Mwaka Mpya mwishoni mwa mwaka jana, ambapo aliridhia mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya na kueleza kuwa ataunda Tume kufanikisha hilo.

  Wakizungumza na waandishi wa habari jana chuoni hapo, viongozi wa Udasa akiwamo Mwenyekiti wake, Dk Mashumbusi Kabogoya, Makamu Mwenyekiti, Dk Kitila Mkumbo na mwakilishi wa wanajumuiya hiyo, Dk Azaveli Lwaitama, walisema kongamano hilo linatarajiwa kutoa mwongozo wa namna nzuri ya upatikanaji wa Katiba mpya.

  Akijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua kama kongamano hilo halina mwelekeo wa kumwingilia Rais katika utekelezaji wake wa kuunda Tume Huru ya kushughulikia mchakato wa Katiba, Dk Kabogoya alisema," tutazungumzia ubaya na uzuri wa Tume, hatumwingilii Rais kwa namna yoyote, maana sisi tutazungumza kitaaluma, na sidhani kama Rais atawaza hilo kwa namna ninavyomfahamu."

  Akifafanua zaidi, Mratibu wa Kongamano hilo, Dk Mkumbo alisema, "hata hivyo Tume
  ikiteuliwa na mtu mmoja, si Tume shirikishi hiyo, kwa kuwa itapaswa kuwajibika kwa aliyeiteua, Tume shirikishi inateuliwa kwa kushirikisha."

  Dk Mkumbo bila kubainisha tume hizo, alisema nchi hii ina historia ya tume nyingi zilizoundwa kwa kazi maalumu kama hiyo, lakini mwisho wa kazi walipaswa kuwajibika kwa aliyewatuma na si kwa wananchi kama inavyopaswa kufanya Tume shirikishi.

  Katika hilo, alisema ndiyo sababu ya kuwapo kongamano hilo ambalo ni ufunguzi wa makongamano endelevu kama hayo, ya kuchambua kwa pamoja, haja ya Katiba mpya, maudhui, ubaya na uzuri wa Tume na kuhadharisha kuwa jukwaa hilo halitakuwa na mwekeleo wa kutetea chama chochote cha siasa.

  Kwa mujibu wa Dk Kabogoya, mwaliko umetolewa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Katiba na Sheria, vyama vya siasa na vya kiraia na wananchi wa kawaida wenye nia ya kujifunza na si ushabiki wa siasa.

  Dk Kabogoya aliongeza kuwa watakaowasilisha mada katika kongamano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah ni Profesa Issa Shivji na Jenerali Ulimwengu.

  Alisema wana mpango wa kurejesha hadhi ya chuo hicho ambacho zamani kilikuwa na makongamano ya kuibua mijadala yaliyokuwa yakihudhuriwa hata na Rais Julius Nyerere, lakini baadaye yalitoweka.

  Awali akielezea mantiki ya kongamano hilo, Dk Kabogoya alisema lengo ni kutoa fursa kwa wananchi kufahamu misingi ya jumla ya Katiba ya sasa, kupendekeza njia bora itakayotumika katika mchakato wa uundwaji Katiba mpya ili kuepuka malalamiko na Katiba isiyo na viwango.

  "Hatuji Jumamosi kutengeneza Katiba mpya, watu wajue hilo mapema, hatuna uwezo huo, ila Katiba yetu ya Udasa imetupa nafasi ya kuibua na kuhamasisha masuala ya kitaaluma, tusipokuwa makini katika hili, tutakuwa na Katiba mbovu kuliko inavyodhaniwa," alisema Dk
  Kabogoya.

  Mwenyekiti huyo wa Udasa alitumia pia fursa hiyo, kubainisha msimamo wa jumuiya hiyo kuhusu Katiba mpya kwa kusema msimamo wao ni Katiba mpya na kuongeza: "Kila mwananchi anahitaji hilo sasa, sisi tutakuwa wa ajabu tukilikataa."

  Lwaitama, alisisitiza kuwa, mustakabali wa Taifa hili uko mikononi mwa wananchi hivyo kuwataka wenye nia ya kufahamu Katiba iliyopo na umuhimu wa mpya kama upo, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kongamano hilo.
   
Loading...