Shirikisho Ndani ya Shirikisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nonda, Jan 7, 2011.

 1. N

  Nonda JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Shirikisho Ndani ya Shirikisho
  Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na
  Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki

  WanaJF na Watanzania wote

  Tunaelewa kuwa Tanzania ni Mwanachama, mshiriki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,

  Katika mchakato huu wa EAC mwishowe ni kuwa na serikali ya shirikisho. Kwa hiyo ni vyema kwa kila mtanzania kulisoma chapisho hili, kupitia link hii.

  http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27

  Utajifunza mambo mengi ya msingi ya Muungano wa Tanzania na pengine kupata mwanga pia juu ya nafasi ya Tanzania katika EAC kwa siku zijazo.

  Chapisho ni refu, kurasa ni nyingi but it is worth spending your time reading it!Utafunguka macho, utapata uelewa wa Muungano wa Tanzania na pia utaweza kutafakari changamoto ya Tanzania katika mchakato wa EAC.

  Hizi ni dondoo chache kutoka chapisho hilo:-

  Kuja kwa Muungano
  Kama tulivyoona katika Sura ya 1, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliundwa tarehe 26 April 1964. Kuelekea mwisho wa mwaka 1964 iliamuliwa kuliacha jina hilo na kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1965 nchi ilichukua jina lake la hivi sasa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (URT). Muungano huu, kwa hiyo, ulizileta pamoja nchi mbili tofauti zilizo huru za Tanganyika na Zanzibar……pg17


  ….Misingi ya Uhalali na Muundo wa Muungano
  Mkataba wa Muungano ndiyo unaoupa uhalali Muungano. Mara kwa mara watetezi wa mkataba huu wameuelezea kuwa ni mkataba wa kimataifa. Kwa mujibu wa utaratibu wa sheria zisizoandikwa, utengenezwaji wa mkataba ni kwa ridhaa ya mkuu wa serikali na mhimili wa utendaji wa serikali, lakini utekelezaji kwa maana ya kuridhia ni suala la bunge......pg22

  ...Kutokupatikana huku kwa nakala halisi ya Mkataba wa Muungano, ile dhana kuwa Mkataba huu ni siri na mada iliyo mwiko kuizungumza, ni jambo la kutia uchungu na linasababisha matatizo, kama wengi walivyosema. Hii inaondoa imani na kuyazidisha matatizo yanayohusiana na Muungano. Kusema kweli hilo ndilo tatizo ambalo hata wanasheria wanauliza ni nini msingi wa Muungano – Mkataba wa Muungano au katiba? Hili linaweza kuwa ni swali lisilokuwa na jibu lakini ni swali linaloonesha kiasi cha kutokuwepo uhakika juu ya uhalali wa kisheria na kikatiba wa Muungano. Ile kuwa huu ni mkataba wa kimataifa na kwa hiyo umesajiliwa na Umoja wa Mataifa huko New York hakuliondoi tatizo hilo……pg25

  …Muundo wa Muungano
  Muundo wa Muungano ni wa serikali mbili na mamlaka tatu tofauti za sheria. Mkataba wa Muungano unaelezea kuwepo kwa Serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar. Ya Muungano ina uwezo wa kisheria wa namna mbili: Wa mambo ya Muungano, na mambo yasiyo ya Muungano ya bara. Serikali ya Zanzibar ina uwezo wa kisheria kwa Mambo ya Zanzibar ambayo si ya Muungano. Hakuna vipengele kuhusu serikali ya Tanganyika; hakuna Rais au bunge liliopo kwa ajili hiyo. Hakuna uhakika juu ya ni muundo gani wa Muungano Mkataba wa Muungano uliufikiria: Mkataba huo ulifikiria kuwepo kwa serikali ya muungano, ya shirikisho, ya muungano wa majimbo au
  utaratibu wa ushirikishwaji? Wengi wanakubali kuwa Muungano si mojawapo ya mifumo hii. Wanauelezea kuwa ni sui generis. Ni muungano kwa baadhi ya mambo lakini si muungano kwa baadhi ya mambo. Baadhi ya watu wanuelezea "upekee" huu kuwa ni kwa sababu ya kutotaka kuudhiwa au kuulizwa chochote juu ya Muungano huo….pg26

  ….Utendaji wa Mgawanyo wa Madaraka na Majukumu
  Usimamizi wa mambo ya muungano umeelezewa na baadhi ya watu kuwa ni wenye matatizo mengi; wanauona kuwa ndiyo tatizo kubwa kuliko yote linaloukabili Muungano. Matatizo haya kwa kiasi fulani yanatokana na matatizo ya kimuundo ambayo yameelezewa hapo kabla…..pg48

  …Kuna masuala ya kiutawala, kwa mfano lile la uhusiano kati ya mawaziri wa Muungano na mawaziri wa Zanzibar. Halafu tena kuna matatizo ya kimuundo na kisiasa ambayo yanahusiana moja kwa moja na utendaji wa Muungano. Haya ni
  pamoja na kutokuwepo kwa muundo wa ndani kujadiliana juu ya matatizo ya Muungano, ya mamlaka tatu zenye uwezo wa kisheria, Zanzibar kusimamia mambo ya Muungano, na serikali ya Muungano kusimamia mambo ambayo si ya Muungano kwa niaba ya bara bila ya kuwepo muundo wowote. Hali za tatizo hili zinaelezewa kuwa
  ni "kuwepo Zanzibar na kutokuwepo Tanganyika", na kwa hiyo kushindwa kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo kati ya serikali ya Muungano na Zanzibar, wakati mazungumzo kama hayo ilibidi yawe kati ya wabia wa asili.
  Suala la msingi linaulizwa na Zanzibar: tunapokuwa na matatizo ya Muungano tunazungumza na nani kwa kuwa Tanganyika imesita kuwepo?.....pg 53/54


  ……Kushindwa kutatua matatizo kunasababishwa pia na mambo ya Muungano kutokuwa wazi kuanzia mwanzo. Mambo hayajadiliwi, si kwa pamoja wala si kwa wanachama wawili wa Muungano peke yao. Hili linaongezeka kwa tuhuma za kuwepo vitisho. Ilielezwa kuwa uongozi wa Tanzania haufurahi kila unaposikia Muungano
  ukijadiliwa. Badala yake kunakuwa na mkono mzito katika kuyashughulikia mambo hayo ili Muungano uendelee kuwa pamoja; matumizi ya mabavu au njia nyingine zisizo za moja kwa moja. Imeelezewa kuwa, mpaka ulipofika urais wa rais Mkapa ilikuwa ni mwiko kuuzungumza Muungano. Matokeo yake ni kwamba watu wa
  kawaida hawana habari za kutosha juu ya taratibu za Muungano.pg 55

  ....Kama ilivyoelezwa, uwezo wa kuanzisha mabadiliko umo ndani ya mikono ya CCM na cha msingi kinachohitajika ni nia ya kisiasa na moyo wa ujasiri. Kikiwa ni chama tawala, kote, Zanzibar na bara , inabidi kiwe na uwezo wa kufanya kitu kama hicho. Jukumu kubwa kama hilo kwa CCM inasemekana kuwa linakwamishwa na "ubinafsi"….pg70/71

  Sasa ni uamuzi wako..nenda kwenye link ujisomee na uongeze maarifa!
   
Loading...