Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeanzisha ligi mpya ya timu za taifa ambayo itaitwa ‘UEFA Nations League’

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
UEFA 2.jpg

Msingi wa mfumo wake ni nini?
  • Mfumo wa 'UEFA Nations League' utahusisha kupanda na kushuka kwa timu hizo. Timu 55 za taifa za Ulaya zimegawanywa kwenye ligi nne kulingana na msimamo wa timu bora za taifa wa UEFA za oktoba 11, 2017
  • Ligi A itajumuisha timu bora za juu wakati ligi D itajumuisha timu za chini kwenye msimamo huo wa timu bora
Ligi A:
Germany, Portugal, Belgium, Spain, France, England, Switzerland, Italy, Poland, Iceland, Croatia, Netherlands
  • Timu zitagawanywa tatu tatu kwenye makundi manne, ambapo mshindi wa kundi atashiriki kwenye fainali yaani nusu fainali, mshindi wa tatu na fainali yenyewe mwezi wa sita 2019 ili kuweza kushinda michuano hiyo. Timu moja ya kuandaa michuano hiyo itachaguliwa mwezi wa 12 miongoni mwa timu zitakazo shinda kutoka kwenye makundi.
  • Timu nne ambazo zitamaliza za mwisho kwenye makundi zitashushwa daraja kwenda ligi B kwa ajili ya michuano ya 2020.
  • Timu za nne za juu za ligi A ambazo hazijafuzu kucheza michuano ya UEFA EURO 2020 watacheza 'play-offs' mwezi wa 3 2020, huku kukiwa na nafasi moja ya kuwa kwenye fainal.
Ligi B:
Austria, Wales, Russia, Slovakia, Sweden, Ukraine, Republic of Ireland, Bosnia and Herzegovina, Northern Ireland, Denmark, Czech Republic, Turkey
  • Timu zitagawanywa tatu tatu kwenye makundi manne. Washindi wa makundi watapandishwa kwenda ligi A huku timu nne za mwisho kutoka kwenye makundi hayo watashushwa hadi ligi C kwa ajili ya michuano ya 2020.
  • Timu za nne za juu za ligi B ambazo hazijafuzu kucheza michuano ya UEFA EURO 2020 watacheza 'play-offs' mwezi wa 3 2020, huku kukiwa na nafasi moja ya kuwa kwenye fainal.

Ligi C:
Hungary, Romania, Scotland, Slovenia, Greece, Serbia, Albania, Norway, Montenegro, Israel, Bulgaria, Finland, Cyprus, Estonia, Lithuania

  • Timu zitagawanywa tatu tatu kwenye makundi manne. Washindi wa makundi watapandishwa kwenda ligi B huku timu nne za mwisho kutoka kwenye makundi hayo watashushwa hadi ligi D kwa ajili ya michuano ya 2020.
  • Timu za nne za juu za ligi C ambazo hazijafuzu kucheza michuano ya UEFA EURO 2020 watacheza 'play-offs' mwezi wa 3 2020, huku kukiwa na nafasi moja ya kuwa kwenye fainal.

Ligi D:

Azerbaijan, FYR Macedonia, Belarus, Georgia, Armenia, Latvia, Faroe Islands, Luxembourg, Kazakhstan, Moldova, Liechtenstein, Malta, Andorra, Kosovo, San Marino, Gibraltar

  • Timu zitagawanywa nne nne kwenye makundi manne. Washindi wa makundi watapandishwa kwenda ligi C kwa ajili ya michuano ya 2020.
  • Timu za nne za juu za ligi D ambazo hazijafuzu kucheza michuano ya UEFA EURO 2020 watacheza 'play-offs' mwezi wa 3 2020, huku kukiwa na nafasi moja ya kuwa kwenye fainal.
UEFA 3.jpg


UEFA Nations League calendar

Group stage draw*: 24 January 2018 – SwissTech Convention Centre, Lausanne

Matchday 1: 6–8 September 2018
Matchday 2: 9–11 September 2018
Matchday 3: 11–13 October 2018
Matchday 4: 14–16 October 2018
Matchday 5: 15–17 November 2018
Matchday 6: 18–20 November 2018
Finals draw: early December 2018
Finals: 5–9 June 2019

UEFA EURO 2020 play-off draw: 22 November 2019
UEFA EURO 2020 play-offs: 26–31 March 2020

Note:
  • Teams in three-sided groups will play on four of the six matchdays
  • Russia and Ukraine will not be drawn into the same group. The same applies to Armenia and Azerbaijan if the current UEFA Executive Committee decisions still apply when the draw is made.
 
Back
Top Bottom