Shirikisho la muungano pasipo washirika

visionary

Member
Aug 26, 2011
41
20
Habari kwenu wanaJF.

Rasimu hii ya katiba ambayo imewasilishwa na ndugu Warioba juzi Jumatatu, imeleta mwangaza mpya kwa watanzania wote wazanzibar na tanganyika. Ama kweli tume ya Warioba imefanya kazi kubwa na inastahili pongezi kutoka kwa kila mpenda maendeleo ya Tanzania yetu. Nimeipitia rasimu hii kwa utaratibu na umakini mkubwa na kugundua utulivu na busara iliyotumika kuiunda ilisahau ama kwa maksudi au bila kujua kuwa Tanganyika haina serikali wa katiba.
Katika kifungu cha (57) katiba inaelezea juu ya muundo wa Jamhuri ya Muungano.

1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni: (a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na (c) Serikali ya Tanzania Bara. (2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na: (a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano; (b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na (c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. (3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo Serikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washirika wa Muungano

Kipengele hiki ambacho ndicho cha muhimu kuliko mengine yote maana ndicho kinachotuambia mipaka na maana ya shirikisho hili kinatambua Jamhuri ya Tanganyika ambayo kimantiki haipo.

Shirikisho hili lina washirika wawili, tanganyika na zanzibar. Sasa mshirika Tanganyika ni yupi na ameshiriki vipi katika uundwaji wa katiba ya Jamhuri ya Muungano?

Katiba hii ya Shirikisho haiwezi kuanza kutumika kabla washirika wake wote kuikubali, yawezekana serikali ya Zanzibar imeshakubaliana nayo lakini je serikali ya Tanganyika iko wapi kuelezea hisia zake kwa hii katiba? Hivi ni kweli maoni yaliyotolewa ni ya watanganyika na wazanzibar au ni ya watanzania na wazanzibar?

Kwa maoni yangu hakuna shirikisho bila washirika na ili hii katiba iwe genuine ni lazima kwanza serikali ya Tanganyika iundwe na iwe na katiba yake. Baada ya hapo wananchi wa tanganyika waulizwe wanataka Muungano uweje na wale wa zanzibar pia. Kama sehemu hizi mbili zitakubaliana basi ndipo kunaweza kukawa na serikali ya shirikisho la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na hii sio kazi ya miaka miwili.
 
Aiseee umenena...Serikali ya Tanganyika haijaundwa ili tutengeneze shirikisho na ni lazima watanganyika washirikishwe kama wanataka au la!
 
Back
Top Bottom