Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) ubunifu wenu uko wapi?

Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) ubunifu wenu uko wapi?

mapinduzi daima

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
1,724
Reaction score
2,709
Ndugu zangu Wananchi,
Awali ya yote polen na pilika za maisha

HOJA:

Baada ya Rais Magufuli kuamuru Makao makuu ya Serikali yahamie Dodoma, watumishi wengi waliokuwa na makazi ya kudumu na wengine waliokuwa wamepanga walihamishiwa mji mkuu

Zoez hili linaendelea had Sasa.

Changamoto;

Kutokuwepo kwa nyumba za kutosha Dodoma , na pia kupanda maradufu kwa Kodi za upangishaji

Watumishi kuishi mbali sana na ofc smbazo nyingi ziko UDOM

Ushauri.

Kutokana na Serikali kutojiandaa kuhusu makaz ya watumishi wake Dodoma (hakuna mpango), yafaa Management ya NHC wawe wabunifu SANA na kuchangamkia hii fursa

Badala ya kujenga nyumba za million 50 hadi 80 na kujarib kuwauzia Watumishi, wajikite kujenga nyumba za KUPANGISHA kwa ajili ya Watumishi wa Umma.

Wajenge nyumba standard mfano apartments na kuwapangishia Watumishi

Huu mradi unalipa na ni quick win

NHC Ubunifu wenu uko wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom