Shirika la ndege la taifa la umoja wa falme za nchi za kiarabu la Etihad limefurahishwa na ufanisi na utendaji wa operesheni zake kwa mwaka wa 2015 zilizowafanikisha kufikia malengo yao ya ukuaji ambapo sasa wanabeba abiria wengi na mizigo mingi zaidi ya awali.
Mwaka jana Shirika lilibeba abiria milioni 17.4, sawa na asilimia 17 zaidi ya mwaka 2014, wakiendesha safari 97,400 za ndege zilizofikisha jumla ya kilomita milioni 467. Hii ni dhahiri kwamba abiria walifurahia huduma hizi na hivyo uhitaji uliongezeka, jambo ambalo lilisisitiza nguvu ya mikakati ya ukuaji iliyowekwa na shirika la ndege la Etihad.
Kwa ujumla, ndege za Etihad pekee zimebeba zaidi ya asilimia 75 ya abiria waliosafiri kwenda na kuondokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi katika mwaka wa 2015. Etihad pamoja na washirika wake walio na ndege zinazofika mji huo mkuu wa UAE wamefikisha jumla ya asilimia 84 ya abiria waliotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.
James Hogan, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Etihad, alisema: “Katika mwaka 2015, tumeweza kuwapa mamilioni ya wasafiri chaguo lenye thamani ya fedha katika usafiri wa anga na tumeleta nguvu mpya ya ushindani katika sekta hii. Yote haya yametokana na huduma zetu zinazokidhi viwango vya kimataifa ambazo pia zimejizolea tuzo mbalimbali. Pamoja na hayo, mashirika mengi yanavutiwa kujiunga nasi na tunazidi kuongeza idadi ya washirika wetu, kukuza ukubwa wa mitandao yetu ili kufika sehemu nyingi zaidi duniani. Hamna shirika lingine lenye kuleta tija na ushindani wa viwango hivi katika sekta hii”.
Katika mwaka 2015, Shirika la Etihad limezindua njia mpya kwenda Kolkata, Madrid, Edinburgh, Entebbe, Hong Kong na Dar es Salaam, pamoja na huduma ya moja kwa moja kwenda Brisbane.
Mwaka jana pia Etihad walianza kutumia ndege aina ya Boeing 787-9 Dreamliner, ambayo ilianza kutoa huduma za ndege za biashara kwenda Washington DC, Zurich, Singapore na Brisbane. Mtandao wa ndege aina ya Airbus A380 umeongeza huduma zake za kuelekea London Heathrow na kuanza safari mpya za kuelekea Sydney na New York.
Mwaka huu, Shirika litaongeza safari zake za kwenda London Heathrow hadi kufikia safari tatu kwa siku hii ni pamoja na mwanzo wa safari mpya za ndege aina ya A380 kufika Mumbai na Melbourne, wakati Boeing 787 itaanza kupaa kwenda vituo vipya vya Düsseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg.
Etihad pia iliongeza mizunguko katika njia za kusafiria 16 zinazotumika hivi sasa ambazo hufika Bangkok, Chennai, Dammam, Delhi, Hong Kong, Hyderabad, Istanbul, Jeddah, Kochi, Kozhikode, Melbourne, Mumbai, Muscat, Seychelles, Tehran na Trivandrum.
Ili kukabiliana na kasi ya ukuaji wake, Shirika la ndege la Etihad liliongeza idadi ya washirika wake mwaka jana. Mkakati huu uliwapa fursa abiria zaidi ya milioni tano kutumia ndege za Etihad, iliyosababisha ongezeko la asilimia 43 ambayo ni abiria milioni 3.5 zaidi kuliko 2014.
Mkakati mwingine ni makubaliano waliyozindua na Shirika la kimataifa la ndege la Pakistan (PIA), wakati Etihad inaendelea kukuza na kuendeleza ushirika wake na mashirika ya Air Serbia, American Airlines, flynas, Jet Airways, Korean Air, NIKI and S7.
Kutokana na hayo, Etihad sasa inawapa fursa abiria wake kuwa katika mtandao utakaowawezesha kusafiri na kusafirisha mizigo kwenda sehemu 600 kwa kuunganisha ndege na moja kati ya washirika wake 197 ama kusafiri na washirika wake wa “codeshare” 49.
Mnamo mwezi wa nne wa mwaka 2015, Shirika la ndege la Etihad lilipata kibali kutoka kwa Ofisi ya Shirikisho la Usafiri wa Anga ya Uswisi (FOCA) kukamilisha asilimia 33.3 ya uwekezaji katika shirika la ndege la Darwin, ambazo ni ndege zinazoruka kanda za Uswisi.
Ndege za shirika la Etihad ziliripoti kubeba tani 592,090 sawa na ongezeko la asilimia 4 mwaka hadi mwaka. Mwaka jana, ndege hizi zimebeba asilimia 88 ya mizigo ya bidhaa kuingia na kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abu Dhabi.
Katika mwaka 2015, Etihad imefikisha mizigo vituo vipya sita duniani na sasa huduma hii ya kusafirisha mizigo inapatikana katika jumla ya vituo 96 ambavyo hutumika na abiria wakati wa kusafiri. Shirika limepanua uwezo wake wa kusafirisha mizigo kufika masoko mapya yakiwemo Dakar, Nouakchott na Douala, ambapo imefanya jumla ya vituo vinavyosafirisha mizigo tu kuwa 20.
Kufikia mwisho wa mwaka 2015, Etihad ilifikisha jumla ya ndege 121 (ogezeko la asilimia 9 mwaka hadi mwaka) yenye wastani ya umri wa miaka 5.8- kulifanya kuwa shirika lenye ndege changa na zisizoharibu mazingira kati ya wapinzani katika sekta nzima. Mwaka 2015 Shirika lilipokea Airbus 11 (A380 nne, A321 sita na A320 moja) na Boeing 787-9 Dreamliner nne huku wakiongeza nafasi za kukodi pia.
Ili kuunga mkono mikakati iliyojiwekea ya kukuza mtandao wao duniani, shirika la Etihad litapokea ndege nyingine mwaka huu, zikiwemo Boeing 787-9 tano, A380 tatu na Boeing 777-200 Freighters mbili.
Bwana Hogan alisema: “Tumeingia mwaka 2016 kwa kujiamini kwamba nguvu tulizoonesha awali zitaendelea na zitatumika kuitambulisha Abu Dhabi kama kitovu cha usafiri wa anga duniani.
“Tunaendelea kukabiliana na changamoto, ikiwemo suala la ulinzi wa urithi wa wasafirishaji wakubwa Marekani na Ulaya. Tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuwahakikishia wasafiri wetu kwamba wanachagua kilicho bora kati ya sisi na washindani wetu”.
***MWISHO***
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi,