Shirika la ndege ATCL halijaunganisha akaunti zake na mfumo wa malipo ya serikali GePG hadi leo

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Baada ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya CAG kwenye sekta ya utalii na biashara , yafuatayo yameweza kubainishwa;

1. Shirika la ndege la Taifa (ATCL) halija unganisha akaunti zake na mfumo wa malipo wa Serikali yaani GePG kinyume na kifungu cha 44-6A(1) na 44(2) cha sheria ya Fedha za Umma, sura ya 348 ya mwaka 2001(Kama ilivyorekebishwa na sheria ya marekebisho ya sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2017) ambacho kinahitaji fedha zote za serikali zikusanywe kupitia mfumo wa kieletroniki wa malipo ya serikali GePG.

Hii inaweza kupelekea kukosekana na taarifa za mapato na matumizi ya pesa za Umma na baadae pesa hizi kupotea.

2. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro hutumia GePG kulipia na kukusanya mapato yasiyo ya utalii pekee kama umeme, minara, uwekezaji nk na kwamba Safari Portal ,mfumo wa ukusanyaji mapato ya utalii uboreshwe ili kukusanya mapato yote.

Pamoja na utafauti huo niongeze changamoto moja ya Safari Portal ni kwamba malipo ya wageni yanaandaliwa na kulipiwa Bank kabla ya siku au muda wa wageni kuingia hifadhini, ikitokea mgeni yule haingii hifadhini kwa sababu yoyote ile inakuwa ni vigumu sana kurudishiwa pesa ambazo Tour Operators wanakuwa wameshalipia huduma hiyo.

3. Tanzania tuna maeneo mali kale 131 ambayo yalisha tangazwa kwenye gazeti la serikali ambayo jati yao 4 yapo kwenye urithi wa dunia. Maeneo yanayo changia kwenye pato la Serikali ni 11% tu sawa na maeneo 15.

4. Bodi ya Taifa ya Utalii imeonyesha uwezo mdogo wa kutangaza vivutio na kuuza bidhaa za utalii kwa kuwa na budget ndogo, kukosa technologia na wafanyakazi wenye weledi.

Jumanne Masonda
Mjumbe
Kamati ya Ardhi, Mazingira na Utalii.
Bunge la Wananchi JMT
 
Back
Top Bottom