Ship Brokers-Madalali wa meli

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,945
12,508
Udalali ni shughuli ambayo inafanyika sehemu mbalimbali katika aina tofauti za biashara tangu enzi za zamani.

Ship Brokers-Hawa ni madalali wanaojishughulisha na meli. Wanahusika sana kwenye kukodisha meli, kutafuta mizigo ya meli na uuzaji wa meli.

NAMNA WANAVYOFANYA KAZI
Ship Broker huwa kama kiungo kati ya mmliki wa meli na mkodishaji, mmliki na mnunuzi wa meli au mtu mwenye mzigo.
shipbroker.png


Ship Broker hawa wengi wamefungua makampuni yao na kudili na biashara za ukodishaji wa aina tofauti za meli duniani.

JINSI GANI UFANYE ILI UWE SHIP BROKER
Ili uwe ship broker itakubidi upate elimu ya hii fani katika taasisi husika na utajiunga na brokers company. Kujiunga hakuna ukomo wa kigezo cha elimu mtu yeyote anaweza kajiunga kupata mafunzo.

Wao sana wana amini mtu mwenye uwezo wa kujieleza,ku bargain na mahusiano mazuri ndio vigezo vikubwa.

NAMNA KAZI KILA SIKU ZINAVYOFANYIKA.
Mtaji mkubwa wa hii kazi ni uaminifu, Broker kila muda hucheza na email mpya na siku zinazoingia na kufanya utafiti wapi kuna meli mpya au mizigo mingi.

images (4).jpeg


Kampuni kubwa za Ship Broker duniani
na CEO wake.

Clarksons – Andi Case
RS Platou – Peter Anker
Braemar Shipping Services – James Kidwell
ICAP Shipping – Henry Liddell
SSY – John Welham
Maersk Broker – Jørn Steen Nielsen
Poten & Partners - Michael Tusiani
Gibson – Nigel Richardson.

Miji ambayo biashara hii inafanyika kwa kiwango kikubwa duniani.

London,Singapore,New York,Houston,Athens,Oslo na Hong Kong.

KIPATO CHA MADALALI WA MELI
Wale waliojiriwa katika kampuni za ship broker huwa kwa kuanzia hulipwa mshahara wa USD 3000 anapoendelea kuwa mashuhuri ufika mpaka USD 10,000. Licha ya mshahara kuna kamisheni ambazo ni kubwa kuliko mshahara kutokana na atakavyofanya kazi ya kukodi au kuuza meli.

Kampuni hulipwa na mmliki wa meli na mkodishaji/muuzaji/mnunuzi wa meli 1.5% mpaka 2.5% ya thamani ya kuuza meli au gharama za ukodishaji hiyo meli(freight charges).

MAISHA YA NJE YA MADALALI WA MELI.
Kutokana na kazi yao kuwa na pesa nyingi endapo utakamilisha biashara na kupata kamisheni. Wengi wao kipindi cha mapumziko huenda maeneo ya starehe na anasa duniani kama fukwe za Ibiza,Copa Cabana, Maldives,Patayya na Mauritius.

Angalizo:Hii biashara haifanyiki kwa ujanja kama huku Tanzania,Dalali sana ofisi zao na kuna hatua zote za kisheria hakuna biashara ya kuuza mbuzi kwenye gunia kisha mteja unamkimbia.
 
Duuuh basi hii kazi nzuri
Haihitaji elimu ya ziada, mtu yeyote anaweza kufanya vigezo ni uwezo wako wa kujieleza, ku bargain na kuvutia wateja.

Kwa sisi huku hatuna sehemu ya kutoa mafunzo ya Ship Broker. Hii unasoma online kupitia Lloyd Institute na ukimaliza wao wanakuunganisha kwenye umoja wa Ship Brokers duniani. Na kazi za awali utafanya chini yao.

Kipindi cha nyuma watu walikuwa wanaenda Kenya kufanya mafunzo Kenya.
 
Back
Top Bottom