Shikamoo wewe kipofu uliyeniibia pikipiki na ukaiendesha

feisar wa moro

Senior Member
Mar 17, 2020
191
500
SHIKAMONI/MARAHABAA

STORY YAHUSU: NILIVYOIBIWA BOBABODA MAGOMENI JIJINI DSM

Nipo zangu kijiweni nikisubiri abiria mara paap wanakuja wanaume wawili mmja mtu wa makamo miaka 40/55 amevaa miwani meusi akionekana ni mtu mwenye ulemavu wa macho (kipofu) na mwingine ambae ni kijana Kati ya miaka 18/25 akimsadia kumuongoza njia huku wote wamekamata fimbo moja.

Wamefika kwangu baada ya salamu fupi yule kijana akanambia "oya abiria anaenda Manzese darajani ni shilingi ngapi"? Nikamwambia buku tatu (3000) kipofu na yeye akaongea na kuniomba kwmba nimsaidia ana buku 2 (2000) tu..

Nikakubali nikampakia na kuanza safari mbele kdogo kipofu akaangusha fimbo yake akaniambia "kijana samahani fimbo yangu imenianguka" fasta nikasimama nikageuka nyuma kweli nikaiona haikuwa mbali na niliposimama kama hatua 15 hivi ila ni katikati ya barabara nikaona bora niende kwa miguu

Sasa kumbe mluguru mimi nilijichanganya kwenda kumuokotea fimbo yake bila kuizima boxer yangu.kudadeq hatua kama kumi hivi nikasikia chombo inapigwa race ya kufa mtu KUGEUKA NYUMA MTUMEEE KIPOFU ANAENDESHA PIKIPIKI MWEEEE
 

K.Msese

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
1,634
2,000
kuna boxer mwenzio, ila yeye ni Mhaya. inaonyesha alipendwa na abiria wa kike, ikawa kama wapenzi, maana huyo dada alikuwa akimkumbatia na kujilaza mgongni kwa boxer (bodaboda wa boxer) kila mara wakiwa wote. watu around walijua ni mpenzi wake..

Mapenzi ama ukaribu wao ulidumu kwa kam siku tatu nne hivi, baadaye ikaanza tabia yule dada anafundishwa kuendesha pikipiki na boxer. Dereva yupo nyuma, dada yupo mbele lakn anashikiwa usukani na dereva, na kwa jinsi dada alikuwa smart alijifanya slow leaner. mara zote walikuwa wakifundishana kuendesha kwnye uwanja wa mpira wa mtaani.

Sasa sijui walikubalianaje, lakn kwa maelezo ya boxer ni kuwa, dada aliomba ajaribu kuendesha mwenyewe wakt jamaa yupo chini baada ya kuwa ame improve kuendesha. Kilicho fuatia ilionyesha dada alikuwa na skills kubwa ya kuendesha kuliko jamaa, maana alitia gia mfululizo na manjonjo kibao, akatembea.. pikipiki ilienda mazima.

huwa tukimwona, tunamtania hadi leo, kikweli alichanganyikiwa sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom