Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza pesa nyingi shows za ndani...

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,386
Eric Shigongo, mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa kampuni ya Global Publishers amelalamika kitendo cha Diamond kuwatoza mapromota wa nyumbani kiwango kile kile anachowatandika wale wa nje.

Shigongo-530x357.jpg

Shigongo ni mmoja wa waandaji wakubwa wa matamasha kupitia ukumbi wake wa Dar Live na huenda miaka ya hivi karibuni ameshindwa kuzimudu gharama za kumchukua kutumbuiza.

Kupitia Instagram, haya ndio mambo aliyoandika:

Kama nilivyosema wakati naanza kwamba ninampenda sana Diamond kwa sababu amekuwa mtu wa kujituma,aliyeng’ang’ania kutoka kwenye umasikini mpaka kuwa na mafanikio aliyokuwa nayo.

Ieleweke kwamba sipo kwa ajili ya kumsema, kumponda, hapana, nipo kwa ajili ya kumshauri kama mdogo wangu, rafiki yangu kwa hiyo naomba nisieleweke vibaya.Diamond Platnumz kwao ni Tanzania, ni mwanamuziki wa Kitanzania na hata wapenzi wake wengi wanaomsapoti kwa nguvu nyingi ni Watanzania ambao asilimia kubwa vipato vyao ni vya chini mno. Wengi wanatamani kumuona akifanya shoo katika ardhi yake ya nyumbani, lakini badala yake wamekuwa wakimuona mara nyingi akifanya shoo Marekani, Ulaya, Nigeria,Afrika Kusini, kwenye Mashindano ya Afcon na sehemu nyingine nyingi ambazo ni nje ya Tanzania, mahali alipozaliwa na kuthaminiwa, mahali ambapo aliweza kujijazia mashabiki wengi.

Mashabiki zake wanahitaji shoo, kumsoma kwamba amejenga nyumba, amenunua au amepata watoto na Zari si kitu ambacho mashabiki wanakihitaji zaidi kutoka kwake, wanachohitaji ni kuona shoo zake kwa wingi kama kilivyokuwa kipindi cha Moyo Wangu, Kamwambie na nyimbo nyingine.

Ni kweli ana jina kubwa, ana mashabiki wengi, amepambana sana kufika alipokuwa lakini kwa upande mwingine anatakiwa kuangalia gharama za shoo zake hasa anapofanya nchini Tanzania,kwa watu ambao walimfanya leo kujulikana zaidi kama Diamond na si Naseeb Abdul.

Leo, Diamond anafanya shoo kwa dola 55,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100. Hii inamaanisha kwamba kwa mtu kama mimi,nikimchukua Diamond kwa gharama hiyo inamaana kwamba nitataka niingize kiasi kikubwa kama faida, kwa hiyo badala ya kufanya shoo Dar Live, Diamond Jubilee au sehemu nyingine, nitaihamishia shoo yangu Mlimani City na kufanya kiingilio cha shilingi elfu hamsini.

Swali la kujiuliza, je, yule bodaboda anayepiga sana nyimbo za Diamond ataweza kuingia kwa kiingilio cha shilingi elfu hamsini? Yule kijana anayatafuta riziki kwa kuingiza nyimbo za Diamond kwenye simu za wateja ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Jibu rahisi ni kwamba hatoweza.

Ni lazima afikirie ajue kwamba gharama anazotoza sehemu nyingine ziwe tofauti na Tanzania, au azifanyie gharama hizo kampuni kubwa za mitandao ya simu na vinywaji lakini si mtu binafsi.

Mara nyingi amekuwa akisema huko nje analipwa zaidi ya milioni mia moja, je, ni halali hata kwa Watanzania wenzake waliomfanya kuwa hapo alipo kuwatoza kiasi hicho cha fedha huku huyo anayemchukua akitarajia shoo yake iingiwe na watu wa hali ya chini wenye kiu ya kumuona?

Labda Naseeb Abdul mwenyewe ndiye aliyelazimisha ada hii, kama si yeye bali ni mameneja wake (Salam na Tale) basi wanamshauri vibaya na matokeo yake kutofanya shoo nyumbani kwake (Tanzania) kutamfanya apoteze kupendwa na mashabiki sababu ya umbali alioutengeneza.

Ikumbukwe kwamba watu hununua bidhaa ya mtu wanayempenda, mtu akichukiwa na bidhaa zake hususiwa.Diamond na WCB ni biashara ya Naseeb Abdul, hivyo basi Naseeb Abdul hatakiwi kuthamini sana fedha na kusahau mashabiki zake waliomfanya kuwa hapo alipo.

Kifike kipindi awaeleze mameneja wake “HAPANA! TANZANIA NI NYUMBANI NA HAWA NI NDUGU ZANGU”

Basi kama waandaaji watashindwa kumudu gharama zake sababu Naseeb ni mfanyabiashara kama mimi, basi afanye shoo ya kujitolea (Charity show) kama tuliyofanya naye huko Tandale huko Mwanza, Kigoma, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro kwenye viwanja kwa kiingilio cha shilingi 3000 na kisha fedha hizo azipeleke kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na hiyo itamfanya kupendwa na mashabiki na kumfanya kwenda juu kimuziki.

TOFAUTI NA HAPA, MBELE YAKE KUNA SHIMO, UKIMYA WAKE BILA SHOO NYUMBANI UTAMZAMISHA!!
 
huyu shigongo alizoea kitonga kutoka kwa wasanii
na kuwanyonya sasa wasanii wameanza kuamka anaanza kuisoma namba..
yeye mbona semina zake za ujasilia mali anatoza pesa nyingi tu wakati ndio zinawahusu watu wa tabaka la chini ili wajikwamue kiuchumi....

tena diamond na wasanii wengine endeleeni kukaza hadi watapike nyongo hawa wanyonyaji..
tena msikubali kupangiwa na mtu sababu wakati mnatunga hizo nyimbo hakuna aliyewashawishi,
wala hakuna aliyewasindikiza studio kurekodi
 
Hahaha we jamaa bhana
 
Hayo maelezo marefu sijayasoma, ila naona kama huyo bwana hizi wiki mbili hatambi kabisa!... Watu wapo busy na nchi yao tu, angetoa kanyimbo angesikika.....astaafu kuimba mapenzi tu
 
huyu shigongo alizoea kitonga kutoka kwa wasanii
na kuwanyonya sasa wasanii wameanza kuamka anaanza kuisoma namba..
yeye mbona semina zake za ujasilia mali anatoza pesa nyingi tu wakati ndio zinawahusu watu wa tabaka la chini ili wajikwamue kiuchumi....

tena diamond na wasanii wengine endeleeni kukaza hadi watapike nyongo hawa wanyonyaji..
tena msikubali kupangiwa na mtu sababu wakati mnatunga hizo nyimbo hakuna aliyewashawishi,
wala hakuna aliyewasindikiza studio kurekodi
Badala ya kumuattack personally ungejaribu kumpinga kwa hoja ingekuwa poa zaidi.
 
Shigongo anajaribu kujivutia biashara upande wake hujui ni vibaya sana kuwa mbali alafu ujirusishe karibu. Diamond na wasafi ni brand tayari na ishakuwa na mashabiki na wateja piah acha kumrudisha dogo nyuma kimaendeleo,, nilijuwa unamshauri aboreshe zaidi ili aweze kupata zaidi,, Dogo nasibu usikubali kufelishwa kiboya komaa kimpango wako anataka akulostishe •
 
kweli bashite kashika hatamu hadi watu wanatafuta pakutokea na hivi habari zake marufuku kutolewa basi tabu tupu
 
Ukweli ni kuwa wafanyabiashara kama Shigongo wameshapitwa uwezo wa kummudu Diamond. Mbona wenzake voda wananunua shoo kwa hela hiyo hiyo halafu wananchi wanalipia buku kumi? Njia ya biashara ya Diamond ya sasa sio ya kutegemea viingilio ni ya kutegemea matangazo ya corporate. Brand inanunua shoo Diamond anapiga hata bure! Shigongo anadhani JayZ alilipwa kutokana na kiingilio chetu?
 
Inabd sasa watambue Diamond kwa sasa ni zaidi ya kusimama mbele ya jukwaa na kuimba Diamond ni influence Diamond ni brand.
 
Ukweli ni kuwa wafanyabiashara kama Shigongo wameshapitwa uwezo wa kummudu Diamond. Mbona wenzake voda wananunua shoo kwa hela hiyo hiyo halafu wananchi wanalipia buku kumi? Njia ya biashara ya Diamond ya sasa sio ya kutegemea viingilio ni ya kutegemea matangazo ya corporate. Brand inanunua shoo Diamond anapiga hata bure! Shigongo anadhani JayZ alilipwa kutokana na kiingilio chetu?
Mwanzako labda anataka amlipe Diamond mil 30 alafu yeye akajaze Darlive kwa 15,000 sasa sijui anataka wakina moses iyobo na kifesi wakale wapi, hapo hapo TRA wanamsubiri
 
Back
Top Bottom