Shigongo adai Diamond anaelekea shimoni, awataja mameneja wake kama chanzo

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,420
30,786
Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ameandika barua yenye ujumbe mzito kwa Diamond kupitia mtandao wa Instagram.

17494084_1668575770114675_4247248564368965632_n.jpg


Kupitia mtandao huo, Shigongo ameandika:

Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo.

Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote.

BRAVO! LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE.

Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.



source : gpl

UPDATE : MAJIBU YA BABUTALE KWA SHIGONGO

MENEJA BABU TALE AMJIA JUU LAIVU ERIC SHIGONGO NA KUANDIKA UJUMBEE HUU
Posted by Williammalecela.com on Saturday, April 01, 2017
16788569_776312742545030_5319073059133456384_n.jpg

Baada ya Eric Shigongo kuandika barua ndefu ya kumuonya Diamond kuhusiana na jinsi anavyowawekea ngumu waandaji wa show za ndani kwa kuwatoza bei zile zile kama anavyowatoza wa nje ya nchi na kuhusisha uongozi wa WCB kuwa ni sehemu ya tatizo hilo, Babutale amejibu.

Tale amefunguka mengi huku akimshutumu Shigongo kuwa na hila ya kuharibu biashara zake kupitia magazeti ya Global Publishers.
Kupitia Instagram, Tale ameandika:
Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya…baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako… siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata…ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali…. tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu…
Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie tume kaa kimya… na kujifanya unazunga eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?….. Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? …na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa….tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe….mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa….yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum’bomoa msanii kupitia magazeti yako…..tafadhali heshimu heshima yetu kwako
…… “Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao…

MAJIBU YA SALLAM


Baada ya kuona post ya yule jamaa mtunzi wa Vitabu ambae sasa ameamua kuchukua kazi ya Utabiri, najua yupo kwenye Kamati ya Serengeti Boys naomba ututabirie matokeo kabisa kama tunachukua Kombe au La! ____________________________ Diamond ana show Leaders Club Tarehe 22 July 2017, halafu ana show zaidi ya 10 kwenye mikoa tofauti nchini mwezi wa Nov-Dec ____________________________ Mwaka Jana Show za Diamond alizofanya Tanzania 1.Mabibo Hostel Kiingilio Bure 2.U-DOM Dodoma Kiingilio Bure 3.CCM Kirumba Mwanza 4.Wasafi Beach Party Dar. 5.Wasafi Festival Iringa. ______________________________ Unachotakiwa kulalamika kuwa kwanini hafanyi Show Dar Live, hapo tungeelewana hata na mie ningekusapoti. ______________________________ : @lukambaofficial
17 hours ago
 
Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ameandika barua yenye ujumbe mzito kwa Diamond kupitia mtandao wa Instagram.

Kupitia mtandao huo, Shigongo ameandika:

Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo. Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha.

Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO!

LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE. Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM.

Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.

Nitaendelea kesho.


Unadhani kwanini Shigongo anahisi Sallam na Babutale wanampoteza Diamond?
 
mimi mwenyewe nashangaa wale kina salaam hawana kazi nyingine za kufanya zaidi ya kufuatana na diamond kila show..

huku ni kumuongezea gharama.. bora awe anasafiri na dancers tu na watu wa kazi..

babu tale nasikia ni meneja wa tip top na madii mbona anakazania kwa diamond tu

salam nasikia mi meneja wa ay mbona huwa amfati fati ay kama diamond.. wanamnyonya mtoto wa watu
 
mimi mwenyewe nashangaa wale kina salaam hawana kazi nyingine za kufanya zaidi ya kufuatana na diamond kila show..

huku ni kumuongezea gharama.. bora awe anasafiri na dancers tu na watu wa kazi..

babu tale nasikia ni meneja wa tip top na madii mbona anakazania kwa diamond tu

salam nasikia mi meneja wa ay mbona huwa amfati fati ay kama diamond.. wanamnyonya mtoto wa watu
diamond ndio kazi yao mkuu
 
mimi mwenyewe nashangaa wale kina salaam hawana kazi nyingine za kufanya zaidi ya kufuatana na diamond kila show..

huku ni kumuongezea gharama.. bora awe anasafiri na dancers tu na watu wa kazi..

babu tale nasikia ni meneja wa tip top na madii mbona anakazania kwa diamond tu

salam nasikia mi meneja wa ay mbona huwa amfati fati ay kama diamond.. [COLOR-RED]wanamnyonya mtoto wa watu[/RED]

Wanamnyonya kitu gani mkuu...?
 
mimi mwenyewe nashangaa wale kina salaam hawana kazi nyingine za kufanya zaidi ya kufuatana na diamond kila show..

huku ni kumuongezea gharama.. bora awe anasafiri na dancers tu na watu wa kazi..

babu tale nasikia ni meneja wa tip top na madii mbona anakazania kwa diamond tu

salam nasikia mi meneja wa ay mbona huwa amfati fati ay kama diamond.. wanamnyonya mtoto wa watu
watu mnafikiria kwa akili za kijima jima!
SASA NYIE KWA MAWAZO YENU DIAMOND YEYE MWENYEWE NDO ANAPANGA AVAE NINI,AONGEE NA NANI,AINGIE MIKATABA IPI,APOST NINI MITANDAONI,VIDEO ZIWEJE,
mnawaza hao walio pembeni yake WANAKULA TU UBUYU!?
 
Nasubiri hoja zake namimi nizichambue...lakini hadi sasa bado sijaona ni wapi atafanikiwa kushawishi hili analo lisema
la kuuza nyimbo zake kwa pesa,yaan bila pesa watu washindwe kusikiliza au kuona video zake...
Hili ni shimo...bado hatujafika huko..
 
meneja bora ni kuhakikisha wasanii wake wanafanya vizuri..

swali makini.. salam ni meneja wa ay, babu tale ni meneja wa tip top yenye wasanii wengi..

mbona hawawaongozi hao wasanii wawe kama diamond na wamebaki kumngangania diamond tu???

number 1 remix nyimbo ambayo imemtoa diamond hao kina salam walikuwa hawapo.. na diamond alimtafuta davido na kumlipa usd 5000 ndio akakubali.. na walionana kwenye fiesta dar ambayo davido alikuja kama top artist

hao mameneja baada ya kuona dogo katoboa wamesusa wasanii wao na wote wamekimbilia kwa diamond.. hawamsaidii hata kulipa kodi ya ofisi ya wcb...

mbona hawafungui ofisi za tip top au wasanii wao wengine..

hii nayo inahitaji digrii kuona wanamnyonya dogo

watu mnafikiria kwa akili za kijima jima!
SASA NYIE KWA MAWAZO YENU DIAMOND YEYE MWENYEWE NDO ANAPANGA AVAE NINI,AONGEE NA NANI,AINGIE MIKATABA IPI,APOST NINI MITANDAONI,VIDEO ZIWEJE,
mnawaza hao walio pembeni yake WANAKULA TU UBUYU!?
 
Unless anazungumzia issue za Diamond kuside na kina Magufuli, CCM ambao mpaka leo Shigongo anajuta kuwafahamu, maana wanamnywesha maji badala ya kumlipa deni.

Otherwise, Shigongo ni moja ya watu waliojaribu sana kumshusha Diamond kisa tu kagoma kuperform kwenye Tamasha la Matumaini kwa hela ndogo.

Shigongo na magazeti yake wamewahi kufanya polls na eti Kiba akaibuka juu ya Diamond, wamewahi kusema Diamond anauza madawa ya kulevya etc etc, na hakushuka.

Ngoja tusubiri.
 
Wanamziki wajanja huwa wanabaidlisha mameneja baada ya mda flan,ni muhimu sana japo ina risk zake
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom