Shida sio mtu bali mifumo ya kiutendaji

Shida sio mtu bali mifumo ya kiutendaji

howardlite

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2016
Posts
248
Reaction score
413
Wapendwa wana jamvi nawasalimu, kwanza niwapongeze kwa hoja nyingi za JamiiForums na michango yenu muhimu kwa maeneo tofauti ya nchi yetu. Mimi ni mmoja wa Watanzania wengi ambao nimepata elimu na taarifa za msingi kupitia jukwaa hili, ni kweli mawazo na michango ni lazima tutofautiane lakini bado tulenge kwenye kujenga, Mwenyezi Mungu awabariki.

Nirudi kwenye hoja, ndugu zangu ni ukweli kuwa nchi yetu kwa vipindi vyote vya uongozi changamoto zilezile zimeendelea kuligharimu taifa letu. Mfano upotevu wa fedha za Umma, matumizi nje ya bajeti, rushwa nk.

Hivi ni kweli shida ni watu wanaoongoza hizo taasisi ndio wote ni wabaya, wabadhirifu sio waaminifu na sio wazalendo kwa watu wao na nchi yao?

Nakubaliana na hoja za kuangalia upya mifumo ya utendaji, kuna uwezekano mkubwa mama akamaliza muda wake tukarudi tulipo sasa.

Bila kubadilisha mifumo inayotoa nafasi za kupigwa hata kama itokee kiumbe nje ya sayari ya dunia hii, hawezi kuondoa changamoto hizi.
 
Back
Top Bottom