Shida humfanya mtu kuwa tapeli!

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,628
9,175
Siamini kama ndugu yangu tuliyekuwa naye pamoja tangu utotoni leo hii kawa tapeli, na muhanga ni mimi mwenyewe (kanitapeli)

Nimewaza sana nikaamua nimuache tu.

Aliyesema usimuamini mtu yeyote hata kama ni mama yako mzazi, wakuu alikuwa sahihi kwa asilimia 100% ,

Napenda kuwapa ushauri wakuu

Zama hizi usimtume mtu akununulie mzigo wa biashara au akuuzie wakati huo wewe ukiwa mbali mfano mkoa mwingine, nenda wewe mwenyewe kanunue mzigo.

Anayesikia na asikie asiyetaka aache

Yamenikuta
 
Simu hapokei kabisa alianza na visingizio naumwa sana pesa nitaituma soon, kapona bado akawa mswahili, mara oooh natuma leo jioni hivi sasa mwezi unaisha kimyaa.
 
Utapeli ni tabia. Narudia tena. Utapeli ni tabia. Wenye shida tuko wengi lakini hatugeuki matapeli. Kuhusu ulivyotapeliwa mimi nadhani ni uzembe wako. Kuna visa vingi sana vya utapeli wa namna hiyo tena kwa watu wanaojuana na wengine ni ndugu vishatokea. Ulikuwa hujasikia? Ulidhani ni utani?
 
Wengi yamewapata.

Kuna rafiki yangu kazini alikopa hela benki kwa kumuamini shangazi yake amtumie mazao awe anauza, kilichotokea ilibidi rafiki yangu aende huko kwa shangazi yake alichokuta ni kichefchef, shangazi aligeuka shangingi hicho kijiji alichoishi alikuwa ndio boss lady kwenye mabaa, pesa za mkopo anazitumia kugawa ofa baa na kichwani ana wigi la laki 3 nyumbani kaweka tv ya milioni.

Rafiki yangu nusu afe ganzi, hakuwa na cha kumfanya ila hadi leo hawana mahusiano mazuri
 
Pole sana.
 
Huyo ni tapeli by nature ulikua humfaham tu hiyo tabia yake. Marafiki hawatapeli wakiwa na shida ila wanakupiga virungu kila baada ya siku kadhaa.
Hivi hawa jamaa janjajanja wanaofinyanga na kulipua virusi duniani halafu hapohapo wanaanzisha miradi yao mikubwa ya viwanda vya teknolojia ya famasia ili kutuuzia chanjo, wao tuwaweke kwenye kundi gani!???
 
IMG_20210130_123255.jpg
 
Huyu ni Mpumbavu, hakuna mahali serikali imeainisha mtu akisomeshwa na serikali lazima ahajiriwe serikalini
Naona unakimbilia kutukana sana. Jiangalie utakuja hivi karibuni kujitukana mwenyewe. Tatizo siyo kuajiriwa serikalini. Tatizo ni kutimka baada ya kuajiriwa. Kwa nini asingekataa tangu mwanzo kujaza fomu za commitments!???
 
Wengi yamewapata.

Kuna rafiki yangu kazini alikopa hela benki kwa kumuamini shangazi yake amtumie mazao awe anauza, kilichotokea ilibidi rafiki yangu aende huko kwa shangazi yake alichokuta ni kichefchef, shangazi aligeuka shangingi hicho kijiji alichoishi alikuwa ndio boss lady kwenye mabaa, pesa za mkopo anazitumia kugawa ofa baa na kichwani ana wigi la laki 3 nyumbani kaweka tv ya milioni.

Rafiki yangu nusu afe ganzi, hakuwa na cha kumfanya ila hadi leo hawana mahusiano mazuri
eti bosslady
 
Naona unakimbilia kutukana sana. Jiangalie utakuja hivi karibuni kujitukana mwenyewe. Tatizo siyo kuajiriwa serikalini. Tatizo ni kutimka baada ya kuajiriwa. Kwa nini asingekataa tangu mwanzo kujaza fomu za commitments!???
Kwanini nijitukane,
Kama alivyoacha kazi alifuata taratibu kuna tatizo mzee?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom