Shida hawataki kugawana sifa

MJ Ryoba

Member
Jun 11, 2017
47
61
Kwa mtizamo wangu upinzani, ccm na serikali yake wote wanafanya jambo jema na wote hawapendi tuendelee kuibiwa na wawekezaji kutoka nje lkn pia wawekezaji wa ndani.

Kinacholeta matatizo ni uchaguzi wa 2020, ccm wakiikubali kazi ya upinzani kwenye madini wanawapalilia njia ya 2020, cdm pia wakiikubali kazi ya jpm wanampalilia njia ya 2020. Hapo ndipo vikumbo vijembe, kuing'ang'ania hoja ya sera ya madini kunapoanzia, na kazia nzima tunayoiona sasa.

Naamini upinzani ungetoa ushauri wao bila kejeri na vijembe kama vile ''uamuzi wa kijinga, uamuzi wa kukurupuka, akili nusu, hii ni hoja yetu, hakuna nia ya kweli, ni siasa tu, ni kick n. k" ushauri wao ungepokelewa na ungetusaidia sana tatizo wangegawana sifa na serikali jambo ambalo hawapo tayari kuliona.

Ccm pia na serikali yake ingefanya inayoyafanya bila vijembe kama vile ''wanatumika, wanatetea wizi, wanatuma vimesaji vya kuomba data, n. k" naamini ingefika sehemu wote tuimbe wimbo mmoja.

Imani yangu ni kuwa upande utakao kubali kugawana sifa na upande wa pili ndio utakao ibuka washindi, upande utakao kubali kuziona na kuzikubari juhudi za upande wa pili utavuna sana 2020, lkn zaidi ya yote hiyo ndio njia bora zaidi ya kutushindia hii vita ya uchumi
 
Wote wako katika kulitetea taifa na maslahi yake.Cha muhimu wawe katika ushirikiano katika mambo ya msingi bila kuweka itikadi za chama
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom