Shibuda, CCM na kauli za utumwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda, CCM na kauli za utumwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzee wa njaa, May 31, 2012.

 1. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HIVI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza vipi kujifananisha na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kulinda na kuheshimu demokrasia?Mimi ni mwanachama wa CCM, lakini nakiri leo hii hatuna hata chembe ya ubavu wa kujifananisha na CHADEMA ambacho tumeshikia bango la kukichafua.

  Ninaandika haya baada ya kuona jitihada za kupindisha ukweli, kuhusu kauli za John Shibuda, mbunge wa Maswa Magharibi kupitia CHADEMA.
  Shibuda amenukuliwa akisema, "…muda wa vyama vya upinzani kukabidhiwa madaraka haujafika." Alisema hivyo Ian Smith, mlowezi wa Zimbabwe, lakini uhuru ulikuja haraka kuliko miaka 1,000 aliyotaka; na "utumwa" ukafutiliwa mbali.

  Lakini mtu anasema haya kwa gharama gani? Kwanza ni matusi kwa wananchi wanaotaka mabadiliko na kwa CHADEMA inayoongoza harakati hizo za kisiasa.
  Nilikuwa mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao cha CCM mjini Dodoma, ambamo Shibuda alitangaza kuwania urais mwaka 2015.

  Alivyoalikwa na alichokisema, ni yeye na viongozi wakuu wa CCM wanaojua.

  Katika mkutano huo, ndimo nilimsikia akitoa kauli za kudhalilisha CHADEMA; chama ambacho anasema anataka kukitumia kupata urais.

  Sasa kinachonisikitisha ni viongozi wa chama changu (CCM), kutoa kauli za kutetea kilichofanywa na Shibuda.

  Huyu anasema CHADEMA inamsakama Shibuda pasipo sababu; sababu ya kusakamwa kwake eti ni kwa kuwa "yeye hatoki Kaskazini." Anaendelea, "…wasimbague Shibuda…Wasitafute visingizio vya kuondoa hoja hii na kumnyanyasa…" Hii ni kauli hatari. Ni dhambi ya unafiki.
  Shibuda huyuhuyu ambaye CCM inataka kubeba sasa, ndiye aliyesukiwa zengwe hadi kuondoka CCM na kujiunga na CHADEMA. Shibuda mwenyewe ni shuhuda.

  Mara kadhaa alizuiwa kugombea nafasi za juu za uongozi, ikiwamo mwenyekiti wa Wazazi.

  Kwenye urais pia, hata kama alikuwa anatania tu, jina lake lilikatwa na Kamati Kuu (CC).
  Katika maisha yake ya kisiasa ndani ya CCM, Shibuda hatasahau kilichompata mwa mwaka 2002 alipokuwa anakwenda Dodoma kwenye mkutano wa chama chake.Akiwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM, uliojumuisha pia uchaguzi, alishushwa kutoka garimoshi mjini Tabora. Kauli iliyotolewa wakati ule dhidi ya kitendo hicho, ni kwamba eti alikuwa anakwenda Dodoma "kuchafua viongozi wa juu wa chama – CCM."John Malecela aweza kuwa shuhuda muhumu wa kilichopo ndani ya chama chake. Yeye mwenyewe amezuiwa kugombea urais mwaka 2005. Hakuzuiwa na vikao vya chama. Ni wakati wa uenyekiti wa Benjamin William Mkapa.Hadi sasa, hakuna kiongozi hata mmoja aliyeeleza sababu za Malecela kutogombea urais.

  Hata mwenyewe anasema hajaelezwa kilichomuondoa kwenye kinyang'anyiro hicho. Hii ndiyo "demokrasia?"
  Thomas Nyimbo, ni shuhuda pia wa kinachotendeka ndani ya CCM.

  Tangu mwaka 2002, Nyimbo amekuwa akizuiwa kugombea uongozi.

  Katika uchaguzi mkuu wa chama mwaka 2007, Nyimbo alijitosa katika kinyang'anyiro cha uenyekiti mkoani Iringa. Alienguliwa na vikao vya chama.
  Mwaka 2005 akajitosa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge jimboni Njombe Magharibi. Akashinda kura za maoni ndani ya CCM. Lakini wenye chama wakamuengua.Ushuhuda mwingine ni upatikanaji viongozi kati ya CHADEMA na CCM. Katiba ya CHADEMA inasema, "Kila mwanachama mwenye sifa ya kugombea nafasi yeyote anaruhusiwa kufanya hivyo," zikiwamo nafasi za mwenyekiti, katibu mkuu, makamu mwenyekiti, naibu katibu mkuu – bara na Visiwani.Ndani ya CCM, Katiba inazuia baadhi ya nafasi kugombewa. Kwa mfano, hakuna anayeruhusiwa kugombea uenyekiti wa chama ngazi ya taifa. Hivyo hakuna mwanachama anayeweza hata kutamka maneno "…nataka kugombea uenyekiti.

  "
  Jina la mgombea mwenyekiti huletwa na "wenye chama," kisha hupelekwa mkutano mkuu kuidhinishwa. Kazi ya mkutano mkuu ni kupiga kura ya ndiyo au hapana kwa jina lililoletwa.

  Basi!
  Mwenyekiti wa chama ndiye "anayeumba;" pia makamu wenyeviti wawili – Bara na Visiwani. Akimaliza kazi ya kuumba hupeleka jina la mhusika kwenye NEC. Kazi ya NEC ni kuidhinisha uteuzi wa mwenyekiti. Hakuna kuhoji. Je, udikteta huu, ndiyo viongozi wanaoita demokrasia?Naye katibu mkuu na naibu wake wawili – Bara na Visiwani – "huumbwa" na mwenyekiti. Yeye ndiye anateua kwa kupeleka majina yao kwenye NEC ili kuidhinishwa. Kazi ya NEC ni kuidhinisha matakwa ya mwenyekiti. Hakuna kuhoji wala kujadili.Ndivyo mwenyekiti wa sasa, Jakaya Kikwete alivyomuumba Yusuph Makamba mwaka 2007 na Wilson Mukama mwaka 2011.

  Mithiri ya kimbunga.
  Kabla ya Makamba kukabidhiwa ukatibu mkuu, Philip Mangula ndiye alikuwa anashikilia nafasi hiyo.

  Bila udikteta wa mwenyekiti, Mangula angeweza kuendelea kutumikia wadhifa wake huo hadi Oktoba 2007 ulipofanyika mkutano mkuu wa uchaguzi ili kukamilisha kipindi chake cha pili cha miaka mitano.
  Hata wajumbe wa CC hakuna anayeruhusiwa kugombea.

  Ni uteuzi wa mwenyekiti. Yeye ndiye anayechomoa majina kutoka miongoni mwa wajumbe wa NEC na kuyapeleka kwa wajumbe ili wayapigie kura.
  Kazi ya NEC, ni kupigia kura jina moja kutoka majina matatu ya wagombea walioletwa na mwenyekiti. Je, uteuzi huu nao unaweza kuitwa demokrasia ya uchaguzi?Ushuhuda mwingine, ni anguko la aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM), makamu wa rais wa Jamhuri na makamu mwenyekiti wa CCM Visiwani, Aboud Jumbe Mwinyi mwaka 1984.

  Alivuliwa nyadhifa zake zote za chama na serikali katika muda wa kufumba na kufumbua na tena ndani ya kikao cha chama chake. Hili amelieleza vizuri katika kitabu chake – The Partnership (Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, miaka 30 ya dhoruba). Uk. VIII.
  Kimsingi siyo kosa kwa Shibuda kutamani urais.

  Siyo kosa pia kutamkia maneno hayo kwenye mikutano ya CCM. Aweza kutoa kauli yake popote pale, hata kwenye klabu ya pombe.
  Nafasi ya CHADEMA katika siasa za sasa nchini inaeleweka. Ndicho chama pekee kilichosalia katika utetezi wa rasilimali za taifa. Ndio kimbilio la waliopoteza matumaini katika utawala wa miaka 50 wa CCM. Huu ni ukweli mchungu kwetu wana-CCM wote.

  Kuruhusu mtu kuvuruga CHADEMA sasa, kwa kukizushia tuhuma za uwongo, ni kutaka kuwarejesha wananchi kwenye utumwa.

  Baadhi yetu hatuko tayari kubeba dhambi hiyo.
  Bali Shibuda anaumwa. Ugonjwa wake ni huu: Ukosefu wa uwezo wa kupima athari ya kauli zake kabla ya kuzitamka.
  Anapenda sifa. Anataka aonekane mwanasiasa makini kuliko aliowakuta upinzani. Huu ni ugonjwa hatari. Nashangaa chama changu kupalilia ugonjwa badala ya kuutibu.

  Source: MwanaHalisi..
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni uchambuzi mzuri
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeamini wewe ni ccm kimwili lakini kiroho upo CDM endelea kukaa humo ili tupate habari Kama hizi lakini kabla ya 5/5/2015 uwe umesha kula corner uwe full CDM kwani ccm itakuwa itakuwa mochwari
   
 4. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kaka asante kwa kugundua na kuchimbua historia ya chama chako tokea enzi zileeee, ila umedanganya kidogo kwani wewe mwenyewe umekiri chadema ndicho chama cha uwazi na chenye matumaini kwa watanzania ndio kumaanisha wewe ni mwanachadema na sio mwana Chai Chapati Maharagwe,

  Twakukaribisha sana kwenye magwanda
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Lahana hizi wanazomshushia chibuda sio mda tutaona madhara kwake na familia yake kwa hivyo vijiela anavyopewa na magamba vitaishia kutibu matatizo tu!mwacheni mungu atamshughulikia tu,sisi kazi yetu ni kuomba mungu tu,
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  VIVA mwanahalisi!
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Kama na nyie mmelitambua hilo basi ni vema,
  kilichobaki mtuunge mkono sasa.
   
 8. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila mahali wanapokwenda chadema wanaambiwa wamtose Shibuda, Huyu mzee atapotea vibaya sana!
   
 9. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Shibuda nimechoka kumsikiliza......hata CCM alikimbizwa sababu ya tabia zake za kike hivyohivyo...
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Ivi CHADEMA kwa nini wasimtoe mapema tukaepuka shari.
   
 11. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I hope dawa yake inachemka msiwe na wasi wasi wanamvutia timing tu.
   
 12. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tumechoka na huyu mzee!
  Anakiaibisha chama cha ukombozi
   
Loading...