elimukwanza
Senior Member
- Dec 27, 2010
- 169
- 23
Jana nilivunjika sana moyo. Heri utukanwe na mtoto wa jirani, kuliko wako wa kumzaa. Inauma sana na ndio maana CCM walishangilia sana! Zilikuwa ni dakika kumi za mashambulizi kwa wanaCHADEMA na uongozi mzima! Nadhani hii inahusiana na bifu na Wenje,maana naona chama kilimpuuza na malalamiko yake ya kijinga.
Chadema kimeshakuwa chama kikubwa sasa, inabidi wawe na uwezo wa kuthubutu kuwachukulia hatua wanaovunja sheria na taratibu za Chama. Ilibidi waanze na Zitto! Hofu yangu ni kwamba itajengeka hisia kwa wanachama kwamba ukiwa mkubwa kwenye chama, hata ukikosea hakuna atakayekuchukulia hatua. Hii impunity ndio inayoiua CCM!
Shibuda anatufundisha umuhimu wa kuwa na katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi! Shibuda anajipendekeza kwa rais na CCM kwakuwa anajua watamlinda wakati wa uchaguzi! Watu kama wakina Cheyo na Mrema wasingekuwa ndumilakuwili kama tungekuwa na tume huru ya uchaguzi! CCM wanapenda kuwa na proxyies upinzani kwakuwa wanajua kuwa upinzani wanaweza kuuana wenyewe kisiasa kwa urahisi sana. It worked with NCCR, why not try it now?
Chadema wachukue hatua,shibuda hastahili kuwa na kadi ya chadema. Ameongea mengi hadharani, sirini anaongea mangapi? Chadema inawezaje kumshirikisha shibuda ktk mikakati yao ya maendeleo ya chama?Chadema ina sapoti kubwa sana ya vjana, hyo ndio hazina yao! Sio wazee kama shibuda ambao wanahesabu siku zao kisiasa. Bank on the youths![/QUOTE]
Huyu anastahili kabisa kufukuzwa kwenye chama kabla ya kusababisha athari zaidi na akifukuzwa anapoteza na ubunge.
Mbunge shibuda akiendeleza kile kinachoitwa Vijembe,mipasho ya bunge la sasa huku akitumia misamiati ya kiswahili cha pwani kumponda kiongozi wa CHADEMA na wanachadema alishangiliwa sana na wabunge wa CCM hadi mwisho bunge kugeuka ushabiki na kuimba CCM CCM CCM.Na alifika mbali zaidi na eti kuwaomba pole wananchi wa zanzibar eti kwa waliyoyapata ya kutengwa kutokana na maamuzi waliyofanya,akuwa wazi zaidi ila alimaanisha CDM kutoishirikisha CUF kutokana na kuunda serikali.
Ilinisikitisha sana huu unafiki na uzandiki mbona kama wanampenda walimchinjia baharini kwenye NEC,Shibuda amesahau au katumwa? maana sikuona kachangia hoja yeyote kuhusu Hotuba ya Rais zaidi ya kumponda(majungu) kiongozi wa CDM.leo pale bungeni kama unataka usifiwe wewe iponde CDM unawezwa ukabebwa
CDM msikate tamaa ila kuweni waangalifu kupokea makada mitumba toka CCM ni bora mkawekeza nguvu zenu kwa vijana wapya ambao hawaijui CCM achaneni na Mitumba ya CCM mlenge wagombea vijana na muutangaze mwaka 2015 kuwa wa vijana 70% ya wagombea wenu wawe vijana wasomi
Nawasilisha
Huyu anastahili kabisa kufukuzwa kwenye chama kabla ya kusababisha athari zaidi na akifukuzwa anapoteza na ubunge.
CUF walimfukuza Naila Jidawi uanachama Msekwa akasema ni mbunge halali nadhani hata Chiku Abwao aliwahi kufukuzwa NCCR kama sikosei lakini akaendelea kula kuku pale Dodoma. Mzee mipango hii huwa inasukwa ikasukika.
Akifukuzwa chamani si mbunge tena, soma hapo chini.
"Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Na Salim Said
OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi, inamtambua aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe kuwa bado ni mbunge wa jimbo la Kishapu kupitia Chama hicho hadi hapo itakapopata taarifa rasmi kutoka CCM.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ge-mpendazoe-bado-ni-mbunge-wa-kishapu-3.html
Aahh, osie uzakosea, sio vyedi...usiwatukane, waache wajitukane wenyewe, maana kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kutukana au kuropoka siri za nyumbani mwako na mkeo/mumeo anaekupa kula...Shibuda hana maadili yupo kimaslahi ziaidi