Shibuda amshambulia mkuu wa wilaya Meatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda amshambulia mkuu wa wilaya Meatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Nov 3, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Shibuda achafua hali ya hewa mkutano wa pamba

  MBUNGE wa Maswa Mashariki (Chadema), John Shibuda, jana alichafua hali ya hewa katika mkutano wa wadau wa pamba baada ya kuwashambulia wakuu wa wilaya ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kuwa, wanakwamisha mafanikio ya kilimo cha zao hilo, huku nao kuja juu kumshambulia.

  Shibuda alisema tangu mkutano huo uanze na majadiliano, watu wamekuwa wakiwatupia lawama wanasiasa kuwa ndiyo tatizo kwa mafanikio ya kilimo cha pamba kwa mkataba, lakini wanaoshutumu wajue kuwa wanamshutumu Rais Jakaya Kikwete na Waziri mkuu wake, Mizengo Pinda, kwa vile nao ni wanasiasa.

  “Nasikitishwa kwa kauli ya kuwa wanasiasa ni tatizo, basi mjue mnamsema rais na waziri mkuu na mawaziri wote kuwa ndiyo tatizo, hata wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa nao ni tatizo wapo kila siku kwenye vikao lakini hawafikishi taarifa kwa wananchi wao…” alisema Shibuda na kukatishwa na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Abihudi Saidea, ambaye alipaza sauti kuwa hata wabunge wamo katika vikao.


  Kutokana na kukatishwa huko, Shibuda alimgeukia mkuu huyo wa wilaya na kusema,
  "tuanzie Meatu ambako wananchi wanalia na kulalamika hawajapelekewa mbegu, baadhi ya mizani zimekuwa zinalalamikiwa pia na kumtaka mkuu huyo wa wilaya kutoogopa kujadiliwa, hali ambayo ilizua tafrani na kurushiana maneno ya hapa na pele."

  Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba, Raphael Mlolwa, aliwatuliza washiriki na kumuomba Shibuda kumalizia kwa vile alikuwa mchangiaji wa mwisho ili wajumbe watoke kuelekea katika chakula cha mchana kisha kurejea.

  Shibuda alihitimisha kwa kueleza kuwa, kilimo cha mkataba kina wapinzani wengi ambao ni changamoto kwa wanaosimamia, lakini aliwaomba kutowachukua watu wanaopinga kwa vile wanataka kuelimishwa.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  poleni sana watanzania wenzetu kwa uonevu huu unaofanywa na serikali hii ya ccm. Nalog off
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kila kona ya nchi ni vurugu tupu, bado tu mwaka wa kwanza tangu uchaguzi upite, uozo umezidi na uvumilivu umefikia kikomo.
   
 4. k

  king kong Senior Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm out of order.
   
 5. S

  Sambega Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Shibudaaaaaaaaaaaaaaaaa! Sijakusoma bado mh.
   
 6. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  suport kimtindooo
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,000
  Trophy Points: 280
  Hata Shibuda ni kada wa CCM mwenye kuvaa magwanda ya Chadema
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  huko Nyuma nilisha wahi kusema kuwa wanamtandao walipo pewa nchi na kuingia IKULU kweli wananchi waliwatarajia kwa mengi sana na Chati ya JK ilikuwa juu sana ila kumbe hawakujua kuwa IKULU kwenda kunahitaji kujipanga sasa wao wameingia IKULU na hawajui la kufanya na ndio maana haya yote yana tokea kutojipanga kwao ndiko kuliko waponza hawa viongozi wa CCM na kuipeleka serikali katika hali hii ya UCHUMI kupanda kusababisha maisha kuwa sio Bora tena kama yalivyo kuwa wakati wa Ben Mkapa kila kitu kimeyumba leo hii uliza hata hawa viongozi wetu Focus ya nchi iko wapi mpaka sasa hawajui ni kufanya majumuisho ya matokeo na kurushiana mpira kama boya mko swimming poor ndicho kinacho endelea kwenye serikali inayo ongozwa na viongozi wa CCM, Na ndio kupolomoka kwake huko sasa

  My Take;


  Serikali inaongozwa na group la watu fulani wakiwa na mtengano na msuguano mkubwa ndani ya CCM na serikali yao,

  Serikali inaogopa kukosolewa na inakuwa kali pindi ikikosolewa na kulalamika kuwa wapinzani wanahatarisha amani wakati wananjisahau kuwa wananchi pia wanachukizwa na wanacho kifanya na kupelekea maisha magumu.

   
Loading...