Shibuda aichana serikali ya CCM

Shibuda aichana serikali ya CCM

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
23 JULY 2012

Na Benedict Kaguo, Dodoma

MBUNGE wa Maswa Mashariki, mkoani Shinyanga, Bw. John Shibuda (CHADEMA), amesema nchi inaongozwa kwa misingi ya Mabepari na kusababisha Watanzania maskini kutengwa na maendeleo kwa sababu CCM haipo madarakani

Bw. Shibuda aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akizungumza na Majira kuhusu utoro wa wabunge ambao wengi wao kutoka chama tawala CCM, kukwamisha upitishaji Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa, CCM ambayo waliiamini kuongoza Serikali, haiko madarakani bali Serikali inajiongoza yenyewe kwa kutumia mifumo ya Kimagharibi badala ya msingi wa kuanzishwa kwa chama hicho.

"Serikali hii inasema wawekezaji kwanza, kilimo nyuma ikitumia nembo ya CCM wakati ukweli ni kwamba, Serikali imeitenga misingi ya kuanzishwa chama chao, sawa na gari ambayo imetengenezwa China na kuwekwa nendo ya Uingereza.

"Shabaha na malengo ya kudai uhuru wa Tanganyika ilikuwa kujenga misingi ya ustawi na maendeleo ya jamii, Taifa kushika hatamu za uchumi kwa masilahi ya uhuru ni maendeleo kwa taifa..dira hii ndio iliyoisukuma Tanzania kuunga mkono madai ya uhuru na ukombozi," alisema Bw. Shibuda

Aliongeza kuwa, kwa misingi hiyo wananchi wa kawaida wataendelea kubaki maskini ndio maana wakulima wanateseka na bei ya mazao likiwemo pamba kutokana na Serikali kuwasahau.

"Serikali inatekeleza siasa na sera za huisho la kufufua umangimeza na mabwenyenye, wamewageuza Watanzania malighali ya huduma ya utwana wa maisha bora Ulaya.

"Uthibitisho juu ya hili ni mikataba mibovu inayopora rasilimali za nchi...maliasili za Tanzania zimechomwa mikuki ya mirija ambayo inafyonzwa na wawekezaji, Taifa linabaki na kuimba wimbo wa kazi ya mungu haina makosa kumbe ni kazi shetani Mungu tunamuonea," alisema Bw. Shibuda.

Alisema inashangaza leo hii kuona mbunge akipewa Uwaziri, anabadilisha mienendo yake na kuwasahau walalahoi ambao ni Watanzania wanaotegemea kuongozwa.

Bw. Shibuda alisema CCM inapaswa kuwa baba wa kuingoza Serikali ambayo siasa na sera zake, zimetelekezwa katika makabati ya vitabu.

"Serikali hii sawa na chui aliyevaa ngozi ya kondoo...ukiona ngozi unajua ni ujamaa na kujitegemea kumbe ni mzimu wa chui ambao unateketeza rasilimali na maliasili kwa mapambio ya kuwaita wawekezaji, rasilimali zetu zinapelekwa nje na mabebari.

"Thamani ya rasilimali ndio bima ya maisha bora kwa kila Mtanzania na mkulima wa pamba, nchi haitaweza kusunga mbele kwa dhamira ya kuwa na Taifa huru la ujamaa na kujitegemea kwa sababu vitendo vya viongozi kuongoza njia ya safari ya kufaidi uhuru na maendeleo na kujitegemea," alisema.

Alisema viongozi wana tabia na matendo yasiyokubalika hata na dini zao hivyo Watanzania wanajazwa ujinga wa hewala si utumwa kwa dhana ya utandawazi unaobarikiwa na vifuniko vya diplomasia za uchumi ambazo ni nusu kaputi za kulala usingizi.



 
CCM jiangalieni hata Mpenzi wenu Shibuda anawaona nyie MABEPARI mnajali wawekezaji...
 
Mnafiki utamjua tu. Anabadilikabadilika kama kinyonga!
 
Huyu bwana haeleweki!!!!
anamtuzi kapteni wake rais J.M.Kikwete.Naomba mshauri huyu Mh Shibuda amwendee huyo rafiki yake ampe huo ushauri sio kusema kwenye magazeti wakati alishatangaza nia ya kugombea urais na akimwomba ampe compani
 
Wala hajaichana kwa nia mbaya. Anasema ccm inapaswa kuwa baba wa kuiongoza serikali. Hapo ana maana gani? Unategemea mtu kama zitto, wenje, mnyika, n.k wangesema hivyo? Kwa nini asiseme kuwa chama kilichoko madarakani, kiwe ccm au cdm kinapaswa kuwa baba wa kuiongoza serikali?
 
Hongera Shibuda. Ni kweli ni aibu kwa Bunge la nchi kama Tanzania, tena Bunge la Bajeti kuwa na viti tupu kama ambavyo huonekana katika Luninga. Hawa Waheshimiwa sijui huwa wanakwenda wapi.

Hata kama wanakuwa na dharura za kibinadamu, ukifanya hesabu kitakwimu nagundua kuwa Bunge huwa na asilimia chache sana ya Wabunge.

Sasa je tatizo ni urefu wa taarifa za bajeti au ukali wa Spika unachangia kuwafanya waheshimiwa wabunge wamuachie viti wazi ili abaki na wachache wanaoweza kuvumilia lugha yake kali?

Ni vyema Waandishi wa habari wakamfuata Katibu wa Bunge ili alitolee ufafanuzi suala hili. Nia aibu na inaudhi, hasa unapolinganisha mahudhurio yao Bungeni na kiasi kikubwa cha pesa wanachopokea kwa ajili tuu ya kuwepo Bungeni.

Wanahabari mliopo jamvini, tafadhalini mtafuteni Katibu wa Bunge ajieleze tatizo ni nini na kwa ushauri wake na kanuni walizonazo nini kifanyike, na kwa nini hakifanyiki?
 
Whether kigeugeu au nini mie sijali!ameongea ukweli kabisa. Mnamuona shibuda ka adui yenu mnapoteza mda bure,hawa watu wapo kwenye jamii na tunaishi nao and wakati mwingine wanatusaidia hata kujua udhaifu wetu,kupitia shibuda tumejua misimamo ya watu kibao,waropokaji tumewajua pia.

So, pamoja na mapungufu ya shibuda,stil anahaki ya kupongezwa akisema kitu kizuri.usitake kila mtu awaze unachopenda wewe,utapoteza maana ya ubinadamu.
 
Back
Top Bottom