Sheria ya PPF Pensions Fund inaruhusu mafao ya kujitoa

tunataka mafao yetu, suala la kusubir mpk retirement age 55-60 ni jambo sio muafaka kwa watz wa sasa ukizingatia our Tanzanian's life expectancy ni miaka 51 kwa wanaume na 54 kwa wanawake( source indexmundi-CIA) wanasiasa zingatieni hili

Mpaka ufikie umri huo wa miaka 55, jamaa watabadilisha tena sheria ya SSRA, na kusema kuwa umri wa kustaafu umeongezwa mpaka miaka 65.
Hapo ndipo watu watakapojua kuwa hakuna mafao wala pensheni, ila ni kudanganyana tu.
 
Wana JF,
Nimefuatilia mijadala mimngi hapa JF inayohusu swala la mafao ya kujitoa.
Nimeona kuwa watu wengi hawajui kuwa mafao ya kujitoa PPF yapo kisheria na kudhani kuwa mafao hayo yanatolewa na PPF kama hisani tu.
Kwa sababu hiyo, SSRA, serikali na watu wengine wametumia mwanya huo kupotosha ukweli kuhusu mafao hayo, na kusema kuwa mafao hayo hayapo kisheria.

PPF Act No. 25 ya mwaka 2001, kifungu cha 44 kinasema yafuatayo:-

“Withdraw Befefits"

44.-(1) Where a member ceases to be employed in circumstances in which he is not eligible for any pension, gratuity or any other benefit under the provisions of this Act, he shall be refunded the amount of his own contributions and that of his employer to the Fund.
(2) Where a member has been employed for a period of not less than five years and the
cessation of such employment is not due to dismissal for misconduct
the amount of his own
contribution and that of his employer together with a simple interest at that rate to be determined
by the Board of Trustees shall be paid to him.

Kwa kifupi kabisa, mafao ya kujitoa PPF yapo kisheria kabisa, na wala sio hisani, na wala sio kinyume cha sheria.

PPF huwa hawataki kusikia hiyo kitu hasa kwa wafanyakazi wa mashirika ya umma ingawa NSSF ndiyo ilikuwa inatoa fao hilo.
nafikiri hata kama hawatatoa hela basi waweke utaratibu hata wa kukopesha nyumba au mali nyingine kama walivyoahidi maana hata wakulipa pesa mwisho wa siku inaweza isiwe na impact kwenye maisha maana siye wengine tukilipwa pesa lumpsum inakuwa taabu
 
Kweli mikopo ya nyumba inaweza ikafaa sana, ila iwe optional kwa anayetaka. Hapa SSRA wanalazimishia kuwa wanachama wa mifuko walazimike kuacha mafao yao kwa kigezo cha kukopeshwa nyumba. Hizo nyumba zenyewe hawana control nazo, maana labda ni nyumba za NHC, au za watu binafsi wenye maamuzi yao ya nani wamkopeshe na nani wasimkopeshe.
Mwisho wa siku unaweza kukuta kuwa hamna muuzaji wa nyumba anayekubali kuwakopesha wanachama wa mifuko ya pensheni.
 
Naona unazungumzia PPF, vipi kuhusu NSSF, PSPF, & LAPF? au ulivyosema PPF ulikuwa na maana ya mifuko yote ya hifadhi ya jamii???
 
Watulipe za mkataba wa zamani kwanza,ndio waanze kutuimbia wimbo wao huo mpya,na mimi ntaziba masikio vilevile,sitataka kuusikia,wezi wakubwa hawa.
 
Sote tunajua kwamba yalikuwepo, lakini sheria mpya ya kuanzisha mamlaka ya kusimamia mifuko ya jamii maarufu SSRA imefuta mafao ya namna hiyo na hicho ndicho kinacholalamikiwa. Kwa ufupi ni kwamba hiyo sheria unayonukuu leo imeishapitwa na wakati na haina nguvu tena kisheria

Mkurugenzi mtendaji wa SSRA, Irene Isaka alijaribu kuwatisha wafanyakazi kwa kusema kuwa mifuko ya pensheni ilikuwa inatoa mafao hayo kinyume cha sheria, wakati sheria za mifuko hiyo ziko wa zi kabisa:-

"... hata hivyo mifuko yote ya hifadhi iliyoko nchini haitoi fao la kujitoa na kwamba waliokuwa wakitoa fao hilo walikuwa hawafuatia sheria ya mafao saba yanayotajwa kisheria..."

Hapa alitaka kuwatisha wafanyakazi kuwa mafao ya kujitoa hayapo kisheria.
Hakujua kuwa watanzania wa sasa wanasoma sheria na kuzijua vizuri. Mifuko ya PPF, LAPF na PSPF inatoa mafao ya kujitoa kisheria kabisa.
 
Naona unazungumzia PPF, vipi kuhusu NSSF, PSPF, & LAPF? au ulivyosema PPF ulikuwa na maana ya mifuko yote ya hifadhi ya jamii???

Nimesoma kwenye website za mifuko hii yote, NSSF peke yake ndio hawagusii kuhusu mafao ya kujitoa. Mifiko mingine yote inataja kuwa mafao ya kujitoa ni mojawapo ya mafao wanayoyatoa.
 
Lengo la kuanzishwa kwa SSRA ilikuwa kudhibiti matumizi ya hovyo ya mifuko hiyo ya pensheni na kuhakikisha kuwa mifuko hiyo inatoa mafao yanayolingana na hali halisi ya maisha kwa wanachama wao.

Bahati mbaya SSRA wakaingia kwenye mtego wa mifuko ya pensheni na serikali kuwa mafao ya kujitoa ni mojawapo ya matumizi ya hovyo. Badala ya kuangalia uwekezaji unaofanywa na mashirika hayo na kuangalia kanuni za ukokotoaji wa mafao kwa wanachama kwa lengo la kuleta uwiano kati ya mafao yanayotolewa na mifuko mbali mbali, wamejikuta wakiingia kwenye ngoma isiyokuwa yao. Ngoma ya kutetea uondoaji wa mafao, badala ya uboreshaji wa mafao.

SSRA wameshasaliti lengo la kuanzishwa kwao na kwa mguu huo, hawana sababu yoyote ya kuendelea kuwepo kwani wameongeza mzigo mwingine usiokuwa na manufaa kwa wanachama wa mifuko. SSRA hupata mapato yao kutokana na mifuko hiyo ambayo huchota fedha za wanachama wao na kuwapa kwa ajili ya kujiendesha. Bahati mbaya SSRA wanafikiria kuwa fedha zinazoifanya iwepo ni fedha za mifuko si za wanachama.

SSRA inatakiwa wafanye marekebisho ya kosa hilo vinginevyo hawana uhalali wa kuendelea kuwepo. Marekebisho watakayoyafanya ni kama ifuatavyo;
  • Wabadirishe uamzi wao wa awali wa kusema mafao ya kujitoa ni matumizi ya hovyo
  • Wajitoe kwenye ushirika wao usio na sababu yoyote wa kushirikiana na mifuko: Wao ni wadhibiti iweje waimbe wimbo wa mifuko
  • Wajue kuwa lengo la kuwepo kwao ni kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha mafao si kuyaondoa au kuyapunguza
  • Wafanye kazi zaidi na wale walio kwenye nafasi ya kugandamizwa - Yaani wanachama wa mifuko. Mifuko tayari ina maguvu ya fedha. Mdhibiti kushirikiana na mifuko dhidi ya wanachama wanyonge kunaondoa maana yoyote ya udhibiti.

Vinginevyo wasubiri kiyama yao. SSRA imeundwa na sheria ya juzi tu. Wasishangae wanasiasa watakaoingia na kampeni ya kufutilia mbali SSRA wanashinda uchaguzi ujao. Hii gia waliyoanza nayo, inayowatambulisha SSRA ni gia mbaya sana na inawafanya waonekane kama mgandamizaji tu. Regulator inatakiwa awe independent. Kwa sasa hivi hawa hawaonekani kuwa independent kwani wamechukua msimamo wa Mifuko na serikali. Wanaojua wanasema hii ni "PR dissaster".
 
Wana JF,
Nimefuatilia mijadala mimngi hapa JF inayohusu swala la mafao ya kujitoa.
Nimeona kuwa watu wengi hawajui kuwa mafao ya kujitoa PPF yapo kisheria na kudhani kuwa mafao hayo yanatolewa na PPF kama hisani tu.
Kwa sababu hiyo, SSRA, serikali na watu wengine wametumia mwanya huo kupotosha ukweli kuhusu mafao hayo, na kusema kuwa mafao hayo hayapo kisheria.

PPF Act No. 25 ya mwaka 2001, kifungu cha 44 kinasema yafuatayo:-

“Withdraw Befefits"

44.-(1) Where a member ceases to be employed in circumstances in which he is not eligible for any pension, gratuity or any other benefit under the provisions of this Act, he shall be refunded the amount of his own contributions and that of his employer to the Fund.
(2) Where a member has been employed for a period of not less than five years and the
cessation of such employment is not due to dismissal for misconduct the amount of his own
contribution and that of his employer together with a simple interest at that rate to be determined
by the Board of Trustees shall be paid to him.

Kwa kifupi kabisa, mafao ya kujitoa PPF yapo kisheria kabisa, na wala sio hisani, na wala sio kinyume cha sheria.

@Mu-Israeli: kulingana mafao ya kujitoa kama ulivoelezea hapo juu, ina maana kwamba kama umefanya kazi miaka 3 au 4 ilo fao kulipata ni ndoto sana in this case unawezapata fao tu kama umefanya kazi miaka 5 na zaidi? Nakipengele cha kwanza je mtu aliyefukuzwa kazi au ka-resignje na amefanya kazi kwa miaka 3 je, anaweza pata kiinuo mgongo chake?? Msaada please!
 
Back
Top Bottom