Sheria ya kutoa

Sheria ya kutoa

Wengi watapinga!lakini ndio asili!hakuna kuongezeka pasipo kutoa!

Nilitoa nikaangusha ngome fulani na Sasa nipo huru,ilihitajika nguvu kubwa sana!
Kutoa ni kutoa na sio kujumlisha , ikija nyingine ni mpya na sio ile uliyotoa , wewe ndio upo kinyume na kanuni za maumbile.
 
Hiyo ndo shida ya kupenda vitu laini laini....hoja Nimekuwekea hapo juu husomi? Ushazoeshwa vitu vifupi vifupi siyo?
Utumbo mwingi umeandika unashambulia binafsi, nipe mchakato wa kutoa unapokea , nnje na maumbile ya kibiashara na kubadilishana uzoefu.
 
Watu ujuaji mwingi kaka...ila hii siri ni nyeti sana wachache wanaijua na kuifanyia kazi.
Wachache kina nan ? Binafsi huwa naweza toa tu bila kutarajia nitoe halafu nipokee kitu , na nikitoa nimetoa nikapata hicho ni kingine na sio kile nimetoa
 
Yani utoe kwa mtu asiekupa ndio upokee?🤣🤣🤣 , kutoa utapokea endapo kile umetoa kitamea kwenye rutuba na kuzalisha zaidi , tofauti na hapa hakuna miujiza .

Kama unatoa ,toa kwa moyo tu bila kutajarijia malipo , huo ndio utu na sio unafki.
 
Yani utoe kwa mtu asiekupa ndio upokee?🤣🤣🤣 , kutoa utapokea endapo kile umetoa kitamea kwenye rutuba na kuzalisha zaidi , tofauti na hapa hakuna miujiza .

Kama unatoa ,toa kwa moyo tu bila kutajarijia malipo , huo ndio utu na sio unafki.
Nilikwambia hapo juu "wewe ni maiti inayotembea"...si unaona unavyojianika?
 
We jamaa huwa unajifanya mjuaji sana,Huwa unajifanya intelligent sana yan.
Waliokwambia elimu ni bahari hawajakosea,Hii Dunia umeikuta Kaka na Hata ulipokuja hukuja kwa plan yako,yupo aliyeplan uje na wewe ukashtukia tu Upo Duniani.
Sasa huyo aliyekuleta Duniani Kuna elimu ameziweka na hzo elimu hazipo hta huko mashuleni,pia ameweka mifumo ya maisha watu waifuate,na usipoifuata utakufa na huo ujinga wako.
Ni Hivi,kutoa kwenda kwa wahitaji ni jambo ambalo hta hao wazungu unaowaabudu wanaijua siri yake,ni sheria ya kimaumbile inayoapply kwa mtu yeyote anayeifanya,haijalishi unamcha Mungu Au laa,Mungu ameiweka sheria hii ya kutoa Kama Zawadi kwa viumbe wake...ni kama ilivyo ile sheria ya UKILA LAZIMA UENDE CHOONI...NA KILA ANAYETOA KWA WAHITAJI MATOKEO CHANYA LAZIMA AYAONE.
Hao wazungu unaowaabudu wanaielewa vzr sana hii sheria ya kutoa na wanaifanyia kazi vizuri sana....unaijua BILLGATES FOUNDATION?....COCACOLA FOUNDATION? Lakini pia si Unaifahamu VODACOM FOUNDATION? Na nyingne nyingi....
Unafahamu kazi za hzo foundations?
Yan watu na Akili zao wameigundua hii siri ya kutoa Afu wewe unakuja na uharo wako kwamba wewe una Akili sana eti ....Akili zenyewe uzitoe wapi kma hta aliyekuumba unamkana,wewe si ni Kama maiti tu Hivi inayotembea?
Acha upuuzi wa kijinga jinga,ukiona watu wanapewa elimu flan usijifanye kimbelembele kudecline idea kana kwamb wewe Unajua sana wakati wewe ni kiumbe wa kawaida sana uliyetokana na shahawa na pengine huna Hata miaka 40 Tangu uje Hapa Duniani...hii Dunia Ina mabilioni ya miaka na hii sheriA ipo Tangu huko wajanja wanaitumia..achaga ujinga.
KILA UNAPOTOA KWA WAHITAJI MUNGU MTOAJI NDO ANAKUJAZIA ZAIDI ULIPOTOA..hii ndo sheria Haijalishi Unataka Au hutaki,hii sheria ipo tu na inafanya kazi kwa yeyote anayeiapply.
Uyu bhana mm siwez bishana nae Bado toto dogo sana kwenye ulimwengu huu,ivyo namuacha TU ahare anavyo taka kama ulivyo sema 😂😂😂😂 sisi tulisha tokaga level izo,ivyo hawez kukuelewa apo unapoteza time yako bure
 
Huwa ananikera sana huyu jamaa..... elimu ni pana sana wazee,Kwenye hii mitandao ukiona mtu kakuletea elimu flan usijifanye wewe ni mjuaji sana,unachotakiwa ni Kukaa na ujifunze na si kupinga pinga tu kila kitu.
Kweli mkuu 💯
 
KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ukitoa ndio unapata.

Hii ni kanuni ya ulimwengu wa roho ,kanuni ya Mungu mwenyewe ambapo pia inatumiwa na pande zote za kiroho ukimwengu wa giza(watu /wafuasi wa shetani) na ulimwengu wa nuru(watu wa Mungu)
na hata wasio dini au waapagani au wanaoamini katika karma,nature kwa kujua au kutokujua.

Shetani anaijua hii ndio mana naye anaitumia kwa watu wake wafuasi wake wachawi,waganga wa kienyeji,mafreemansory n.k

1)KWA IMANI YA KIKRISTO UKISOMA BIBLIA UTATHIBITISHA HILI
mkono unaotoa ndio inaonarikiwa kuliko mkono unaotoa.

kipimo kile unachowapimia watu kuwapa ndicho hicho hicho Mungu atakupimia kwa scale yake mana kwa Mungu miaka 1000 ni sawa na siku moja,kipimo chako mwanadamu mfano ukimpa mtu kwa kipimo cha mkono wako mwanadamu Mungu anapokurudishia akikupimia mkono wake mkubwa mkuu basi inakuwa kingi kicho jaa kusukwa sukwa hata kumwagika.

Anayemsaidia masikini anakuwa anamkopesha Mungu Mungu atamlipa kwa tendo lake hilo jema.
KIFUPI MKONO UNAOTOA NDIO UNAOBARIKIWA ZAIDI KULIKO UNAOPOKEA .

Kwa dini nyingine pia naona wao wanatoa zaidi kwa masikini,wagonjwa mahospitalini,wafungwa ,yatima ,na wasiojiweza

kama waislamu kwakweli huwa naona watoa sana sadaka kwa wahitaji...hasa wagonjwa na hao wengine masikini ,yatima ..nafikiri kwao ni NGUZO KABISA ya imani yao..mfano mahospitalini wanawaletea wagonjwa chakula alfajiri,mchana,nguo ,maji,na kadhalika.

FREEMANSORY ..wao ndio kabisa wanajiita shirika la kutoa misaada kwa wahitaji charity.

WAGANGA WA KIENYEJI NA WACHAWI
Baadhi ya masharti yanahusisha kutoa zawadi au vitu kwa watu,
zawadi kamaa vyakula ,nyama za kafara,pesa zilizonuiziwa,nguo,viatu,vinywaji n.k

unaweza kukuta mshirikina kazi yake anachinja makafara yake anawagawia watu nyama ,au anaandaa sherehe watu waje kula na kunywa,au anawagawia watu pesa,zawadi,vyakula,vinywaji n
k
kupitia kutoa ndio anapata zaidi...

Hata nchi wahisani...zinatoa sana misada kuja nchi za kiafrica kwa sababu zinafaidika zaidi kwa kanuni hii ya kiroho KUWA ANAYETOA NDIO ANAYEBARIKIWA ZAIDI KULIKO ANAYETOA.

Na waliogundua KANUNI HII watakubalina na mimi kuwa kuoitia kutoa wamepokea baraka zaidi,na mara nyingi utagundua watu walioifahamubsiri hii utakuta hawaachi kutoa kila wakati ,wameshagundua siri iliyopo.

HATA katika ibada yoyote iwe ya madhabahu za nuru au zile za giza
lazima kuna sadaka utoe sadaka

tena wachawi na wa waganga wa kienyeji freemansory wanatoa sadaka 60% tena inatolewa kwa lazima na kwa wakati..
wakati Zaka inayotolewa kwa Mungu ni 10% ..tu.

yani ukiona mpaka mchawi anafanikiwa kuwa na nguvu za kichawi au kiganga ametoa sana sadaka hata damu yake kama watoto ama kuimarisha vizimba vyake sadaka mbalimbali.

kutoa kunakupa nguvu ya kiroho ya madhabahu yako,kama ni ya guza au nuru.

Hata waumini wanaotoa sadaka ya ZAKA 10% kwa Mungu kwa uaminifu wanakuwa na nguvu kubwa ya madhabahu zao na baraka nyingi.
na mchawi anayetoa sadaka mara kwa mara sadaka kubwa naye anaimarisha vizimba vyake nguvu zake za uchawi wake.

KIFUPI HAKUNA CHA BURE ILI UPATE LAZIMA UTOE KWANZA.

na kuna azuiaye isivyo haki lakini huishia kuwa muhitaji.
yani kuna azaniaye kuwa anakusanya kumbe anataoanya au anatia katika mfuko uliotoboka.

WENYE UELEWA WA KANUNI HII huwa wanapenda sana kutoa bila kuchoka sio wachoyo kabisa.

lakini wachawi wanaitumia vibaya..USIPENDE KUPOKEA POKEA vutu vya bure bure hovyo,usipende kula kula ovyo wengine wanaandaa sherehe na kugawa vyakula bure,au vinywaji au pesa wakiwa na lengo la kuchukua kutoka kwenu ushurikina,au ni rahisi ukala nyama ama vyakula vya matambiko,auakafara yaliyonenewa nuiziwa.

SALI OMBEA CHAKULA KABLA YA KULA..ombea zawadi unazopewa .
omba sali kila wakati.
 
Mdo 20:35
Daima niliwaonesha kwamba mnapaswa kufanya kazi nilivyofanya na kuwasaidia wadhaifu. Niliwafundisha kukumbuka maneno ya Bwana Yesu aliyosema, ‘Ni baraka kuu kutoa kuliko kupokea

ni heri kutoa kuliko kupokea

blessed is the hand that giveth than the one that taketh.

Lk 6:38
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

(kipimo mtakachopimiwa na Mungu kinakuwa kikubwa kuliko mlichopima mara 1000 zaidi)

Methali 19:17 BHN
Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema.

ukimsaidia masikini umemkopesha MUNGU ni haki yako kulipwa ,uwe na dini usiwe na dini hata kama ni moagani..Mungu ni wa haki atakulipa kwa tendo lako jema.

maandiko yako mengi sana siwezi kuyaandika yote.


ILA KIFUPI KANUNI YA KUPATA NI KUTOA na baraka sio kupata mali tu hata baraka nyingine ikiwemo afya ,ulinzi, n.k

sadaka zako ni akiba yako ni ukumbusho mbele za Mungu zinapiga kelele zina ongea zitasimama kukutetea wakati wa shida ukiwa hujiwezi,,WEMA NI AKIBA mbele za Mungu hauozi.

Zaburi 41
Hakikisho la msaada wa Mungu na ombi la uponyaji
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 Heri amkumbukaye mnyonge;
BWANA atamwokoa siku ya taabu.
2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,
Naye atafanikiwa katika nchi;
Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.
Katika ugonjwa wake unamponya maradhi yake yote.

nabmwisho kabisa dini iliyosafi ni
kisaidia wahitaji masikini ndiyo dini

Yakobo 1:27
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.

huwezi kusema wewe una dini ama una imani kama huna matendo ,mtendo yenyewe ndio haya ya huruma kwa wahitaji na upendo kwa watu wote na upendo kwa Mungu,ikiwemo kumtii Mungu.
 
Back
Top Bottom