Sheria ya kushitaki makampuni ya mitandao na simu kwa usumbufu na hasara

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,732
7,611
Leo nimejiunga kifurushi cha Tzs. 5,000 kupitia Tigo Pesa nimekatwa pesa na sikupata kifurushi nimepiga simu huduma kwa wateja nikaambiwa nisubiri masaa 72 nitarejeshewa pesa yangu iliyokatwa kuna tatizo la mtandao.

Je kwa huu usumbufu hatuna sheria ya kuwashitaki mitandao ya simu?

Mwaka huu mwezi wa 5 nikiwa safarini mkoani Kagera nilienda kwa wakala kutoa pesa kiasi 250,000 M-Pesa nilipotoa kiasi hicho walikata katika akaunti yangu lakini wakala hakupata meseji wala salio. Majibu ya huduma kwa wateja masaa 72 ilinichukua siku nne kurejeshewa pesa zangu na kuanza safari tena.

Mwaka huu jana mwezi wa 12 nikiwa safarini mkoani Singida nilienda kwa wakala kutoa pesa kiasi 300,000 Tigo Pesa nilipotoa kiasi hicho walikata katika akaunti yangu lakini wakala hakupata meseji wala salio. Majibu ya huduma kwa wateja masaa 24 ilinichukua wiki nzima kusitisha safari kurejeshewa pesa zangu na kuanza safari tena.

Ipo sheria inayotulinda na usumbufu mkubwa pamoja na hasara ambayo mitandao ya simu hutusababishia?
 
Back
Top Bottom