Elections 2010 Sheria ya kugombea ubunge irejewe?

Son of Africa

JF-Expert Member
Jan 16, 2011
233
31
Sheria ya kugombea ubunge kuanzia mwaka 2015 irejewe? Kwamba bila qualifications zifuatazo iwe stop?
1. Sharti uwe na shahada moja yoyote
2. Usiwe na uraia wa kuandikishwa?
3. Usiwe na Account yoyote nje ya nchi?
4. Uthibitike hujawahi kutuhumiwa na umma kuhusika na biashara yoyote serikalini i.e kupewa zabuni ktk biashara baina yako na serikali kwani ndo mwanya wa ufisadi.

KAZI NI KWENU
 
nitaunga mkono hoja(son of africa) utakapo oanisha @ moja ya kigezo no umuhimu wake
 
Sheria ya kugombea ubunge kuanzia mwaka 2015 irejewe? Kwamba bila qualifications zifuatazo iwe stop?
1. Sharti uwe na shahada moja yoyote
2. Usiwe na uraia wa kuandikishwa?
3. Usiwe na Account yoyote nje ya nchi?
4. Uthibitike hujawahi kutuhumiwa na umma kuhusika na biashara yoyote serikalini i.e kupewa zabuni ktk biashara baina yako na serikali kwani ndo mwanya wa ufisadi.

KAZI NI KWENU

Ni wazo zuri ila halisaidii kupunguza ufisadi. Kwa sababu zifuatazo

1. Watu watatafuta degree hata za miezi mitatu, ila sidhani elimu ndiyo inatoa kiongozi msafi au bora, bali ni combination ya elimu na maadili
2. Uraia mbona watu wana-forge tu?

Mimi ningependelea kuachana na yote hayo bali sheria ilenge katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki. Unapokuwa na system inayomuhakikisha mgombea wa CCM kushinda kwa vyovyote inamjengea kiburi mtu huyu na kuelekeza unyenyekevu kwa chama ili kisikate jina lake badala ya wananchi ambao ndiyo wanatakiwa kuwa na ultimate decision ya nani awe kiongozi wao.

Kwa Tanzania ya leo na uelewa wa watu ulivyoongezeka, ni dhahiri kuwa mtu yeyote mwenye tuhuma hawatamchagua na kwenye hili ni kwamba CCM inapoteza uongozi wa nchi. Ninaamini kabisa kwa mzalendo hasa hataangalia masilahi ya chama bali ya nchi na wananchi. Chama kinaweza kuwa genge la waroho wa mali wanaotumia siasa na uongozi kama sehemu ya kujitajirisha ila nchi haiangalii kundi bali ni aggregate society.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom