Sheria ya kazi na ajira

MaluguMlp

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2018
Messages
576
Points
250

MaluguMlp

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2018
576 250
Habari yako kiongozi.

Nimeona post yako ukitoa msaada kuhusu masuala ya sheria ya kazi na ajira.

Kwanza naomba nikupongeze kwa hili, na nizidi kukutia moyo na kukuombea kwa Mungu uzidi kutusaidia sisi tusio na ufahamu juu ya sheria.

Pili nina ishu binafsi ya utata juu ya kazi yangu. Ninafanya kazi katika kampuni moja ya masuala ya real estate.

Kampuni hii ilituajiri tukiwa vijana watano kwa ajili ya kutafuta wateja (marketing) pasipo na mkataba wa kazi ila kwa makubaliano ya malipo ya mshahara pamoja na commission ya 3% ya kila kiwanja tunachouza.

Malipo ya viwanja yalikuwa yanafanywa kwa awamu mpaka miezi 12. Kwa hiyo kila mwezi tunaangalia mapato yaliyoingia kutokana na wateja wanaoendelea kulipia viwanja vyao kila mwezi kisha sisi kama team ya watu watano tunagawana hiyo 3% pamoja na mshahara.

Sasa tatizo limeibuka kwamba hawataki kutupatia mshahara ila wanataka kuongeza commission kuwa 7%. Jambo ambalo binafsi sikubaliani nalo (maslahi yanakuwa madogo sana).

Sasa Ninaomba kujua binafsi au nina nguvu gani kisheria haswa ukizingatia endapo watanifukuza bado nina haki ya kudai ile 3% iliyotokana na wateja niliowaingiza ambao bado wanaendelea kulipa (malipo ni miezi 12).

Changamoto kubwa nliionayo ni kwamba hatuna mkataba wa kazi wala docs isipokuwa makubaliano tuliyoyafanya katika kikao tulichowahi kukaa (Attached).

Ninaomba sana msaada wako mkuu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati

Richard
0742258837
 

Forum statistics

Threads 1,389,947
Members 528,062
Posts 34,039,357
Top