Sheria ya fao la kujitoa lini itajadiliwa tena bungeni?

Ccm nawabia mapema kwenye hili swala la fao la kujitoa ntafanya kampeni mbaya zaidi ya nnazofikiria kufanya.....
Hakikisheni fao la kujitoa linarejeshwa....m
 
Nikionaga hizi nyuzi za mafao nachefukwa.
Najiskia kuwatukana PPF.
Hawa ndio walioanza huu ungese.
Any way Tcra wananifanya nikae na povu langu.
 
Nafikiri ni wakati sasa wa kila mmoja wetu kumpigia simu au kumtumie ujumbe wa maandishi SMS mbunge wake kumtaka akalisemee hili bungeni. Kwa kweli sisi vibarua wa sekta ya madini tunaumizwa sana na hii dhulma.

Tafadhali kila asomaye hapa na amtumie ujumbe mbunge wake. Na pia tusaidiane kupata namba za wawakilishi wetu hapa hapa jukwaani ili zoezi lifanikiwe
 
Hakyanani ninkaribia 80m nssf siku wakisema "suu" naacha na kazi huo ni mtaji tosha
 
hasa wenye mikataba mifupi. mtu asubiri hela hiyo mpaka umri wa kustaafu . badala apewe ashughulikie familia yake wakati anatafuta sehemu ya kujishikiza tena ? huo ni mtaji wa biashara ndogo ndogo badala ya mtu kwenda kukopa akumbane na riba zisizo eleweka.
 
Inauma sana, kuna jamaa yangu aliambiwa a-claim baada ya miezi sita tangu alipoacha kazi, kwani utaratibu ukoje kwa sasa?
 
Nasikia pesa inapitiaga serikalini hata hao wenye mifuko ya kijamii wanalalamika kwamba dola imeshikilia pesa. Wastaafu tu wanacheleweshewa pesa zao sembuse wewe kijana mwenye nguvu za kufanya kazi
 
Mimi nilishajaza claim form nikakamilisha kila ktu cha ajabu PPF wakakataa kunipa hela yangu tangu mwaka jana mwezi wa 6. wakati huo nna matatizo hospital inahitajika 3mil niweze kufanyiwa operation. nikawaambia basi wanipe mafao ya ugonjwa kama wanavojinadi kwenye matangazo yao, wakasema sina vigezo coz natakiwa kuchangia miaka 15 ndio niwe na hiyo sifa. iliniuma sana na itaendelea kuniuma coz kampuni yenyewe nliyokua nafanya kazi sidhani kama bado ipo, Hua najiuliza hata wakianza kutoa hayo mafao sijui ntaanzia wapi. nchii hii wanyonge tunaonewa sana.
 
Njia nzuri sana ila kupata namba za waheshimiwa ni ngumu mfano kama mimi mbunge wangu kigamboni ni dk. Faustine Ndugulile namba yake sina na nimetafuta bila mafanikio
I hope watu wakitoa ushirikiano tutapata namba zao maana si siri, ni wawakilishi wetu. Hakuna namna, lazima tuwasisitize watupazie sauti...tudhulumiwe tukijua angalau tulijaribu kufurukuta
 
Habari wanajamvi,
Kwa yeyote mwenye kujua juu ya suala la Sheria ya fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
a)Lini itajadiliwa?
b) Kuna uwezekano wa kurudishwa kuwa kama awali?
c) Serikali ina mpango gani juu ya suala hili?
Kwa yeyote mwenye majibu au taarifa katika hili tafadhali atujuze hapa, nawasilisha.
Hilo ni jambo la kundi dogo tu, hivyo halina maslahi mapana kwa Taifa, labda lingetuhusu sisi wakulima. Njooni huku shamba enyi wapiga dili.
 
Back
Top Bottom