Ndugu wapendwa,
Kuna suala moja naona kama lina walakini, na ningepata wasaa ningemshauri Waziri wa Ardhi aliangalie kwa makini.
Mtu umejipinda ukapata pesa kidogo ukaingia maeneo ya Mbezi, Bonyokwa, Goba n.k kutafuta kipande cha Ardhi ili ujenge maana kodi haziaminiki mjini.
Unamalizana mwenye ardhi na kupitia michakato yote pale kijijini ili isiwe tabu baadae.
Kwakua hutaki shida unakwenda ardhi ili kukipima upewe hati kabisa,
Cha ajabu watu wa arhi wanakuja kukuambia kua kwa mujibu wa "Master Plan" ya mji, hapo ulipopata ni eneo la wazi/soko/barabara,
Swali langu ni kua, kwanini basi hizo master plan zisiwekwe huko kijijini ili kila anaenunua ajue hukohuko kua kaliwa?
Serikali ya kijiji inakupitisha kununua kwamba ni mahali halali,
Serikali kuu inakuja kukuambia kua sio, hapa imekaaje?
Kuna masuala ya kuchukua location ya eneo (GPS) ili ukapate uweli kuhusu hilo eneo wizarani, but ni wangapi wanajua kuhusu hii kitu?
Ni kweli unaweza kuomba amendment ya hiyo plan ikafanikiwa?
Kweli kabisa mkuu, sheria ya ardhi ina matatizo makubwa sana. Mipango miji hwawezi kuweka master plan wazi kwa sababu wanataka usubiri viwanja wapime wao na wakuuzie kwa rushwa na tena kwa gharama kubwa. Ukinunua kiwanja kwa wanakijiji maanake wao watakosa pesa.
Pia sheria ya aridhi inachangia umaskini. Watu wenye mashamba huko nje ya mji wananyang'anywa ardhi yao wanayoitegemea kwa kilimo bila kulipwa fidia, badala yake vinapimwa viwanja ambavyo vinauzwa na halmashauri badala ya wenye mashamba. Mtu anaponyang'anywa eneo ambalo amekuwa akilitegemea kujipatia mapato yake bila fidia maana yake ni kwamba huyo mtu tumemsukuma aende kuwa ombaomba wa milele. Ni unyama wa hali ya juu.
Ni afadhali mipango miji wachore ramani, viwanja auze mwenye ardhi maana Hilo ndo tegemeo lake, upimaji ufanywe na makampuni binafsi.
Shark, sheria ina tatizo gani hapo specifically? Umesema "unamalizana na mwenye ardhi" halafu unaenda Ardhi kutafuta hati unakuta "umeliwa." Sasa hapo ndugu yangu, tatizo ni sheria au ni wewe uliyefanya mambo kinyumenyume? Hata ukinunua pikipiki huwezi "kumalizana" na mwenye pikipiki halafu useme "kwa kuwa hutaki shinda" unaenda TRA kuangalia usajili wa pikipiki kama aliyekuuzia ndie alikuwa mmiliki halali. Too late! Huwezi kufanya hivyo. Sembuse kiwanja?Ndugu wapendwa,
Kuna suala moja naona kama lina walakini, na ningepata wasaa ningemshauri Waziri wa Ardhi aliangalie kwa makini.
Mtu umejipinda ukapata pesa kidogo ukaingia maeneo ya Mbezi, Bonyokwa, Goba n.k kutafuta kipande cha Ardhi ili ujenge maana kodi haziaminiki mjini.
Unamalizana mwenye ardhi na kupitia michakato yote pale kijijini ili isiwe tabu baadae.
Kwakua hutaki shida unakwenda ardhi ili kukipima upewe hati kabisa,
Cha ajabu watu wa arhi wanakuja kukuambia kua kwa mujibu wa "Master Plan" ya mji, hapo ulipopata ni eneo la wazi/soko/barabara,
Swali langu ni kua, kwanini basi hizo master plan zisiwekwe huko kijijini ili kila anaenunua ajue hukohuko kua kaliwa?
Serikali ya kijiji inakupitisha kununua kwamba ni mahali halali,
Serikali kuu inakuja kukuambia kua sio, hapa imekaaje?
Kuna masuala ya kuchukua location ya eneo (GPS) ili ukapate uweli kuhusu hilo eneo wizarani, but ni wangapi wanajua kuhusu hii kitu?
Ni kweli unaweza kuomba amendment ya hiyo plan ikafanikiwa?
Shark, sheria ina tatizo gani hapo specifically? Umesema "unamalizana na mwenye ardhi" halafu unaenda Ardhi kutafuta hati unakuta "umeliwa." Sasa hapo ndugu yangu, tatizo ni sheria au ni wewe uliyefanya mambo kinyumenyume? Hata ukinunua pikipiki huwezi "kumalizana" na mwenye pikipiki halafu useme "kwa kuwa hutaki shinda" unaenda TRA kuangalia usajili wa pikipiki kama aliyekuuzia ndie alikuwa mmiliki halali. Too late! Huwezi kufanya hivyo. Sembuse kiwanja?
Kaangalie allocation ya matumizi ya kiwanja kwenye master plan kabla hujanunua, na kabla ya kulaumu sheria.
<br />A very big concern. Sheria ya ardhi ina matatizo makubwa. Haikufanyiwa utafiti wa kutosha kabla ya kuipitisha. Waziri Tibaijuka ayaangalie haya mapungufu ni ya msingi sana tena sana. Lakini wana muda huo?
Hapo ndipo panapotokea tatizo, ushanunua halafu ndio baadae unakwenda kwa hao wataalamu wa ardhi ambao wanakuambia kua umeuziwa barabara,Tumia wataalamu wa ardhi ilikuepuka matatizo baada ya kununua kiwanja.