Sheria ni msumeno, kweli??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ni msumeno, kweli???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Dec 21, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Zamani tuliaminishwa kuwa sheria ni msumeno kwa maana kuwa hukata mbele na nyuma na kwamba hauchagui pa kukata.

  Lakini taraaatibu ukweli nimeanza kuujua kuwa sheria siyo msumeno. Baada ya vuguvugu la Richmond na EPA tuliambiwa na watawala wetu kuwa kama serikali ingeamua kuwakamata wale wote waliokuwa wanatuhumiwa basi nchi ingeyumba, wakati huo huo serikali hiyo hiyo iliendelea kuwakamata na kuwanyanyasa raia wake waliokuwa wanadai haki zao bila kuvunja sheria (mfano wanafunzi wakidai walipwe fedha za kujikimu, wazee wakidai mafao yao, n.k)
  Leo tena wakati tunatafakari maamuzi yaliyotolewa kwenye mahakama moja ya nchini Uingereza shirika la kuzuia magendo la huko SFO liliingia mkataba wa kiharamia na wezi wetu hivyo kutukosesha fursa ya kuwajua wale wote waliohusika kwenye wizi wakati wa ununuzi wa Radar, hawa bila shaka walifanya hivyo kwa ombi la serikali ya Tanzania kwani hii kesi ingesikilizwa mahakamani serikali yetu ingevuliwa nguo, tunajua Mkapa, Mramba, Chenge na wengine wengi walihusika katika mpango mzima wa kutuibia, lakini kwa sababu wana fedha hawatajulikana na wataendelea kuishi kwa kugharimiwa na walipa kodi masikini wa kitanzania ambao waliwaibia.
  Mkapa analipwa pension kama rais mstaafu, Mramba, Chenge na wengine nao wanalipwa pension kama wafanyakazi wastaafu wa serikali... hawa wamefanya uharifu na wanatesa, kuna wengine wengi wako lupango kwa kutembea na wanawake ambao wateule wetu walikuwa wanawapenda.

  Je kama sheria kweli ni msumeno mbona unakata kwa kuruka ruka, je kuna haja ya kuipitia hii misemo yetu ya kiswahili ili kuweka mambo sawa?
   
Loading...