Habari ya leo ndugu wana jf,
Mimi ndugu zangu napenda kusikia na kusoma maoni yenu kuhusu hili jambo ninalotaka kulizungumzia... Lahusu maeneo yanayopaswa kujengwa mabaa, misikiti na makanisa,
Sheria inasemaje kuhusu hili? mana naona kama hakuna utaratibu mzuri unaosimamia mambo haya, siku hizi makanisa, mabaa na misikiti inajengwa katika makazi ya watu bila hata kujali jamii inayowazunguka.
Kwa mfano hili la mabaa, tena utakuta wanafungua muziki mkuubwa hadi watu wanaona kero,lakini pia sio baa tu.. kwa mfano makanisa pia.. utakuta wamefunga maspika makuuubwa utadhani wanaendesha ibada ya mtaa mzima..hata misikiti pia nayo wameweka maspika yao na kila baada ya muda utasikia wakiswali..tena ile mbaya ni ile ya alfajiri..
Sasa wadau embu niambieni hivi hawa wanaopima na kupanga miji huwa wanafikiria vitu kama hivi? au hawajui ni kero gani zinazotokea?
Kaka hii imani au ndo sheria inavyosema? Bila kua na mtu ka presda Kagame Bongo haiendi? Ki msingi bongo hakuna plani watu wanajifanyia ka watakavyo!!Mkuu ziraili hayuko mbali na wewe. Yaani unagroup pamoja bar na nyumba za ibada? Mbona hujachanganya magereji, filling stations nk? Piga magoti mwombe Mungu radhi. Makanisa na misikiti inatakiwa ijengwe sehemu yoyote ili watu wasicheze mbali na Mwenyezi Mungu.
Kaka hii imani au ndo sheria inavyosema? Bila kua na mtu ka presda Kagame Bongo haiendi? Ki msingi bongo hakuna plani watu wanajifanyia ka watakavyo!!
Sio kihivyo mjomba,Mkuu ziraili hayuko mbali na wewe. Yaani unagroup pamoja bar na nyumba za ibada? Mbona hujachanganya magereji, filling stations nk? Piga magoti mwombe Mungu radhi. Makanisa na misikiti inatakiwa ijengwe sehemu yoyote ili watu wasicheze mbali na Mwenyezi Mungu.
Sio kihivyo mjomba,
Sasa kama mi nimelala halafu nikasikia muazana alfajiri na mimi si muisilamu hiyo si kero? au umepumzika ukasikia watu wanaimba kwa sauti sana kanisani na wewe si mkristo na unahitaji utulivu, si kero hiyo? Hiyo ni mifano tu..hayo magereji na filling station zote zinaingia kwenye mada hii... Je sheria inasema nini? achana na suala la imani