Babu la Bara
JF-Expert Member
- May 24, 2017
- 529
- 575
Habari wanaJF,
Mi ni mmoja wapo wa wanachama wa NHIF, nikiwa mfanyakazi wa serikali kuu.
Leo hii mmoja wa wategemezi wangu anaumwa so akaenda hospital kupata tiba. Kufika kule akaambiwa kadi yake imesitishwa kwa maana haisomi kwenye mtandao wa NHIF. Akanipigia simu kujua kinachoendelea.
Kwa kuwa na mimi sijui kilichotokea ikabidi niulizie kwa wenzangu. Majibu niliyopata ni kuwa mwajiri hajapeleka mchango wa mwezi mmoja, nahisi ni mwezi uliopita. Na sio mimi tu hata wengine imewakumba toka last week. Ikanibidi nitoe pesa mfukoni kumtumia huko halipo ili apate huduma.
-Hivi, kwanini kosa la mwajiri linamwathiri mwanachama ambaye tena kalazimishwa kujiunga na mfuko huo na hana access ya hayo makato?
-Kwanini wasitoe huduma kwanza mengine yafuate? Kwa mtu anayehitaji huduma ya haraka na hana pesa kwa muda huo zaidi ya kadi anafanyaje?
-Nimefuatilia NHIF kwa kuongea nao, wanasema sheria ndio inawataka wafanye hivyo. Katika hili tatizo ni kuwa wakipelekewa tena makato yetu, wanayachukua japo katika kipindi hiki ninakosa huduma yao.
Sasa sio wizi huu jamani? Kwanini wasiturudishie makato yetu kama kweli wao ni wastaarabu?
NHIF ACHENI WIZI, KAMA MAKATO YAMECHELEWA NA MWANACHAMA KAKOSA HUDUMA, MNATAKIWA MRUDISHE HAYO MAKATO YA MWEZI HUSIKA.