Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 788
- 1,015
Wasalaam na jpili njema wadau !
Kuna wengine wataanza kuhoji kwanini tunaongea vitu vya imani imani hapa, lakini kabla hujahoji jiulize jambo moja muhimu hapa,
*Kwanini viongozi wenyewe wanaapa kuilinda katiba kwa kutumia vitabu vitakatifu ?
Moja kwa moja wanaonyeaha kuwa kwa kuilinda katiba watakuwa wamempendeza hata muumba wao bila shaka.
Ingekuwa Mungu yupo mbali ama kinyume na katiba basi kamwe asingeruhusu tumuhusishe nayo, ilo la kwanza, (1) KATIBA NI MAPENZI YA MUNGU.
Kwa wafuatiliaji wa historia ya ustaarabu, siasa , demokrasia na utawala wa serikali , mambo yote haya ya sheria awali kabisa yalikuwa derived from the TORAH, yaani torati , ambacho ni kitabu chenye sheria zinazopaswa kutuongoza tulizopewa na MUNGU Baba mwenyewe. Kitabu hichi kinaaminiwa na kutumiwa na dini zote mbili ; waislamu na wakristo.
(2) Sio kweli kwamba kila mtu ni mpenda kufuata sheria na utaratibu ,kuna watu ni mbwa mwitu wakali, hata ulaji wao hawa hawatengi sahani mezani na kula kistaarabu, ulaji wao ni wa kunyang'anyana minofu midomoni. Ndio maana hata ukiwapa vyeo bado wanasigana humo kwa humo kugombania ulaji amabao upo mezani mwao tayari !!
Kundi hili lisilopenda utaratibu wala haliwezi kufuata utaratibu halina kabisa urafiki na kanuni kali ambazo zitawalazimisha wawe watulivu hivyo ni ujinga kuwasubiria hawa watu watupe KATIBA kwa ridhaa yao.
###
Kundi hili hujulikanaa pia kama uzao wa nyoka, ndio walewale, wana sumu chini ya ndimi.zao na sumu hizi zinatabia ya kuwasha na kuwalazimisha kufanya uovu. Hivyo sio watu watakaaokubali kamwe kuwekewa sheria kali kwani kwa maumbile yao ya nyoka sheria hizo zitakula kwao wenyewe,
HIVYO ANAEKWAMBIA ANAJIVUA GAMBA SIO MTU WA SHERIA HUYO.
Ni bahati nzuri kwa sisi tunaoelewa tunaona viashiria vyao hata wakijaribu kuficha sura zao halisi, mfano wanapoambiana wale lakini wasivimbewe, kwa kauli hii hapo hakuna hofu ya MUNGU wala huruma na upendo wa kweli kwa watanzania bali ni unafiki mtupu.
KATIBA NI JUHUDI ZA BINADAMU WAKRISTO NA WAISLAMU WENYE HOFU YA MUNGU SIO KITU KITALETWA NA UZAO WA IBILISI KWETU HIVYO YATUPASA SISI WATU WA KAWAIDA KABISA TUIPIGANIE KWA PAMOJA.
Nyoka na mbwa mwitu ni lawless society, hawana utii kwa sheria.
www.jamiiforums.com

Ukweli mchungu: Ngumu lakini ndivyo ilivyo...
Jiulize swali hili kwanza Je, kwa wale wa mama na wadada waliowahi kupata matatizo ya uzazi na hatimae katika kuzunguka mwisshoni wakajikuta kwa waganga wa kienyeji ma kubahatika kupata watoto huko, je watoto hao kwa asilimia ngapi walitoka kwa MUNGU BABA muumbaji wetu? Ni dhahiri kuwa dini...
Kwenu Polepole, Ndugai na kampani yenu yote: A conspiracy theory
Nawasalimu kwa heshima zote enyi waheshimiiwa ! Lakini mtanisamehe kwa wale wenzetu waislam sijabahatika kuijua quran kiasi cha kukopa mistari yake hapa, mniwie radhi nitatumia biblia peke yake. Kwa kuanza nimuongelee mwalimu JK Nyerere katika moja ya hotuba zake alikuwa anaongelea jambo...
Serikali na mwarobaini wa matatizo yetu
Asalaam. Alekyum, BWANA. YESU KRISTO ATUKUZWE ! Nawasalimu wote na nnawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki. MADA HII ITAONEKANA KAMA YA KIIMANI ZAIDI, LAKINI HEBU VUTA SUBIRA UISOME KWANZA Leo naomba niwaletee tafakuri hii ndefu sana na inayohitaji utulivu wa fikra. Na kwa wale ambao...