Sheria hii ya kubaka ibadilishwe, inaumiza vijana wetu.

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,894
Wandugu, I declare interest, mimi ni mdau wa sheria kwa miaka mingi. nimekutana na kifungu cha 130(2)(e) of the Penal Code kinachotoa adhabu ya kosa la kubaka kwa mtu mzima (kuanzia 18 years and above) atakayefanya mapenzi na binti wa miaka 18 ambaye sio mke wake, hata kama ni kwa ridhaa yake. nimewahi kutembelea magereza mara nyingi, na zamani nilishaprosecute kesi nyingi na vijana wa miaka kati ya 18 hadi 25 wengi tu wameenda jela miaka 30. tafakari yafuatayo.

1. kijana wako wa miaka 20 amekutana na binti wa miaka chini ya 18, wakatongozana, au binti kamfuata yeye mwenyewe nyumbani kwake wakafanya mapenzi kwa kukubaliana kabisa na si kwa kubakana, akikamatwa anaenda jela miaka 30.

2. kuna baadhi ya mikoa, ipo mila na desturi unapotaka kuoa unamwita binti geto kwako kwa makubaliano, au binti anahamia kwako halafu wewe unatuma watu asubuhi wakawaeleze wazee wake kwamba yupo kwako na unataka kutoa mahali....hapo ridhaa haijafanyika na ameshalala kwako, umebaka, ni 30 years.

3. kijana wa miaka 19 hadi 22 akili yake haina tofauti sana na binti chni ya miaka 18, wengi bado watoto tu na wapo katika nyakati za kujaribu kujifunza kufanya mapenzi, je, adhabu ya miaka 30 ni fair? (atatoka akiwa na 45 to 50 years).

USHAURI

1. sishabikii uzinzi kwa watoto wetu, sheria hii ilitungwa kwa shinikizo la wanawake baada ya mikutano yao ile ya beijing, wanawake walishangilia sana wakifikiri wanawakomoa wanaume, matokeo yake, vijana wanapofungwa miaka 30 watu wa kwanza kutoa machozi ni mama wa hao vijana. sasa huwa nashangaa wanaume tumekomolewa namna gani?

2. napenda vijana hao hata kama wadogo, wapate adhabu, lakini isiwe 30 years, wapate hata 5 years walau hata 4 years. miaka 30 jela kwa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, unafungwa sawa tu na mbakaji wa kawaida, sio fair. WAPUNGUZE MIAKA JELA ILA ADHABU IWEPO.

3. tunatakiwa kuja na definition mpya ya kubaka, statutory rape ililenga wababa watu wazima wanaolaghai watoto wa shule kufanya nao mapenzi, matokeo yake, wanaokamatwa wengi ni watoto wadogo tu wa miaka 19 hadi 25 na ndio wanajaa jela...hao watu wazima wengi kwanza wana hela kesi zao wanahonga zinayeyuka. vijana wetu wamejaa jela huko kwa statutory rape 30 years, kwanini? hebu tujaribu kufikiria hapa.
 
ngoja ninyamaze tu maana
nimeshawahi kuendesha mashitaka ya vijana wengi tu. kwa wale wasio wanasheria, kuna rape/kubaka kwa aina mbili.
1. kubaka kwa kumkamata na kumlazimisha mwanamke bila yeye kuridhia

2. kubaka kwa kigezo cha umri (statutory rape) yaani kutembea na binti chini ya 18 hata kama ameridhia, hata kama yeye ndio alikufuata home akaomba umfanye, hata kama mnapendana, achilia mila na desturi zote...maadamu huyo sio mkeo. kubaka kote kuwili huko ni 30 years. sasa wanaopata shida zaidi ni watoto wadogo tu hao waendesha bodaboda, failures za form four hao wanaozurura tu hao....ila mibaba miwatu wazima kama mimi hawafungwi kwasababu hata hayo mambo wanayafanya kwa akili na ujanja hawakamatwi, labda awe mtu wa kijijini. wanaokamatwa ni watoto wadogo.s heria ililenga watu wazima wanaoharibu wanafunzi hao waliolengwa haiwapati ila vijana wetu wanajaa jela.
 
mnajisikiaje mnavyoona vijana wadogo wakipewa miaka 30 jela kwasababu ya kutembea na binti ambaye walielewana?
 
Back
Top Bottom