Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,142
- 26,132
wanabodi,
Serikali ya awamu ya 5 imejipambanua kwa kubana matumizi hasa kwa mambo yasiyo na ulazima.Katika maeneo ambayo serikali imeshagusa ni pamoja na safari za nje,warsha na makongamano,sherehe za kitaifa kama Uhuru na Muungano.
Pamoja na kugusa sherehe za uhuru lakini Mwenge wa uhuru ambao kimsingi hugharimu pesa nyingi kuliko hizo sherehe zote kwa pamoja kwa kiwango kikubwa sana umeachwa.Mfano kwa mwaka 2015 mwenge wa uhuru ulichukua zaidi ya miezi 6 mpaka kufikia kilele.Hii ni ishara tosha kuwa mwenge huu una gharama kubwa bila kuwa na matokeo yoyote chanya na yenye kuridhisha.
Mwenge wa uhuru umelalamikiwa sana na wadau wengi kama chaka la kutumia pesa za serikali,wakafika mbali na kushauri mwenge huu uwekwe makumbusho ili basi iwe sehemu ya kumbukumbu na si kuuzungusha nchi nzima.Mh Lymo,aliyekuwa mgombea urais wa TLP alifika mbali zaidi na kusema ni sawa na kutufanyisha ibada ya moto watanzania kwa kitendo cha kuukimbiza nchi nzima.Pamoja na malalamiko mengi,serikali hii ya kubana matumizi imeoneshwa kutokujali au kuguswa na jambo hilo kabisa.Kama waliona kuonesha bunge live ni gharama ila hawaoni kama kuzungusha mwenge live nchi nzima ni gharama,hapo ndio wenye kufikiri nje ya box tukaanza kutupia jicho la mashaka.
Katika ufuatiliaji wangu wa mwenendo wa mwenge nimebaini kuwa mwenge umekuwa ukitumika kama sehemu ya harakati za kueneza chama cha mapinduzi.Sherehe za mwenge kwa kiwango kikubwa zimekuwa kama sherehe za chama cha mapinduzi.Wakuu wa wilaya ndio wamekuwa wakipokea mwenge kwenye wilaya zao na hatimaye mkuu wa mkoa.Hawa wote na wapambe wao ambao ndio huchukua jukumu la mwenge kwa kipindi chote ambacho mwenge unakuwa maeneo yao ni makada wa chama cha mapinduzi.Hata pale mwenge unaposhuka kwenda chini zaidi,viongozi wa ccm wa ngazi mbalimbali ndio huwa wanahusishwa.Ni kawaida sana kukuta sherehe za mwenge zimepambwa na nguo za kijani na njano kwa wingi.Imeshakua kama utamaduni kuwa wanaccm ndio wenye sherehe pale mwenge unapofika eneo fulani.
Kama serikali ilivyozuia bunge live kulinda maslahi ya chama na serikali,ndivyo ilivyoshindwa kuutumbua mwenge ili kulinda uhai wa chama.Hii ni rahisi,unatumia gharama za serikali kufanya uenezi wa chama,logic iko hivyo na ndio maana pamoja na gharama kuwa kubwa pasipo na tija,athari mbalimbali(uzinzi na ulevi uliopindukia pale mwenge unapolala) lakini bado serikali imeshindwa kuuondoa mwenge.
NB;Iruhusu akili yako iwe huru ndio uchangie
Mods msipende kukurupuka kubadili tittle za waanzisha thread.Kwa heading mliyoniwekea inaonesha kuwa sipingi mwenge ila napinga maudhui ya mwenge,jambo ambalo si kweli kama ukisoma content.kwenye content naelezea kwanini serikali imesita kuzifuta mbio za mwenge.Tittle yangu ilisomeka ''nyuma ya pazia;mwenge wa uhuru'' kabla mods hamjaharibu.