Sherehe za Muungano Zanzibar, wananchi wasusia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sherehe za Muungano Zanzibar, wananchi wasusia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaimati, Apr 27, 2011.

 1. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tamko la Jumuiya za Kiislamu Zanzibar juu ya sherehe za Muungano

  Sherehe za Muungano Zanzibar, wananchi wasusia

  Posted on April 26, 2011 by zanzibarpost

  [​IMG]
  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, akiwa kwenye sherehe za mwaka huu za kuadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo hii.


  MVUA kubwa iliyoanza ghafla leo hii ilisitisha sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Aman mjini Zanzibar.
  Sherehe hizo zilizoanza majira ya saa 3:00 asubuhi, ziliingia dosari hiyo huku tayari mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete, akiwa ameshakagua gwaride na kujumuika na viongozi wenzake katika jukwaa kuu.


  Viongozi wengine waliokuwepo katika sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wake wa Kwanza, Seif Sharif Hamad, na Makamu wake wa Pili, Balozi Seid Idd.

  Wengine waliokuwepo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Anna Makinda, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange, Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa na Rais mstaafu wa awamu ya sita wa SMZ Dk Salmin Amour.

  Vilevile walikuwepo viongozi wa vyama vya siasa, kamavile mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Katibu mkuu mstaafu wa CCM Philip Mangula, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia na wanadiplomasia wanaoyawakilisha mataifa yao yao nchini.

  Rais Kikwete aliingia uwanjani hapo majira ya saa 4:00 asubuhi akiwa kwenye gari la wazi na kuwapungia mamia ya wananchi waliokuwepo na baadaye kukagua gwaride. Baada ya hapo gwaride lilipita mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa kasi na mwendo wa pole.

  Ulipowadia wakati wa halaiki iliyoshirikisha wanafunzi 500, ndipo mvua ilianza kunyesha na baadaye kuivuruga kabisa sherehe hiyo.

  Kwa mujibu wa ratiba hiyo kipindi kilichokuwa kikifuata ni ngoma za asilia. Lakini mvua ilipozidi, washereheshaji walitangaza kukatisha sherehe hiyo na viongozi wakaanza kuondoka.

  Kauli mbiu ya sherehe hiyo ilikuwa ni “Miaka 47, Tuwaenzi Waasisi Wetu, Tudumishe Muungano, Matunda ya Miaka 47 ya Mapinduzi naMmiaka 50 ya Uhuru. Amani, Utulivu na Maendeleo ni Matokeo ya Muungano Wetu.”

  Lakini sherehe zenyewe zilionekana kudorora hasa kutokana na mahudhurio hafifu ya wananchi. Sehemu mbalimbali za uwanja huo zilionekana kuwa wazi, huku hata wafuasi wa CCM waliokuwa wamevaa sare zao, nao wakiwa wachache. Ukiacha wanafunzi waliokuwa wamevaa sare nyeupe na wale waliovaa sawa na rangi za bendera ya taifa na wale wafuasi wa CCM, maeneo mengine ya uwanja huo yalikuwa wazi.

  Taarifa zaidi zinasema kuwa Serikali ilituma mabasi zaidi ya 20 vijijini ili kukusanya watu kwa ajili ya kuhudhuria sherehe hizo, lakini hawakufika.

  Hali hiyo imejitokeza huku kukiwa na manung’uniko mengi kutoka kwa wananchi wa Zanzibar, wakitaka Muungano huo ufanyiwe tathimini upya.

  Wakati huo huo, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar umetoa tamko kuhusu hali ya Muungano. Huku zikitoa ushahidi wa tume kadhaa zilizoundwa ili kutafuta maoni ya wananchi, kama vile Tume ya Jaji Nyalali na ile ya Jaji Kisanga, jumuiya hizo zimesema kuwa Muungano kati yaTanganyika na Zanzibar umekosa kukubalika na Wazanzibari tangu siku yake ya kwanza hadi leo.

  Huku wakiilaumu CCM kwa kuhodhi Muungano, wamesema kuwa nguvu za Zanzibar katika kama mshirika mmoja kamili wa Muungano huo hazipo kwa kuongezewa mambo ya Muungano na yale yasiyo ya Muungano yamekuwa yakiilemea Zanzibar.
  “Kwa karibu miaka yote 47, Muungano huu umekuwa ni miliki ya chama kimoja cha siasa cha CCM, ukitoa miaka michache ya 1964-1977.”

  Jumuiya hizo zimetaka kuwepo kwa majadiliano ya Muungano ambapo wametaka pia nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Muungano kama makamu wa kwanza wa Rais irudishwe.

  “Mjadala wowote ule wa Muungano, urudishe nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Muungano na sio ilivyo hivi sasa ambapo Rais wa Zanzibar hana maana wala amri yoyote ile katika Muungano,” imesema taarifa hiyo
   
Loading...