Shemeji ananichonganisha na mke wangu

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,880
Salaaam kwenu wakuu,

Mimi ni kijana, namshangaa shemeji yangu huyu wa kike amekuwa akinichonganisha na mke wangu mara kadhaa.

Baada ya kumuoa dada yeke akahamia kwangu wakati anasoma chuo kimoja hapa DSM.Tabia zake zilikuwa za visa visa tu kwanza haniheshimu,siku moja amenikuta naongea na mama mwenye nyumba wakati huo nimepanga akataka kunivamia eti kwanini naongea na yule mama mwenye nyumba.

Hayo yakapita sasa akawa anataka kuolewa na jamaa ambaye nilisoma naye cha ajabu anakuja kunihoji eti nimpe wasifu wa huyo jamaa,well mimi nilimwambia tu in short kwamba huyo jamaa me nilikuwa sina ukaribu naye wakati tupo chuo, kama unavyojua relations za watu sio za kuingilia sana.

Wakati ninaishi naye alikuwa na tabia ya kumpiga mwanangu tena hata nikiwepo sikutaka kumkaripia bali nilienda kwa wife nikamwambia amkanye mdogo wake kupiga wanangu. Well siku zimenda ameolewa sasa yupo kwake huko mimi sijawahi kukanyaga huko wala sijui anaishi wapi.

Cha ajabu mpaka saivi hana kazi sasa jana tumekaa vizuri na wife tunapiga story mara anaanza kunishutumu kwamba oooh mbona humtafutii mdogo wangu kazi,nikamjibu ebooo mtu anafamilia yake mimi naanzia wapi kuanza kumtafutia kazi? Lakini nikamjibu kama anaweza kufanya kazi mkoani mwambie then mimi nitamtafutia kazi,ila akubaliane kwanza na mumewe.

Kwa kuwa ni married kaanza ooooh una upendeleo kwanini usimtafutie hapa DSM unampeleka mkoani daaaah!Sasa tangu jana mpaka leo ameninunia.
Eti wajameni kosa langu ni lipi hapo?
 
hivyo vituko anavyokufanyia ni maagizo kutoka juu.kama wife alivyomalizia kuwa kwa nini humtafutii mdogo wangu mme?

swissme
 
We una bahati mbaya, mi nimeishi na dada mkubwa wa mke wangu kwa muda sasa. Kwa kweli anaheshima kuliko mdogo wake. Na anampenda mwanangu sana. Kwa ujumla sitaman aondoke kwangu coz mi natumia pombe mke wangu ana ulokole flan nikirud nimeshakunywa ni ngum hata kuniandalia chakula ila kwa shem anakuwa anajali sana. Ila kwa kuwa huyo shem wako kaolewa we achana naye hakuhusu kwa lolote huyo ni mke wa mtu.

Duc in Altum
 
Mwache.anune lakini usiingilie maisha ya ndoa yake unaweza mtafutia kazi mumewe asikuelewe au labda mumewe hataki afanye kazi......ingekuwa mumewe kakushirikisha kwenye hilo ingekuwa hakuna shida....mwanamke anayejitambua hawezi kununa kwa hilo angeweza kuongea na mume wa mdogo wake wakikushirikisha wewe
 
tatizo lako wewe mleta mada umepoteza mfumo dime. hiyo imesababisha mkeo na Dada take kuongea chochote wanachojisikia. jaribu kuwachenjia kidoooogo.
 
Be a real man.Kuwa na maneno machache yenye maana.Alaf yaelekea umeingia kwa ndoa ukiwa mdogo sana.Kaa na mtu mzima unayemuamini akuelekeze jinsi ya kuishi na mke.
 
Salaaam kwenu wakuu,

Mimi ni kijana, namshangaa shemeji yangu huyu wa kike amekuwa akinichonganisha na mke wangu mara kadhaa.

Baada ya kumuoa dada yeke akahamia kwangu wakati anasoma chuo kimoja hapa DSM.Tabia zake zilikuwa za visa visa tu kwanza haniheshimu,siku moja amenikuta naongea na mama mwenye nyumba wakati huo nimepanga akataka kunivamia eti kwanini naongea na yule mama mwenye nyumba.

Hayo yakapita sasa akawa anataka kuolewa na jamaa ambaye nilisoma naye cha ajabu anakuja kunihoji eti nimpe wasifu wa huyo jamaa,well mimi nilimwambia tu in short kwamba huyo jamaa me nilikuwa sina ukaribu naye wakati tupo chuo, kama unavyojua relations za watu sio za kuingilia sana.

Wakati ninaishi naye alikuwa na tabia ya kumpiga mwanangu tena hata nikiwepo sikutaka kumkaripia bali nilienda kwa wife nikamwambia amkanye mdogo wake kupiga wanangu. Well siku zimenda ameolewa sasa yupo kwake huko mimi sijawahi kukanyaga huko wala sijui anaishi wapi.

Cha ajabu mpaka saivi hana kazi sasa jana tumekaa vizuri na wife tunapiga story mara anaanza kunishutumu kwamba oooh mbona humtafutii mdogo wangu kazi,nikamjibu ebooo mtu anafamilia yake mimi naanzia wapi kuanza kumtafutia kazi? Lakini nikamjibu kama anaweza kufanya kazi mkoani mwambie then mimi nitamtafutia kazi,ila akubaliane kwanza na mumewe.

Kwa kuwa ni married kaanza ooooh una upendeleo kwanini usimtafutie hapa DSM unampeleka mkoani daaaah!Sasa tangu jana mpaka leo ameninunia.
Eti wajameni kosa langu ni lipi hapo?

HUNA KOSA HAPO MKUU...SEMA MKEO NDIO ANAKOSA..TENA KOSA KUBWA TUU LA KUINGILIA MAISHA YA FAMILIA ZA WATU...HAIWEZEKANI AACHE KUFUATILIA MATATIZO YA FAMILIA YENU ANAANZA KUINGILIA MATATIZO YA FAMILIA YA WATU...

BY THE WAY...KWANINI USIMTIE MIMBA SHEMEJI YETU ATULIE AWE BIZE NA NDIMU NA UDONGO WA PEMBA NA VICHEFUCHEFU VYA HAPA NA PALE?

KUHUSU KUMSAIDIA SHEMEJI YAKO KAZI....UNAWEZA AU PIA HUWEZI KUMSAIDIA...WASWAHILI WANASEMA CHA KUOMBA HAKINA NYONGEZA...KAOMBA KAZI KAPATA SUMBAWANGA ATULIE AFANYE.
PIA MUULIZE SHEMEJI YETU YANI MKEO...VIP UKIMTAFUTIA KAZI AKAPATA NA JAMAA YAKE YANI MUME WA MDOGO MTU AKACHUKIA NA KUMUACHA MDOGO MTU KWA KUMTUHUMU ANATEMBEA NA WEWE YEYE MKEO ATASEMAJE?
 
Wanawake tuishi nao kwa kutumia akili sana,,,jambo dogo km hilo hata usiumize kichwa angalia familia yako mkuu km jambo lolote unaona lina utata liache tu km lilivyo
 
Back
Top Bottom