Shein: Sitikiswi na staili ya utumbuaji majipu ya Magufuli, kila mtu na aina yake ya uongozi

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Dk. Shein akihojiwa na Tido Mhando amesema kuwa hatikiswi na staili ya Magufuli ya uongozi kwa kuwa kila mtu na staili yake ya uongozi duniani akitolea mfano wa Hitler alivyokuwa akiongoza na kusema hizo ni moja ya aina nyingi za uongozi zilizopo duniani

Amesema amefanya kazi na Magufuli kwa kipindi kirefu awamu zilizopita na anamfahamu vizuri na majipu yanayotumbuliwa anayatumbua kisheria bila uonevu

Pia amesema sio kwamba Zanzibar hakuna hatua zinazochukuliwa kuhusu 'majipu' ya huko bali ana namna yake ya kutumbua na waandishi wa habari wakitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuhusu ukwepaji kodi huko basi wafuatilie na watajua na sio kujikita tu bara.

well said, coverage ya habari za Zanzibar Tanzania bara iongezwe ,katika magazeti ,television ,pia yapo mambo ya kusisimua na kuburudisha yapo bara mengine yapo zenji ,mfano tamasha la ziff.huku bara ziko timu za simba na yanga .
 
Keshamchoka Faru John...eti mtu anajitengenezea sherehe zake za Mapinduzi kwake Usukumani
 
Kwa maana Shein anamfananisha JPM na Hitler??? Au sijaelewa vizuri
Dk. Shein akihojiwa na Tido Mhando amesema kuwa hatikiswi na staili ya Magufuli ya uongozi kwa kuwa kila mtu na staili yake ya uongozi duniani akitolea mfano wa Hitler alivyokuwa akiongoza na kusema hizo ni moja ya aina nyingi za uongozi zilizopo duniani

Amesema amefanya kazi na Magufuli kwa kipindi kirefu awamu zilizopita na anamfahamu vizuri na majipu yanayotumbuliwa anayatumbua kisheria bila uonevu

Pia amesema sio kwamba Zanzibar hakuna hatua zinazochukuliwa kuhusu 'majipu' ya huko bali ana namna yake ya kutumbua na waandishi wa habari wakitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuhusu ukwepaji kodi huko basi wafuatilie na watajua na sio kujikita tu bara.

Tido ananiboa sana woga wake akiwa mbele ya hawa wakubwa!! Kukaa kote kwenye media house kubwa duniani bado anatetema hivyo?
 
Back
Top Bottom