Shein ni mwanasiasa au analazimishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shein ni mwanasiasa au analazimishwa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ochu, Jun 25, 2010.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  HATUA ya Makamu wa Rais, Dk. Dk Ali Mohamed Shein kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa Zanzibar, imeelezwa kusukumwa na wagombea Urais wa Jamhuri walioko Bara, Raia Mwema limeelezwa.
  Raia Mwema limefahamishwa kwamba, ukimya wa Dk. Shein na kutokuwa kwake na makundi, pamoja na elimu yake, kungemfanya kuwa Rais wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kama akiendelea kufanyakazi Bara kwa miaka mingine mitano ijayo.
  “Wanaowania Urais kumrithi Kikwete wana nguvu sana, na sasa wanajipanga kwa kila njia…. UnajuaDk. Shein hakuwa chaguo la wanamtandao lakini kutokana na nguvu ya wazee na nguvu ya Mkapa (Benjamin Mkapa, Rais mstaafu), Kikwete alilazimika kumpendekeza,” anasema kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM Zanzibar.

  Kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye ni kada wa siku nyingi wa CCM, Dk. Shein hakuwa na nia kabisa ya kuwania nafasi Zanzibar, pamoja na kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliowahi kusukumwa kuchukua fomu mwaka 2005 kumrithi Mkapa, lakini heka heka za wakati huo zikaonekana kuwa nzito kwake kabla ya kuamuliwa kuendelea kuwa Makamu wa Kikwete.

  “Baada ya Mkapa kumaliza muda wake, ilikuwa ni zamu ya Zanzibar kutoa Rais na Dk. Shein alitajwa sana kuweza kuchukua nafasi hiyo kwa kupanda kutoka Makamu wa Rais, lakini kilichotokea kila mtu anajua, maana Dk. Salim Ahmed Salim ambaye alibaki katika tatu bora alikwisha kushughulikiwa na wanamtandao.
  “Baada ya Dk. Salim kukwama, na Dk. Shein kutojitokeza mwaka 2005, hatua ya kuendelea kuwa Makamu wa Rais, ingemfanya kuwa na uzoefu wa miaka 15 na kwa uwezo wake na uadilifu, isingekuwa jambo rahisi kumnyima urais wa mwaka 2015 maana Wazanzibari wasingeelewa japo hata sasa kuna kazi kubwa kwao kuzuia Mzanzibari,” anasema mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kutoka Zanzibar.
  Wanasiasa wanaotajwa sana kuwania kumrithi Kikwete na ambao wanaelezwa kuwa na nguvu kubwa ni pamoja na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ambaye sasa ameanza kutajwa kama mstaafu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi. Anatajwa pia Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

  Taarifa zinasema wanaomsukuma Dk. Shein kwenda kuwania Zanzibar, wamepania kwa nguvu zote kukabiliana na vikwazo vilivyoanza kujitokeza kikiwamo kile cha kudai kwamba hana kitambulisho cha ukaazi cha Zanzibar na hakujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura Zanzibar, mahali ambako atalazimika kupigiwa kura bila kupiga.

  Lakini akichukua fomu ya kuwania kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar juzi, Jumatatu, mjini Zanzibar, Dk. Shein alisema kwamba hakujiandikisha kupiga kura Zanzibar kwa zaidi ya chaguzi mbili sasa, lakini huko si kuvunja Katiba wala sheria za uchaguzi na kumuondolea sifa ya kuwa Rais wa Zanzibar.

  “Wapo watu wanasema hivyo kuwa mimi sijajiandikisha kupiga kura Zanzibar ...nimekutupa kwetu....Si kweli, mimi naongoza kwa kuwasaidia wananchi wa kwetu Mkanyageni na wale ambao hawajui Katiba wakasome wasikurupuke tu,” alisema.

  Alisema ameingia katika kinyang’anyiro hicho kwa utashi wake mwenyewe, pamoja na kuwapo taarifa za karibu kabisa kwamba hakuwa amejiandaa kabisa kuwania nafasi hiyo.
  “Namalizia kwa kusisitiza niliyosema mwanzoni kuwa uamuzi huu nimeufanya mwenyewe baada ya kutafakari kwa makini na kupima uwezo wangu na kuzingatia mapenzi kwa chama changu na kwa Zanzibar na imani ya wana CCM wenzangu waliyonayo kwangu. Hakika nimetiwa moyo sana na imani na mapenzi hayo,” alisema Dk. Shein katika hotuba yake ambayo imechapwa kwa kirefu ndani ya toleo hili.

  Dk. Shein amekuwa akitajwa kuungwa mkono na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Karume anayemaliza muda wake, lakini kumekuwa na ukimya kumhusisha Rais Kikwete na uamuzi huo pamoja na kujengwa imani kwamba naye anaunga mkono.

  Hata hivyo, taarifa za Karume kumuunga mkono Dk.Shein zimeanza kutiwa doa na wafuasi wa mgombea mwingine wa Zanzibar ambaye naye alichukua fomu juzi, Dk. Mohamed Gharib Bilal, ambao wanasema kwamba hatua hiyo ya Karume ni sawa na “undumakuwili” kwa kuwa Dk. Salmnin Amour alipomuunga mkono Dk. Bilal alidaiwa kwamba anataka kujenga himaya yake na hivyo kusababisha kuachiwa kwa Karume kuwa mgombea wa CCM.
  “Huu ni undumakuwili, Salmin alipokuwa anamaliza muda wake, alimtaka Dk. Bilal lakini akaambiwa anataka kuweka himaya yake, lakini sasa kwa Karume kumtaka Shein ni sawa… na sisi tunaona anataka kuweka mtu atakayelinda maslahi yake, awaachie Wazanzibari waamue baada ya yeye kumaliza muda wake,” anasema shabiki mmoja wa Dk. Bilal.
  Wengine waliochukua fomu mbali ya Shein na Bilal ni Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud ambaye alisema Zanzibar hivi sasa iko kwenye mazingira mazuri zaidi kuliko nyakati nyingine zozote katika historia yake na hivyo anaamini kuwa anaweza kuiendeleza na kuahidi kuendeleza malengo ya maridhiano kwa amani na utulivu wa visiwa hivyo.

  Mgombea mwingine ni Balozi wa Tanzania Italia, Ali Karume ambaye alisema pamoja na kuwa anaunga mkono maridhiano, lakini suala la kura ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa ya ndio au hapana hawezi kutaja msimamo wake kwa kuwa kura ya maoni itategemea wakati husika.


  Kwa upande wake, Dk Bilal ambaye ni mtaalamu wa fizikia aliahidi kusimamia suala zima la elimu na afya na kusema kwamba endapo Wazanzibari watampa ridhaa ya kuongoza ataendesha nchi kwa misingi ya utawala wa sheria huku akisisitiza suala la nidhamu.


  “Najua kisasi ni haki, lakini mimi alipoingia Rais Amani hajanifanyia kisasi chochote kwa hivyo wananchi wasiwe na hofu juu ya hilo, sitalipiza kisasi,” alisisitiza Dk Bilal.

  Alisema kwamba msimamo kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa itategemea matokeo ya kura ya maoni itakayopigwa Julai 31, mwaka huu, lakini kimsingi anakubaliana na hali ya amani iliyopo.

  Kamishna wa Elimu na Utamaduni, Hamad Bakari Mshindo ambaye naye anawania urais wa Zanzibar alisema kwamba Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuleta maendeleo ikiwemo elimu.

  Kwa upande wake mgombe mwingine, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, alisema msimamo wake katika kura ya maoni yeye binafsi anataka iwepo amani, lakini katika hilo ni vyema Wazanzibari wakafanya maamuzi ya busara yenye kuendeleza umoja na mshikamano.

  Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna alisema uadilifu wake katika chama chake na Serikali ndiyo nguzo yake kuu katika kuwania nafasi hiyo.

  Jumla ya wagombea wanane juzi walichukua fomu huku Waziri wa Elimu ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman akitarajiwa kuchukua fomu yake siku ya Alhamisi wiki hii na mfanyabiashara maarufu, Mohamed Raza akiliambia gazeti hili wakati tukienda mitamboni kwamba naye amekubaliwa na CCM kuchukua fomu ya urais kesho.
  “ Nilikuwa safari. Lakini nimerudi nikakuta barua ya kukubaliwa kwenda kuchukua fomu. Kwa hiyo kifupi ni kwamba nami nimeingia katika kinyang’anyiro,” alisema Raza ambaye mwaka 2005 alinusa na kisha kujitoa katika mchakato kama huu.
  Aliongeza: “ Naijua Zanzibar. Nimetembelea majimbo yote. Nilikuwa mshauri wa Rais kwa miaka 10. Naujua Muungano vizuri, nikipita biashara zangu zote nitaacha kwa kuwa sitaki kuchanganya mambo haya. Lengo kubwa litakuwa ni kuweka umoja.
  “ Sitavumilia unafiki, wala hamtawaona ndugu zangu serikalini na nitainua maisha ya wenye hali ya chini kwa kutoa huduma bora za afya, maji na elimu. Lakini kama maamuzi ya chama yatakwenda kinyume na matarajio yangu, nitayaheshimu .”
  Hayo yakiendelea, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhamed Seif Khatib ambaye amekuwa akitwajwa sana kuwa ni miongoni mwa waliomo katika orodha ya watakaowania urais Zanzibar bado hajatangaza nia hiyo.
   
 2. T

  Tanzania Senior Member

  #2
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  It doesn't matter whether he is/is not. I have not seen anything from those who believe they are politicians. If the current ruling leaders are politicians then, we probably don't need them. Therefore we need the kind of Shein to move forward.
   
 3. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Tata hii mkuu..can you fafanua more?

  Sidhani kama kuna kulazimishwa kwenye siasa....anayo karia yake...asingependa siasa tusingemwona katika safu hizi. Mimi nadhani anapenda siasa na hana mpango wowote wa kutoka huko....kama kuna kulazimishwa nbona wengine hawalazimishwi!!!!??? anapenda sana huyu siasa
  Mix with yours
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi sijawahi kufikiria kama shein yupo kama kiongozi wa nchi.....naona kama mtu tu ambaye huwa anatajwa katika vyombo mbalimbali vya habari...........hata siku moja sijawahi kuona uwezo wake wa kujitambulisha kuwa kiongozi wa ngazi za juu..yaani msaidizi wa rais.....naona kama kiongozi aliye bubu zaidi.............ahutubiapo sijawahi kujisikia kama makamu wa rais anahutubia namuona mtu wa kawaida........sijui kama wazanziberi watakuwa wanamjua zaidi huko kwao...........
  mimi sijui na wala sijui uwezo wake...........................kugombe kwake inawezekana anagombea kwa sababu yeye ni makamu wa rais na sio kwa sababu anauwezo na sifa au anajiandaa ili 2015 aonewe huruma kwani tayari atakuwa alishajaribu 2010 na kama tujuavyo sera na mikakati ya ccm ya kuoneana huruma pengine ndicho anachokisubiri.........
   
 5. f

  fatakifataki Member

  #5
  Jun 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  kaka i think he is in a right way to go, as those leadrship theorist from the greatman theory was placed leaders are born and they exist only wherever there are the need, dr shein namweka hapo kwani ni kweli anahitajika pale zanzibar, hata hivyo smz inahitaji mtu makini kama mzee shein na sio watu wanaotaka kukimbilia pale ikulu pana nini?
   
 6. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hivi umakini wa sheini wenzangu mnautoa wapi? wapi sheil kaomyesha umakini? au mtu kuwa mkimya ndio tafsiri ya makini?
  Mix with yours
   
 7. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Nakuunga mkono kama Z'bar ianataka kiongozi basi huyo ndie kiongozi na anakubalika kote ila ikatokea kuwa Rais wa Z'bar nawapa onyo angalieni CCM kuna majitu mle kazi yao ni kuhalibu tuuuuu ndio watakao kuja haribu uongozi wake kama shein mwenye atalegeza kamba.
   
 8. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Me naona amekaa kama Imamu hivi..au macho yangu jamani
   
 9. N

  Nangetwa Senior Member

  #9
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mpeni nafasi then mhukumuni kwa hayo atayotenda. Nani alikuwa anamjua mkapa sana?
   
Loading...