Sheikh Yahya amfagilia Spika Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Yahya amfagilia Spika Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 27, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  MNAJIMU wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amemwelezea Spika Samuel Sitta kuwa ni kiongozi ambaye kwa sasa yuko juu na kwamba, hakuna atakayeweza kumgusa kwa lolote.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magomeni jijini Dar es Salaam jana, Sheikh Yahya alisema Sitta ataendelea kung'ara na kuibuka kidedea katika kutetea wadhifa wake huo baada ya uchaguzi mkuu kwa kuwa nyota yake ndivyo inavyoeleza.

  Alikuwa akitoa utabiri wa mambo mbalimbali ya kijamii na siasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

  "Sitta anaonekana kuwa bado kidedea, atang'ara na hakuna mtu atakayemgusa, nyota yake ndivyo inavyosema bado yuko juu,"alisema Sheikh Yahya.

  Hata hivyo alidai kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautakuwepo, kwani kutatokea machafuko makubwa nchini na mgawanyiko mkubwa visiwani Zanzibar utakaosababisha Rais Aman Karume aongezewe muda.

  Alisema Karume ataongezewa muda kwa kuwa machafuko hayo yatasababisha uchaguzi kutokuwepo lakini, hakuelezea upande wa Tanzania bara itakuwaje.

  Sheikh Yahya pia ametabiri kuwa Waziri Mkuu aliyeachia madaraka baada ya kutajwa katika kashfa ya Richmond, Edward Lowassa bado anang'ara pamoja na kwamba mwaka 2015 atajitokeza kugombea nafasi kubwa ya uongozi nchini.

  Alisema kuwa utabiri umeonyesha kuwa wakati Lowassa akiendelea kung'ara, viongozi maarufu wataendelea kufa kama alivyowahi kutabiri hapo awali.

  Sheikh Yahya alizungumzia pia CCJ kuwa kiliundwa kukiua CCM, lakini hakitafanikiwa kwa kuwa kilikosea nyota. Ili kifanikiwe kilipaswa kuitwa CCN.

  "Lakini CCJ wasiogope kuona vigogo wa CCM hawajahamia kwenye chama chao kwani utakapokaribia wakati wa uchaguzi kutotokea mmegeko mkubwa katika CCM na wabunge wengi watakihama," alisema Sheikh Yahya na kuongeza:

  "Wamekosea nyota, lakini wasiwe na hofu wakati wa uchaguzi ukifika wataona mmegeko mkubwa utakaotokea," alisema.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18763
   
Loading...