Sheikh Mussa Salum: Kijana kama huna uwezo usioe

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Akizungumza kwenye kipindi cha SUPERMIX East Africa radio.Sheikh Mussa Salum"amesema"Sheria ya dini inasema mwanamume kama hana uwezo wa kumnunulia mke mavazi, chakula na malazi asioe.

Nimejiuliza kwa njinsi vijana wengi hawana ajira Tanzania.Wakishikilia sheria hii kinadada wengi si watabaki wapweke sana?

Kina dada ambao hamjaolewa jiandaeni kisaikolojia Shekhe keshatoa tamko vijana wamebaki kutekeleza agizo tu.
 
Kwa hiyo wanawake kwenye uwezo shekhe semaje kuhusiana na hilo
 
Anasema kuwa sio vizuri kuoa alafu unamwacha binti wa watu hata mlo 1 tu shida,alafu we kila siku ni kumkwea tu....kwani amekuja hapo kuteseka???
 
Akizungumza kwenye kipindi cha SUPERMIX East Africa radio.Sheikh Mussa Salum"amesema"Sheria ya dini inasema mwanamume kama hana uwezo wa kumnunulia mke mavazi, chakula na malazi asioe.
Nimejiuliza kwa njinsi vijana wengi hawana ajira Tanzania.Wakishikilia sheria hii kinadada wengi si watabaki wapweke sana?
Kina dada ambao hamjaolewa jiandaeni kisaikolojia Shekhe keshatoa tamko vijana wamebaki kutekeleza agizo tu.
Sio uwezo huo ulioutaja tu, ni pamoja na uwezo wa nguvu za kiume, km huna uwezo wa kulimudu tendo bora usioe tu!
 
huyo shekhe ana mustawa (level) ndogo sana ya elimu ya dini hivyo kabla hajatoa fat'wa yambidi arejee mafundisho sahihi ya uislamu tena juu ya ufahamu wa wema walotangulia kisha ndo atoe fat'wa......nawanasih na wengineo ''jamani elimu ya dini ni taaluma pana sana hivyo inatubidi kuuliza maswali yetu kwa masheikh wenye taaluma na sio hawa masheikh wa media.....ingia website ya ALHIDAYA uliza swali na utajibiwa kwa kina ...hata msiokuwa waislamu tunawakaribisha alhidaya kuuliza maswali
 
Tatizo ndugu yangu watu wasio kuwa waislamu watadhani kuwa kiongozi wao kasema ndio hivyo. Mimi sina elimu ya dini lakini ni makosa kiongozi kutoa maoni yake binafsi yakawa ya kidini. Aibu kubwa. Unawaambia vijana wasiowe sababu ya umaskini. Kwa hiyo matajiri tu waowe na malofa wakae ni vimada. Kwa kweli nimechukizwa sana kama ni kweli kasema maneno haya.
 
Kasema kwa vijana woote bila kujali dinii sasa kijana jobless unashinda maskanihalafu unandoto zakuoa haya tumekuchangia umeoa sasa huyo mke utamtuza vepeee nahapo bado mjapata watoto mkiwa na watoto itakuaje na baba mtu waskani tu
 
Tatizo ndugu yangu watu wasio kuwa waislamu watadhani kuwa kiongozi wao kasema ndio hivyo. Mimi sina elimu ya dini lakini ni makosa kiongozi kutoa maoni yake binafsi yakawa ya kidini. Aibu kubwa. Unawaambia vijana wasiowe sababu ya umaskini. Kwa hiyo matajiri tu waowe na malofa wakae ni vimada. Kwa kweli nimechukizwa sana kama ni kweli kasema maneno haya.
Hajasema uwe tajiri bali anasema wale vijana wasio jishughulisha achana nawale wanaojipatia kipato kwa siku
 
Back
Top Bottom