Sheikh Mohammed Iddi: Hivi Dk Dau hana jema hata moja?

Status
Not open for further replies.

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156
UKURUGENZI MKUU NSSF 1997 – 2016

HIVI DOKTA DAU HANA JEMA HATA MOJA?

2016%2B-%2B1

Kabla ya kuanza kuandika chochote kuhusu maudhui yenye anuani hiyo hapo juu, niwakumbushe wasomaji wangu ‘kisa’ kimoja nilichohadithiwa na rafiki yangu ambaye alikishuhudia yeye mwenyewe katika nchi moja (sipendi kwa leo kumtaja wala kuitaja hiyo nchi).

Dereva wa gari ambaye ni mzaliwa wa nchi hiyo aligonga gari ya mwenzake ambaye ni raia wa kigeni kwa dhahiri shahiri. Huyu dereva mzalendo ndiye aliyevunja utaratibu lakini cha ajabu yeye akawa akimlaumu, akimgombesha na kumtukana matusi mazito mazito yule aliyemgonga.

Yule aliyegongwa baada ya kuona watu wamejaa katika eneo la tukio akauliza: “Jamani! Katika hali hii mimi hapa kosa langu ni lipi?” Yule mzalendo aliyemgonga akamjibu hivi (na hapa ndipo kwenye nukta ninayoikusudia): “Kosa lako wewe ni kuwepo hapa nchini petu kwani kama ungekuwa kwenu, Je ningekuja kukugonga huko?”.

Kisa hiki kinanikumbusha kwamba kuna baadhi ya makosa yanasababishwa na kumchukia tu mtu mwenyewe na wala si kuangalia kosa kama kosa katika mizania ya sheria.

Katika muktadha huo, ni vizuri tukajiuliza maswali kadha wa kadhaa juu ya ‘mlipuko’ wa baadhi ya wanahabari kumshambulia kwa kasi kubwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dokta Ramadhan Dau. Kulikonii? Au kosa lake ni kwamba alikalia mahala pa watu ambapo leo pamerudishwa kwa wenyewe?

Baadhi ya Watanzania wamestaajabishwa sana na ‘mlipuko’ huo mkubwa wa kumtangaza na kumshambulia Dokta Dau kwa tuhuma za ufisadi kwa sababu:

a) Hao ‘washika bango’ wa kuutangaza huo waliokwishauhukumu kuwa ni ufisadi hawaonekani kama wana lengo la kuhabarisha bali wamejipa kabisa mamlaka ya kuhukumu kwa kiwango ambacho hata hawakuhitajia kumhoji huyo wanayemtuhumu, jambo ambalo linaitia kasoro taarifa yao hiyo kwa jamii.

b) Wakati wanamjengea ‘kuchafuka’ huko katika jamii ya Kitanzania wamesahau kwamba ndio ‘wanamkejeli’ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli, kana kwamba hana vyombo makini vya kumpa taarifa na ‘akapotoka’ kwa kumteua kuwa Balozi mtu ambaye kwa mtazamo wao ni ‘mhalifu’ anayehukumiwa hata bila ya kustahiki kuulizwa na kujitetea.

c) Wakati washika bango hao wakikazia kumchafua Dokta Dau huku wakisahau kwamba katika uhalifu wowote ambao ni ‘shirikishi’ kumng’ang’ania mtu mmoja tu tena kwa kumtuhumu tuhuma nzito huku wakiwaacha wengine, ni dalili ya kuwepo ‘ajenda’ zilizofichwa nyuma ya mpango huo.

d) Washika bango hao wanastaajabisha kwa ufahamu wao juu ya taarifa za Dokta Dau lakini ‘wakazikalia’ mpaka alipoondolewa ndipo ‘wapumue’ kwa kuzitoa. Je, waliogopa nini kuzitoa hapo awali? Na kwanini sasa hawaogopi kuzitoa taarifa hizo?

Kama ni kweli kwamba chanzo chao kikuu cha taarifa ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) (Ripoti ambayo tayari Ofisi ya CAG imeshaikana), hivi Watanzania leo hii tumefikia kuifanya taarifa ya ukaguzi kuwa ndio hukumu halafu eti huo tuuite ndio utawala bora unaofuata sheria? Hivi Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inajadiliwa kwanza na wanahabari kisha wafikie au iwafikie watuhumiwa katika kadhia husika?

Amma kwa upande wa pili ndipo linapozalika swali ambalo huenda lingekuwa ndio ufumbuzi wa dhana ya chuki ‘binafsi’ dhidi ya Dokta Dau. Nayo ni kwamba huyo Dokta Dau aliyetumikia katika Shirika la NSSF kwa zaidi ya miaka kumi; hivi hana hata jema moja linalofaa kutangazwa?

Hivi jicho lenye uadilifu linaweza kuangalia mapungufu ambayo ni dhana na likawacha mafanikio ambayo ni hakika? Je, washika bango wanakitazama Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa mtazamo upi? Je, wanaitazama miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi inayofadhiliwa na NSSF kwa mtazamo upi? Je, wanalitazama Daraja la Kigamboni kwa mtazamo upi? Je, hayo na mengineyo kwa mtazamo wao ni mafanikio au mapungufu?

Hivi utendaji wa Dokta Dau katika Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutokea mwaka 1997 hadi 2016 mwanzoni, hakuna jema hata moja linalofaa kutamkwa kabla ya kupekua kinachoonekana kuwa ni mapungufu?

Watanzania lazima tuwe wakweli na kamwe tusiache kujifunza kutokana na msemo wa Waswahili usemao: “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.” Kitendo cha kusahau kabisa mambo mema na mafanikio ya Dokta Dau katika Shirika hilo, hapo ndipo inapopata nguvu ile dhana kwamba Waislamu katika Tanzania hawatarajiwi kuwa raia wa daraja sawa na wenzao wa dini nyengine.

Kwa hiyo, Muislamu ‘msomi’ katika Tanzania akishika wadhifa wowote katika serikali au shirika la umma hata kama atafanikisha mafanikio makubwa, anaonekana amefanikiwa kwa bahati mbaya tu kwa sababu sio matarajio Muislamu kutegemewa kuwa na uwezo katika utendaji.

Tumeshuhudia mara zote ambazo Waislamu wamekuwa viongozi wa juu katika nchi hii au katika idara, taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali wamekumbana na matatizo na vizingiti kadha wa kadhaa mpaka walipobadilishwa na kupewa ‘wenyewe’ nafasi hizo, hapo sasa ndipo utulivu hupatikana.

Katika nchi yenye uwiano wa kukaribiana kiidadi raia wake kiimani ni aibu kubwa kuona kila eneo katika idara, taasisi na mashirika ya serikali kujazwa na raia wa dini fulani na akipatikana mmoja tu wa dini nyengine katika idara, taasisi au shirika lolote la serikali ‘atachimbwachimbwa’ mpaka ang’olewe na akishang’olewa kwa sababu tu amekalia sehemu ya ‘watu’ atachafuliwa ili jamii iaminishwe kwamba alistahili kuondolewa.

Katika hali ya ubaguzi wa aina hiyo, Watanzania Waislamu wanajiuliza: Hivi kweli tatizo ni kuwa Waislamu ‘hawakusoma?'

Hivi kwa nchi iliyo huru kwa takriban miaka hamsini sasa yule aliyewabagua raia wake kwa misingi ya dini mpaka kundi moja likapewa fursa ya elimu na kundi jengine likanyimwa; Je, huyo ni mzalendo au ni mbaguzi? Na Je, ni kweli kwamba Waislamu hawakusoma? Je, hawa Waislamu waliofikia viwango vya kushika urais, uwaziri, ukatibu mkuu wa wizara, ukurugenzi na kadhalika, sio Watanzania?

Ukweli ni vizuri ukasemwa kwamba Dokta Dau ashukuriwe kwanza mpaka Watanzania wajiridhishe kwa mafanikio haya makubwa yanayoonekana kabla ya kugeukia hayo yanayoitwa mapungufu. Huo ndio uungwana na ndio ustaarabu.

Katika hali hiyo sio vyema kukaa kimya kwani jamii kama inavyobadilika kitabia basi inabadilika kiuvumilivu na viwango vya subra.

Hivi ni kweli Dokta Dau hana jambo jema hata moja katika utumishi wake kama Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kiasi cha kuandamwa na ‘kusulubiwa’ namna hiyo? Na kama lipo, basi litajwe kwanza kwa sababu jema lipo wazi na linaonekana lakini mapungufu ni dhana inayohitaji ushahidi uliothibitishwa katika vyombo husika.

Hii ndiyo kauli yangu ya wiki hii na mjadala uko wazi.

Mwandishi wa makala haya ni Mwenyekiti wa ARRISAALAH ISLAMIC FOUNDATION.

Unaweza kuwasiliana naye kwa namba: +255 754 299 749, +255 784 299 749.
 
Attachments

  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 45
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 45
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 43
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 55
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 44
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 38
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 55
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 47
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 39
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 47
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 46
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 48
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 33
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 47
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 43
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 46
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 40
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 47
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 44
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 42
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 44
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 45
  • upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    upload_2016-4-15_17-38-51.gif
    43 bytes · Views: 32
Ukifanya ufisadi, the least you can expect ni kuadhibiwa kwenye media. Tulia dawa iingie. Anavuna alichopanda.
 
Toka lini Muislam akawa na jema mbele ya wagalatia.
Kweli kabisa. Ndio maana hata nchi za kiislam kama Pakistan, Iran, Somalia nk zinapokuwa na shida wananchi wengi wanaishia kuomba ukimbizi Saudi Arabia na Falme za Uarabu na si Ulaya na Marekani!
 
Nanialikudanganya ULAYA na MAREKANI ni nchi za kikristo?? jidanganye,
 
Dau na Uislam mbona sioni kitu hapa! Basi Lugumi,Jk,Mramba wa Tanesco na n.k waandamwa kwasababu ni Waislam sio?! Acheni ujinga nyie watu.
 
Europians pia wanasema wameanza kuwa na roho za kibinadamu walipouacha ukristo! na hata vita vya wao kwa wao vikaisha. Unapokuwa mkristo unakuwa na zigo kubwa na chuki moyoni hasa dhidi ya muislam
Hahahahahaaa akili ndogo hoja dhaifu. Nenda kajiendeleze kielimu na wewe upate nafasi nyeti na muache kukaa vibarazani, kutegemea ushirikina, muache majungu,fitina na kuwa wavivu.
 
Jecha naye ni Muislamu! Ndio maana ukaunga mkono vitendo vyake vya ufedhuli. Masheikh wengine wanataka wasikilikane tu katika vyombo vya habari 24/7.
 
Nanialikudanganya ULAYA na MAREKANI ni nchi za kikristo?? jidanganye,
Duu na huyu alietoa au kuandika haya anaongoza waumini au ana kundi analoongoza? Kama ndio basi nimeelewa kwanini wenzetu wengi wao wana shida kwenye mambo yanayohitaji kutumia akili! Kama kiongozi ni wa aina hii unategemea wafuasi waweje?
 
Kwa hiyo kama kafanya mazuri,mabaya yake kama yapo yasijadiliwe?

Kila mtu ana haki ya kuchagua upande wa kuusemea kwa hiyo asiwatake watu wote washinde wakizungumzia mazuri tu ilhali mabaya yapo.

Siku akifa mazuri yake yatasemwa!!!
 
HIVI DOKTA DAU HANA JEMA HATA MOJA?

Kabla ya kuanza kuandika chochote kuhusu maudhui yenye anuani hiyo hapo juu, niwakumbushe wasomaji wangu ‘kisa’ kimoja nilichohadithiwa na rafiki yangu ambaye alikishuhudia yeye mwenyewe katika nchi moja (sipendi kwa leo kumtaja wala kuitaja hiyo nchi).

Dereva wa gari ambaye ni mzaliwa wa nchi hiyo aligonga gari ya mwenzake ambaye ni raia wa kigeni kwa dhahiri shahiri. Huyu dereva mzalendo ndiye aliyevunja utaratibu lakini cha ajabu yeye akawa akimlaumu, akimgombesha na kumtukana matusi mazito mazito yule aliyemgonga.

Yule aliyegongwa baada ya kuona watu wamejaa katika eneo la tukio akauliza: “Jamani! Katika hali hii mimi hapa kosa langu ni lipi?” Yule mzalendo aliyemgonga akamjibu hivi (na hapa ndipo kwenye nukta ninayoikusudia): “Kosa lako wewe ni kuwepo hapa nchini petu kwani kama ungekuwa kwenu, Je ningekuja kukugonga huko?”

Kisa hiki kinanikumbusha kwamba kuna baadhi ya makosa yanasababishwa na kumchukia tu mtu mwenyewe na wala si kuangalia kosa kama kosa katika mizania ya sheria.

Katika muktadha huo, ni vizuri tukajiuliza maswali kadha wa kadhaa juu ya ‘mlipuko’ wa baadhi ya wanahabari kumshambulia kwa kasi kubwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dokta Ramadhan Dau. Kulikonii? Au kosa lake ni kwamba alikalia mahala pa watu ambapo leo pamerudishwa kwa wenyewe?

Baadhi ya Watanzania wamestaajabishwa sana na ‘mlipuko’ huo mkubwa wa kumtangaza na kumshambulia Dokta Dau kwa tuhuma za ufisadi kwa sababu:

a) Hao ‘washika bango’ wa kuutangaza huo waliokwishauhukumu kuwa ni ufisadi hawaonekani kama wana lengo la kuhabarisha bali wamejipa kabisa mamlaka ya kuhukumu kwa kiwango ambacho hata hawakuhitajia kumhoji huyo wanayemtuhumu, jambo ambalo linaitia kasoro taarifa yao hiyo kwa jamii.

b) Wakati wanamjengea ‘kuchafuka’ huko katika jamii ya Kitanzania wamesahau kwamba ndio ‘wanamkejeli’ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli, kana kwamba hana vyombo makini vya kumpa taarifa na ‘akapotoka’ kwa kumteua kuwa Balozi mtu ambaye kwa mtazamo wao ni ‘mhalifu’ anayehukumiwa hata bila ya kustahiki kuulizwa na kujitetea.

c) Wakati washika bango hao wakikazia kumchafua Dokta Dau huku wakisahau kwamba katika uhalifu wowote ambao ni ‘shirikishi’ kumng’ang’ania mtu mmoja tu tena kwa kumtuhumu tuhuma nzito huku wakiwaacha wengine, ni dalili ya kuwepo ‘ajenda’ zilizofichwa nyuma ya mpango huo.

d) Washika bango hao wanastaajabisha kwa ufahamu wao juu ya taarifa za Dokta Dau lakini ‘wakazikalia’ mpaka alipoondolewa ndipo ‘wapumue’ kwa kuzitoa. Je,waliogopa nini kuzitoa hapo awali? Na kwanini sasa hawaogopi kuzitoa taarifa hizo?

Kama ni kweli kwamba chanzo chao kikuu cha taarifa ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) (Ripoti ambayo tayari Ofisi ya CAG imeshaikana), hivi Watanzania leo hii tumefikia kuifanya taarifa ya ukaguzi kuwa ndio hukumu halafu eti huo tuuite ndio utawala bora unaofuata sheria? Hivi Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inajadiliwa kwanza na wanahabari kisha wafikie au iwafikie watuhumiwa katika kadhia husika?

Amma kwa upande wa pili ndipo linapozalika swali ambalo huenda lingekuwa ndio ufumbuzi wa dhana ya chuki ‘binafsi’ dhidi ya Dokta Dau. Nayo ni kwamba huyo Dokta Dau aliyetumikia katika Shirika la NSSF kwa zaidi ya miaka kumi; hivi hana hata jema moja linalofaa kutangazwa?

Hivi jicho lenye uadilifu linaweza kuangalia mapungufu ambayo ni dhana na likawacha mafanikio ambayo ni hakika? Je, washika bango wanakitazama Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa mtazamo upi? Je, wanaitazama miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi inayofadhiliwa na NSSF kwa mtazamo upi? Je, wanalitazama Daraja la Kigamboni kwa mtazamo upi? Je, hayo na mengineyo kwa mtazamo wao ni mafanikio au mapungufu?

Hivi utendaji wa Dokta Dau katika Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutokea mwaka 1997 hadi 2016 mwanzoni, hakuna jema hata moja linalofaa kutamkwa kabla ya kupekua kinachoonekana kuwa ni mapungufu?

Watanzania lazima tuwe wakweli na kamwe tusiache kujifunza kutokana na msemo wa Waswahili usemao: “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.” Kitendo cha kusahau kabisa mambo mema na mafanikio ya Dokta Dau katika Shirika hilo, hapo ndipo inapopata nguvu ile dhana kwamba Waislamu katika Tanzania hawatarajiwi kuwa raia wa daraja sawa na wenzao wa dini nyengine. Kwa hiyo, Muislamu ‘msomi’ katika Tanzania akishika wadhifa wowote katika serikali au shirika la umma hata kama atafanikisha mafanikio makubwa, anaonekana amefanikiwa kwa bahati mbaya tu kwa sababu sio matarajio Muislamu kutegemewa kuwa na uwezo katika utendaji.

Tumeshuhudia mara zote ambazo Waislamu wamekuwa viongozi wa juu katika nchi hii au katika idara, taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali wamekumbana na matatizo na vizingiti kadha wa kadhaa mpaka walipobadilishwa na kupewa ‘wenyewe’ nafasi hizo, hapo sasa ndipo utulivu hupatikana.

Katika nchi yenye uwiano wa kukaribiana kiidadi raia wake kiimani ni aibu kubwa kuona kila eneo katika idara, taasisi na mashirika ya serikali kujazwa na raia wa dini fulani na akipatikana mmoja tu wa dini nyengine katika idara, taasisi au shirika lolote la serikali ‘atachimbwachimbwa’ mpaka ang’olewe na akishang’olewa kwa sababu tu amekalia sehemu ya ‘watu’ atachafuliwa ili jamii iaminishwe kwamba alistahili kuondolewa.

Katika hali ya ubaguzi wa aina hiyo, Watanzania Waislamu wanajiuliza: Hivi kweli tatizo ni kuwa Waislamu ‘hawakusoma?'

Hivi kwa nchi iliyo huru kwa takriban miaka hamsini sasa yule aliyewabagua raia wake kwa misingi ya dini mpaka kundi moja likapewa fursa ya elimu na kundi jengine likanyimwa; Je, huyo ni mzalendo au ni mbaguzi? Na Je, ni kweli kwamba Waislamu hawakusoma? Je, hawa Waislamu waliofikia viwango vya kushika urais, uwaziri, ukatibu mkuu wa wizara, ukurugenzi na kadhalika, sio Watanzania?

Ukweli ni vizuri ukasemwa kwamba Dokta Dau ashukuriwe kwanza mpaka Watanzania wajiridhishe kwa mafanikio haya makubwa yanayoonekana kabla ya kugeukia hayo yanayoitwa mapungufu. Huo ndio uungwana na ndio ustaarabu.

Katika hali hiyo sio vyema kukaa kimya kwani jamii kama inavyobadilika kitabia basi inabadilika kiuvumilivu na viwango vya subra.

Hivi ni kweli Dokta Dau hana jambo jema hata moja katika utumishi wake kama Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kiasi cha kuandamwa na ‘kusulubiwa’ namna hiyo? Na kama lipo, basi litajwe kwanza kwa sababu jema lipo wazi na linaonekana lakini mapungufu ni dhana inayohitaji ushahidi uliothibitishwa katika vyombo husika.
Hii ndiyo kauli yangu ya wiki hii na mjadala uko wazi.

Mwandishi wa makala haya ni Mwenyekiti wa ARRISAALAH ISLAMIC FOUNDATION.
Unaweza kuwasiliana naye kwa namba: +255 754 299 749, +255 784 299 749
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom