Sheikh mkuu wilayani Tunduru ashambuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh mkuu wilayani Tunduru ashambuliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  THURSDAY, OCTOBER 25, 2012

  [​IMG]
  Sheikh mkuu Wilayani Tunduru Alhaji Waziri Chilakweche akiwa hospitali
  [​IMG]
  Rajab Abdalah (17)

  --

  Na Steven Augustino,Tunduru


  Watu wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu wenye msimamo Mkali wa Dini wamemvamia na kumpiga Shekh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilayani Tunduru Alhaji waziri Chilakweche na kumsababishia maumivu makali.


  Kabla ya tukio Shekh huyo alifatwa nyumbani kwake na vijana na kumuomba watoke nae nje ya eneo la nyumba yake wakidai kuwa wanaomba awasaidie kusuluhisha Mgogoro uliokuwa umezuka katika msikiti wa Kitumbini katika Mtaa huo.


  Sambamba na tukio hilo pia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajab Abdalah (17) Amelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru akiwa hajitambui baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu ambao walidaiwa kukimbilia katika tukio la shambulizi la Shekh Chilakwechi.


  Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane kuamkia leo ambapo katika madai yao vijana hao walimtuhumu Alhaji Chilakwechi kuwa amekuwa akishiriki na kula vyakula vya wakirsto.


  Akiongea kwa taabu Alihaji Chilakwechi alidai hakuwa na ubaya nao na wala hajwahi kugombana na mtu hali ambayo inamshangaza na anaiomba Serikali ifuate mkondo wake kwa wahusika.


  Kuhusu tuhuma za yeye kushiriki katika shughuli za dini katika madhehebu ya wakristo alidai kuwa hicho siyo kitu cha ajabu kwa viongozi wa dini na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini huwa na ushirikiano na huitana na kutembeleana kwa vile dini hairuhusu uhasama miongoni mwao.


  Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedth Nsimekli amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshji la polisi linaendelea na uchunguzi ili kujua kiini cha tukio hilo.


  Aidha kamanda Nsimeki alikiri pia kufahamu matukio ya udini yanayo endelea Wilayani Tunduru nakuongeza kuwa jeshi limejipanga kuhakikisha kuwa wanadhibiti vitendo hivyo.


  THURSDAY, OCTOBER 25, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  This is too MUCH...
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  pole shekh....mbegu ya udini ilipandwa na sasa imekua na kuzaa mtoto (uamsho).....


  kuna kundi la waislam wana mpango wa kuwamaliza mashekh wa bakwata nini???
   
 4. don12

  don12 JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 676
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  waislam wenye msimamo mchafu hamna akili,mbona mnakuwa kama mashetani?
   
 5. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Hayawi hayawi! Yamekuwa. Ccm imelea na kutukuza udini na sasa dhambi hiyo inawatafuna
   
 6. d

  danizzo JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bado issa bin simba
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ASANTE kwa UFUMBUZI.. Hiyo Habari IMETOKEA LEO? NIPE LINK nitaiweka SASA hivi...
   
 8. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,596
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Kidogo kidogo tunakuwa wazoefu wa kumwaga damu, shehe kalipuliwa na bomu Arusha huyu naye kakatwa mapanga, ni wazi kila mwislamu anayeshirikiana na wakristo anakuwa hatarini, SERIKALI mpo wapi?
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yaani sheikh anapigwa kwa sababu anatembeleana na wakristo...kwa waislam wanatakaje kwamba wao wawe na maisha yao na sehemu yao wenyewe na wakristo wawe na mitaa yao na wawe wao wenyewe ama shida iko wapi? kama waislam wanampiga sheikh wao hivi watakua na huruma na madhehebu mengine? huku tunakoelekea huku? Hongera Jakaya umetimiza ndoto zako sasa nchi iko kwenye mgawanyiko wa kidini....are you happy now?
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  waislam hua wanaswali sijui mara 6 kwa siku....hua mara zote hizo mnasali nini...kwamba mue na chuki na watu wenye madhehebu mengine, hua mnasali kua mkiamka asubuhi mpate nguvu za kuchoma makanisa na kuchinja polisi mara zote hizo sita hua mnasaligi na kuombea nini hasa?
   
 11. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,275
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  kazi ipo
   
 12. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii siyo vita ya udini, ni shetani kamili.
   
 13. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kata ninayotoka (by the time nikiwa mdogo) kulikuwa na familia tano tu zenye waumini wa Kiislamu ( and remember I mean kata nzima sio kitongoji au kijiji). Walikuwa wana-rotate weekly kusali ijumaa. Uongozi wa kata (wote wakristo) ukaamua kuwasaidia kujenga msikiti kwenye makao makuu ya kata (ambapo palikuwa centrally located)
  Wakazi wote wa kata walishiriki kujenga huo msikiti, na hakuna alieathirika. Leo iweje sheikh apigwe kwa kwenda kushirikiana na wakristo? Ukisikia ugonjwa wa akili ndio huu!
   
 14. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ziwekwe na nani sasa, kama unazo si uweke, au ndo ubishi wenyewe.
   
 15. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Waislamu wenye msimamo mkali i.e(farida na ponda =magaidi
   
 16. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  duh tanzania inakoelekea na huu udini sielewi.........
   
 17. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Huyu mungu wa machafuko si Mungu wetu.

  Sent from my LT26i using Tapatalk 2
   
 18. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  walikuwa wanapanda walidhani mbegu hazioti, sasa zimeota na kibaya zaidi zimeota wakiwa hai.
  kuzing'oa shughuli ipo, wale jamaa waliokuwa wakihubiri pale Morogoro wakati wa kampeni 2010, kwa kusema kanisa katoliki litaleta vita sasa tunawatyaka waseme limeleta wapi vita.
   
 19. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Edson tuache waislamu tutiane adabu wenyewe hayakuhusu.
   
 20. n

  ngogo JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 359
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa suni ni waislam kweli, hivi kumwaga damu ya binadamu ndio ibada yao? Kweli japo mimi ni muislam lakini nakiri kwamba Yesu ni kiboko alishasema saa watawaua wakidhani wanamtolea mungu sadaka.
   
Loading...