GE2025 Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar: Tukikubali kuvunja amani tutamwambia nini Mungu?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Bin Zubeir Ally, amewataka Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, maadili na ustawi wa jamii, hasa katika kipindi hiki ambapo Taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025

Akizungumza mbele ya waumini wa Kiislamu katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Sheikh Dkt. Abubakar amesema amani ndiyo msingi wa Uislamu na chachu ya maendeleo ya jamii yoyote, akisisitiza kwamba Waislamu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha utulivu, mshikamano na maadili vinaendelea kudumishwa nchini

Aidha, kiongozi huyo wa dini amezungumzia changamoto ya mmomonyoko wa maadili unaoikabili jamii, akibainisha kuwa malezi ya watoto katika misingi ya dini na maadili ya taifa ndiyo ngao pekee ya kulinda kizazi kijacho dhidi ya athari hizo

Amewataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao kwa misingi ya dini, heshima na upendo ili kulinda tunu za Taifa

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, amewataka wananchi wote wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi mkuu ili kutimiza haki yao ya kikatiba


Your browser is not able to display this video.
 
Amani gani anaisemea ... Wasimuingize Mungu kwenye mambo ya kipuuzi
 
Tarehe 29 tunatoka kuandamana. Unataka ni hivyo hivyo, hutaki ni hivyo hivyo!
 
TUNAIVUNJA AMANI ILI TUANZE UPYA ,UKWELI NA HAKI IKIWA NDIP MSINGI WA KILA KITI
 
Hivi Hawa mashehe kwa nini wanajitoa ufahamu kiasi hiki?

Amani ni tunda la haki,kama hakuna haki hakuna amani. Mbona hawahubiri haki ambayo ni shina la mema na uadilifu linalozaa "amani" wanayoihubiri majukwaani?

Ngoja nimpe mfano Shehe;

Wakati nakua,nipo Chalii, siku Moja tulitoka na Bro kwenda shambani/porini kuokota maembe. Jumla tulikuwa watano(Mimi na wenzangu watatu na bro ambaye ni mkubwa kwetu akituongoza).

Tukipata maembe mengi ile siku.

Muda wa kugawana ili Kila mmoja asepe na chake turudi home,Bro alichokifanya ni kujichagulia maembe mazuri na makubwa alafu mengi kisha akatuachia Yale yaliyobaki tugawane.

Kile kitendo Kila mmoja wetu kilimuuma,kwa nini bro ajichagulie maembe mazuri na mengi alafu atuachie mabaya tugawane wanne? Kisa wadogo? Tukawa tumestuck bila kufanya chochote Huku suds zimefura.

Jamaa akauliza "mbona hamgawani tusepe,muda umeenda?"

Dogo mmoja akasema "kaka umetuachia maembe ya hovyo siyo sawa,Hatuwezi kugawana embe za hivi"

Sasa mnatakaje?

Tukamjibu 'rudisha maembe yote kisha tugawane kwa haki,Kila mmoja aridhike. Usitukandsmize kisa sisi ni watoto"

Akarudisha kisha akaweka system Kila mmoja anachagua embe analoona linamfaa kisha anafata mwingine hadi mzunguko uishe...hadi maembe yote yaishe.

Pale Kila mmoja alitoka anafuraha mana tuligawana kwa haki hadi embe la mwisho. Na kuanzia siku ile ukawa ndiyo utaratibu wetu,bila kuangalia cheo Wala ukubwa.

Umeona faida ya HAKI KABLA YA AMANI?

1.Bro alifanya u babe kama serikali na sisiem wanavyofanya.

2.Tukareact(kudai haki sawa)

3. Bro aliona tunaleta fujo(tunavunja amani)

4. Baadae alibadilika akasema sawa tugawane kwa haki.

5. Amani ikarejea tukarudi home salama Huku tunafufahi pamoja.

HUBIRINI HAKI MAJUKWAANI NA MADHABAUNI,AMANI ITAKUJA AUTOMATIC BILA VITISHO.
 
Kwa Mungu maswali huhusiana na "haki" si "amani."

Ritz, Malaria 2 kwani kule Gaza kinachogomba haki au amani? Kwani huyu shehe wenu ni wale wa ubwabwa?
 
Jinga kabisa kabisa 😤😡👺
 
HUYU SHEIKH ANAMZUNGUMZIA MUNGU GANI?! AU MUNGU WAO WA MACHAWA?
 
Hakuna wa kuvunja amani bali ni wa kutaka haki. Wanaovunja haki ndio wanaovunja amani
 
Una vituko wewe.
Kweli utatoka ukaandamane, au unasukumiza wenzio tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…