Sheikh Kipozeo ndani ya Take One ya Clouds TV

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Nimecheka sana, na hakika sitaikosa hii!

Leo Jumanne, saa 3 usiku sheikh Al-Habib Hilal Kipozeo atakuwa mgeni kwenye msimu mpya wa kipindi cha Bongo Movie (Take One, New Chapter) akizungumzia masuala mbalimbali ya kinyumba baina ya mke na mume.. Patamu hapoooo!

Kwenye Jingle ambayo Mtangazaji Zamaradi Mketema anaonekana mwenye furaha na kutabasamu kwa maneno ya muhadhir huyu, Kipozeo anasikika akisema, ''Wanawake wametofautiana, kuna mwingine fundi zaidi, awe mtundu mtundu chumbani, mwenye kukuridhisha wewe... Naam''!

Sheikh huyu ni maarufu kutokana na uwasilishaji wake wa mawaidha kwa lugha lainiiiii..
 
hahahahahahahhaha...mzeee wa mizigoooo........nyie pendeni wembamba tu...yaani mamisss...mimi napenda ile mizigo sheikh...iliyojazia neema za allah sheikh...yaani miss bantu
 
Hebu tupieni basi baadhi ya vijipande vya video zake tuone kabla hatuja mkimbilia leo usiku.
 
Mashehe wote wangeubili kama huyu hakika uislam ungekuwa dini ya kila mtu kuikimbilia. Napenda kumsikiliza anahubiri mazuri, rehema uzuri wa uislam. Wengine ni vitisho na kuitana majina mabaya.
Indeed!
 
Back
Top Bottom