Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya Tanzania, linaunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kupambana na dawa za kulevya
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa amesema baraza linapinga na kulaani hatua yoyote ya kushiriki katika biashara na utumiaji wa dawa za kulevya
"Tunampongeza kwa dhati kabisa Mkuu wa Mkoa kwa ujasiri aliouonyesha kwa kuwa ameamua kujitoa mhanga kwa ajili ya Taifa", amesema.
Chanzo: Mwananchi