Shehena la vifaa vya Serikali lakamatwa mkoani Pwani

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
21,381
Reaction score
55,972
Serikali mkoani Pwani, imekamata shehena ya miundombinu mbalimbali ya serikali iliyoibiwa na kuhifadhiwa katika kiwanda cha kutengeneza vifaa vya ujenzi Mkuranga mkoani Pwani.

Miundombinu hiyo imekamatwa baada ya kuundwa kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia uharibifu wa miundombinu uliyokuwa ukifanyika katika taasisi mbalimbali ikiwemo TANESCO.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, ameongozana na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo kukagua miundombinu hiyo ambayo imebainika kuwa ni ya TANESCO, DAWASA na Shirika la Reli (TRC).

"Hatutavumilia yeyote atakayehusika kurudisha nyuma maendeleo ya Serikali tutafuatilia tujue nani anayehusika katika hili," amesema Kunenge.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kiwanda cha LN Feature Building Material kilichopo Mkuranga, ilipokutwa miundombinu hiyo Kunenge amesema wapo wananchi wanaisaliti serikali yao na kuhujumu miundombinu inayosambaza huduma.

Kunenge amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada ya kuboresha miundombinu lakini bado wapo wachache wanaohujumu na kurudisha nyuma maendeleo kwa kufanya uharibifu.

#EastAfricaTV
 
Kamata mwizi meen...

..Ni Hayo Tu!!

.
 
China angekutwa mtu na vifaa hivyo ni kifo tu matokeo yake ni nchi ya kupigiwa mfano kwa maendeleo duniani.

Maendeleo hayaji kwa kucheka na kima tena katika nchi yenye wajinga wengi.
 
Back
Top Bottom