Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Shaweji Mkumbura, ametoa wito kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025, akisisitiza kuwa nafasi pekee isiyopaswa kuwania ni ya Urais ambayo tayari imekwishapatiwa mgombea ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan
Akizungumza janaJuni 17, 2025, katika mkutano maalum wa usomaji na utekelezaji wa Ilani ya CCM, uliofanyika Kinondoni, Mkumbura aliwahimiza wana-CCM kutathmini dhamira zao kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kisiasa, akibainisha kuwa uongozi ni dhamana ya muda inayohitaji moyo wa kujitoa na mapenzi kwa wananchi
“ Fanyeni mnachofanya kama Mungu hajaweka mkono haiwi
Niwaombe Wana Mikocheni Tusilazimishe Mapenzi ya Mungu, Tusiseme Liwalo na Liwe, Liwalo na Liwe lipo kwa CCM tu,” alisema Mkumbura
Aidha, alitumia fursa hiyo kukinadi Chama Cha Mapinduzi kwa kueleza kuwa kimetekeleza Ilani yake kwa kiwango kikubwa, hali inayokifanya kuaminika zaidi mbele ya wananchi na hivyo kuwa na nafasi nzuri ya kuungwa mkono tena katika uchaguzi ujao
Mwisho, alitoa wito kwa wana-CCM kuendelea kushikamana na kudumisha mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu, huku wakisimama kidete kuendeleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan