Shauri la CHADEMA Mahakama Kuu Mwanza

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Leo Juni 15, 2016, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kwa niaba ya chama, kupitia kwa mawakili Gasper Mwanalyela, Paul Kipeja na John Malya, amewasilisha maombi manne Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, yote yakihusu kutafuta haki ya wananchi kukusanyika na kutoa maoni yao dhidi ya zuio lililowekwa na amri ya Jeshi la Polisi.

Katika shauri hilo la madai, namba 6 la mwaka 2016, Mwenyekiti Mbowe kupitia maombi hayo, ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza KUTAMKA, kwamba amri iliyotolewa na OCD wa Wilaya ya Geita kuzuia mikutano iliyopaswa kufanyika Katoro na Geita Mjini kuwa si sahihi na iliyo kinyume cha sheria.

Ombi jingine ni kuiomba Mahakama KUTENGUA amri ya OCD wa Geita ya aliyoitoa Juni 7, 2016 kuzuia mikutano ya CHADEMA kwa muda usiojulikana iliyokuwa imetangazwa na kupangwa kufanyika wilayani humo kuanzia tarehe hiyo.

Aidha ameiomba MahakamaKUMZUIA OCD huyo asitoe tena amri zilizo kinyume cha sheria dhidi ya CHADEMA na suala la nne ni kuiomba MahakamaKUMUAMURU OCD wa Geita afuate na kuzingatia sheria kwa kuruhusu mikutano ya CHADEMA ifanyike katika wilaya yake.

Tofauti na maombi yaliyokuwa katika shauri la awali namba 79 la mwaka 2016, yaliyowasilishwa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Juni 10, mwaka huu, katika shauri la sasa lililowasilishwa leo, washtakiwa watakuwa ni wawili, OCD wa Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Inatarajiwa kuwa maombi madogo, kwa ajili ya kusikilizwa kwa maombi ya msingi, yatasikilizwa Jumatano, Juni 16, 2016 mbele ya Jaji atakayekuwa amepangiwa shauri hilo.

Makene
 
Back
Top Bottom